Kigogo wa madawa ya kulevya wa kike, akamatwa na madawa ya kulevya

billduke

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
860
898
Hawa wadada wa mjini kujifanya wanauza nguo na simu kumbe uongo tu mwingine akamatwa....

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji' mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.

Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.

Christina Naphtali Kigaye akiwa katika kituo cha polisi.

Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.

"Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.

Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.

"Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani," alisema Kamanda Nzowa.

Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
 
ImageUploadedByJamiiForums1415079388.393438.jpg mdada mwenyewe ndio huyo
 
hawakumkamata na sembe (kidhibiti) wamemkamata kama mtuhumiwa,
walitakiwa waendelee kucheza naye kufatilia nyendo zake,kusikiliza simu zake pengine kuna vigogo zaidi yake,network nzima ingewezekana kuishika kama huyo dada ni mtu wa kati.
kama hawana kidhibiti wakuu tusubiieni uchunguzi ukamilike wa kumtia hatiani ,maana anaweza pia akagundulika hana hatia
 
Kukamatwa not a deal watuambie nayalemmadawa yanaendagawapi???

ukimsifia babayako kwa kukuzaaa msifie na aliemkimbiza.......
 
Hawa wadada wa mjini kujifanya wanauza nguo na simu kumbe uongo tu mwingine akamatwa....

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania kumkamata mfanyabiashara bilionea Mharami Mohamed Abdallah ‘Chonji’ mkazi wa Magomeni, Mtaa wa Kondoa jijini Dar akidaiwa kukutwa na unga, jeshi hilo linamhenyesha anayedaiwa kigogo mwingine wa unga ambaye ni mwanamke.Christina Naphtali Kigaye mkazi wa Mikocheni anayehusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kamanda wa kitengo hicho, SACP Godfrey Nzowa, wiki iliyopita aliimbia Uwazi kwamba mwanamke huyo, Christina Naphtali Kigaye (pichani), mkazi wa Mikocheni, Dar alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi lake.

Kamanda Nzowa alisema, Christina amekuwa akitajwa na watu wengi wanaokamatwa na unga kuwa, yeye ndiye kigogo wa unga na amekuwa akiwabebesha mzigo na kuwatuma sokoni nje ya nchi.

Christina Naphtali Kigaye akiwa katika kituo cha polisi.

Kamanda Nzowa alisema siku ya tukio kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar, saa tatu asubuhi ya Oktoba 29, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akitokea nje ya nchi alinaswa baada kitengo chake kutonywa na watuhumiwa wengine ambao tayari wameshakamatwa lakini wakawa wanaijua ratiba yake.

“Pamoja na kwamba anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza nguo na simu lakini hizo amejiegesha tu. Kwa mujibu wa watuhumiwa waliokamatwa na unga wamemtaja kwa asilimia kubwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.

Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.

“Kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi yake na utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kumpandisha mahakamani,” alisema Kamanda Nzowa.

Habari zaidi kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mwanamke huyo alipelekwa makao makuu ya kitengo cha kuzuia madawa hayo Kilwa Road na kuhojiwa maswali mengi ambayo yalimtoa jasho.
kukamatwa mbwembwe nyingi na maelezo kibao kuonyesha polisi wamefanya kazi. ngoja basi kama atafungwa mtu! hata kwenye magazeti kama utasikia kuna mtu anafuatilia kesi. chezea pesa..rushwa inji hii usiseme
 
hata kama ataachiwa kesi hamna cha kitendo cha kuwa mtuhumiwa kinamfanya asiwe comfortable tena!!
 
Back
Top Bottom