Kiba na Diamond wagoma kuimba wimbo wa hamasa kwa Serengeti Boys

Uzalendo ni kujitoa kwaajili ya manufaa ya nchi yako!

kwani kutoa wimbo wataifa uwape vijana inacost bei gani?

Tuweke tofauti zetu pembeni tulisaidie taifa
Wimbo ndo unacheza uwanjani? Wimbo ndo unafunga magoli?? Uzalendo uonyweshe na Chama cha Soka na Wachezaji acheni kutafta wa kumtupia Lawama andaeni timu
 
kwakweli hawajakosea aliyewaunganisha ni Nape na hayupo wagome tu kuimba kwani lazima msiwapangie
 
haafuu..nnekumbuka..hivi..ile ishu ya mwakyembe kuwaita kiba na diamond kule dom ili awapatanishe....iliishiaje...???
nianzie hapo kwanza...!!!
 
kwani lazima waimbe wimbo wa pamoja?!

Haiwezekani kila mtu akaimba kivyake vyake?
 
Hapa ndipo nashindwa kuamini kwamba kweli serikali imeondoa viroba.! Hii akili uliyo itumia kuleta hii mada ni ya viroba kabisaa.
 
Naunga hoja kabisa kama ni kweli wamegoma. Ikiwa rais w TFF kapoteza pesa zaidi ya billions 1
 
Teheeeee teheee Mpoto na Wanne Star ndio watu muafaka kwenye suala hili,sipati picha mmoja angekubali na mwingine akakataa hii thread ingekua na urefu wa treni ya Kigoma wapuuzi na timu zao wangecharuana hapa mpaka aibu ila leo wameungana bila kujua hakika hizi timu zinawapenda wasanii wao.
 
Uzalendo ni kujitoa kwaajili ya manufaa ya nchi yako!

kwani kutoa wimbo wataifa uwape vijana inacost bei gani?

Tuweke tofauti zetu pembeni tulisaidie taifa
Uzalendo pia ni pamoja na kuonyesha kwamba Ryan Babel hampendi Jodoki Kalimilo na hayupo tayari kufanya nae kazi pamoja kwa sasa mpaka hapo moyo utakapoamua na si kwa shinikizo la watu....mkilazimisha huo utakuwa sio uzalendo bali ni unafiki
 
Dito ndio mtaalamu wa hivyo vitu angepewa hiyo Kazi ingenoga kama angeifanya na v money.waaacheni kiba na chibu walinde biashara zao kwani siku watayoshirikiana watakuwa wameua ule upinzani wao ambao ndio unawapa hela ya kula mjini
 
Back
Top Bottom