Nabii kiboko ya wachawi aingia mtegoni na kuthibitika kua kweli ni tapeli baada ya Mwandishi kutoka Mwananchi Digital kupiga simu kwa kiboko ya wachawi na kujifanya mgonjwa na kiboko ya wachawi aliomba shilingi milioni kumi ili amponye.

Licha ya Serikali kulifungia Kanisa la Christian Life (CLC), lililoongozwa na Dominique Dibwe maarufu kama ‘Kiboko ya Wachawi’, imebainika kiongozi huyo wa dini anaendelea kutoa huduma hiyo, huku akiomba mamilioni ya fedha kwa waumini wake.

Tofauti na awali, Dibwe ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) kwa sasa anatoa huduma ya maombezi na kile anachokiita uponyaji kwa njia ya simu, akiomba kulipwa mamilioni hayo kwa waumini wenye matatizo.
Soma pia

>Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali
Hivi kwanini kina mwamposa hawakamatwi
 
Hawa Manabii na waganga ni matokeo ya mfumo wetu wa huduma za afya kushindwa!

Magonjwa yenye majina ya watu kwenye hospitali zetu utakufa hujui unachoumwa ni ugonjwa gani
 
MASHETANI WAMEIINGILIA DINI YA KIKRISTO NA WANATAKA KUIANGUSHA, NI BUDI WAKRISTO KUSIMAMA IMARA KUISIMAMIA DINI HII, SHETANI APOKONYWE DINI YETU, IRUDISHWE KWENYE MSINGI YAKE MIKUU, THANKS SO MUCH MASAUNI ZIDI KUFUNGIA MATAPELI HAYA, MAJIZI!
Ashakum si matusi, shetani alishaharibu hiyo dini toka ilipotawazwa rasmi kuwa ni dini ya taifa la kirumi, ila hamtaki tu kuuona ukweli! Mnachokijua sasa katika ukristo na Yesu ni kile walichotaka warumi mkijue na kuamini.

Na kama unabisha hebu rejea sababu zilizopelekea kupatikana kwa protestants from the main christian Church (RC). Kuna sababu za kiimani na kuna sababu za kiutawala.
 
Back
Top Bottom