Kigoma: Watu 6 wa familia moja wauawa kikatili usiku wa kuamkia Julai 3

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,229
4,554
Watu sita wa familia moja wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili na Watu wasiojulikana katika Kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma Mkoani Kigoma.

Familia hiyo ya Mussa Cheche kwa sasa waliobaki hai ni Mtoto mwenye umri wa miaka 4 ambaye amejuruhiwa na Mtoto mwingine mdogo wa miezi minne ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Kigoma Menrad Sindano amesema chanzo bado hakijafahamika.

Kamanda Sindano amesema “Hawa Watu wote wameuawa wakiwa wamelala kwenye vitanda vyao si mauaji ya Mtu mmoja au wawili na kuna vyumba vitatu na miili hiyo imekutwa kwenye vyumba hivyo, na inaonekana wauaji ni zaidi ya Mtu mmoja, uchunguzi bado unaendelea, msako mkali unafanyika kuhakikisha wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria”

Chanzo: Millard Ayo
 
kigoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo inamatukio ya Kijambazi/kihalifu, na hiyo inachangiwa zaidi na mwingiliano kati ya warundi na wakongo.

Ni Mkoa unao ongoza kuwa na wahamiaji haramu wengi ambao wanaishi kiholela bila kuwa na vibali, kuna warundi na wakongo wengi ambao wamefanya uhalifu ktk nchi zao na kukimbilia Kigoma, hivyo usalama wa wananchi wa Kigoma kuwa mashakani.

Vyombo vya ulinzi na usalama havina budi kufanya operesheni ya kusfisha kabisa wahamiaji haramu ktk Mkoa huo ambao wamekuwa tishio kwa usalama wa raia na mali zao.
 
Back
Top Bottom