Kiapo cha Baraza la Mawaziri na ukimya wa Lowassa!

Wampeleke mahakama mashaidi wapo akina LEMA, SLAA, LISU, MNYIKA, MDEE NA MBOWE kwani kwa vinywa vyao walisema wana ushahidi wakuprove LOWASA ni fisadi (video zipo YouTube, sijui mtazikataa, manake unafiki ndio asili yenu). Najua upinzani ni wazalendo kama vipi walisaidie taifa, bila kumsahau shahidi mwengine KUBENEA kupitia gazeti lake la MWANAHALISI , kwa miaka minane alikuwa akiandika habari za kiuchunguzi kuhusu ufisadi alioufanya LOWASA na ROSTAM.
upload_2017-4-22_7-59-33.jpeg
Please please waheshimiwa nilio wataja walisaidie taifa
 
mhhhh mpango safishasafisha

kwahio Kama ni uozo aliuona au ulijadiliwa kweny hilo baraza haruhusiwi kusema kisa Tu amekula kiapo

Kama ni kweli kunatatizo kweny sheria zetu ila nnapata wakati mgumu kuamin ulichosema
Huo ndiyo ukweli wenyewe. Ni pale tu atakapokula kiapo cha Kimahakama ndiyo atakapokuwa na uhuru wa kusema yaliyojadiliwa kwenye baraza la mawaziri!! Hata nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri kubwa (Top secret) kiasi kwamba hata ukiondoka hutakiwi kuwa nazo!!
 
Ha
Hivi kama lowassa ni Fisadi kwanin asipelekwe mahakamani?mahakama ya mafisadi imeanzishwa kwa kazi gan?ikumbukwe kwamba mikataba mikataba yote mikubwa lazima ipitishwe na baraza la mawaziri na kusainiwa na mwenyekiti wa baraza la mawaziri ambaye ni rais wa nchi,kwaiyo mkataba wa Richmond ulisainiwa na rais wa awamu iliyopita kwa mujibu wa sheria,kama Richmond ni kampuni ya kitapeli na mkataba ulikuwa wa kifisadi mtuhumiwa number moja ni rais aliye pita,Richmond kama kweli ni ya lowassa kwanin iliendelea kulipwa hata lowassa alivyo ondoka?kama lowassa anahusika na Richmond kwanin haku hojiwa?kama mwakyembe anajua ukweli juu ya Richmond kwanin ukweli wote hakuuweka wazi?ikumbukwe wakati mwakyembe anakabidhi report ya uchunguzi wa mkataba wa Richmond alisema kwamba angeweka wazi ukweli wote nchi ingevurugika je ni kipi ambacho mwakyembe alikificha?turudishe kumbukumbu nyuma mh lowassa alisema anajiuzuru ili kuilinda mamlaka ya juu je mamlaka ya juu ni IPI?lowassa aliamua kujiuzuru kumlinda swaiba lakin ukweli wa Richmond unajulikana,ifahamike kwamba mwakyembe ni moja kati ya viongozi walioamua kudhalilisha taaruma zao,mwakyembe angekuwa na ubavu wa kusema ukweli angeusema bungeni sio vichochoroni.
Anaweza kuwa siyo fisadi lakini pia anaweza kuwa lakini inawezekana hakuna evidence zenye mashiko ili kuthibitisha ufisadi wake na kumtia kolokoloni. Lakini whether ni fisadi ama siyo hilo ndiyo limeshakuwa jina lake. Ikumbukwe pia kwamba CCM pamoja na opposition wamekuwa wakimwita hivyo kwa muda wote mpaka hapo alipogombea opposition ndiyo wakaacha kumwita na kutaka kulazimisha na wengine wasimwite hivyo. Dawa kwa opposition kwenda mahakamani kuliharamisha hilo jina lake la Fisadi. Vinginevyo walikubali na walione ni jina la kawaida kama vile Bwege, Pombe, Masikini, Masalakulagwa, etc
 
Richmond ni Mfano tu wa Tabia za Rushwa rushwa za Lowassa!

Tuachane na Richmond jee zile Rushwa za kwenye Misikiti na Makanisa ambazo hata Chadema walikuwa wakizilaani hasikutosha kumnyima U Rais au nazo alitumwa na Kikwete?
 
Richmond ni Mfano tu wa Tabia za Rushwa rushwa za Lowassa!

Tuachane na Richmond jee zile Rushwa za kwenye Misikiti na Makanisa ambazo hata Chadema walikuwa wakizilaani hasikutosha kumnyima U Rais?
Usihamishe Magoli!!
 
Unachotetea ni nn?
Jamaa yako mwambie akae mkao wa Kula.
Kujificha nyuma ya mgongo wa Mzee wa msoga haisaidii.
Jinai haifi hata miaka 100.
Ukweli utajulikana baada ya mahakama kutoa uamuzi, na si vinginevyo
 
But delivered in a Wrong Number!!
HAkuna cha wrong number, message imekuwa delivered penyewe. Kama issue ya Richmond haitoshelezi ku justify issues iliyoko mezani lazima zitafutwe issues zingine zilizowahi kufanywa na mtu yule yule na zipimwe ili zitueleze tabia ya mhusika.
 
Mimi huwa nasikia wanasema Richmond ilikuwa kampuni feki. Sasa ile mitambo pale Ubungo alileta nani? Hivi kweli kampuni feki inaweza kuleta mamitambo yote yale aliyozindua Obama?
 
Lowassa yuko kimya kabisa wala hazungumzii mambo yalivyokuwa ndani ya Serikali tangu atoke kwenye Uwaziri Mkuu ambao alijiuzulu mwaka 2008. Kuna baadhi ya watu wanautafsiri ukimya wa Lowassa kama ni woga ama kukiri kwamba alishiriki kwenye "Ufisadi" wa Richmond. Lakini Lowassa alikuwa ni Waziri Mkuu na kwa kawaida Waziri Mkuu hula kiapo cha uaminifu na cha kutunza siri za Baraza la Mawaziri ambacho kipo Kisheria.

Lakini pia kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 52 ambayo inataja majukumu na mipaka ya kazi za Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Rais aliyeko Madarakani. Ukisoma pia Ibara ya 35 (i) wafanyakazi wote wa serikali wanafanya kazi kwa niaba ya Rais.

Jambo la Richmond kupewa Tenda ya kuleta Jenereta za Kufua Umeme lilianzia kwenye Baraza la Mawaziri. Lowassa kutaka jambo hilo liende mahakamani ni kwa kuwa ni kwenye mahakama ndiko kwa kuapa kiapo cha kimahakama ndipo kiapo cha kutunza Siri za Baraza la Mawaziri hutenguka.

Leo Lowassa akithubutu kusema yale waliyojadiliana kwenye Baraza la Mawaziri kuhusu Richmond atakuwa anafanya jinai inayofanana na uhaini. Kama alivyosema Nape kwamba "Hawezi kusema kila kitu" ndivyo na Lowassa naye anavyobanwa na kiapo cha uaminifu kwa Rais na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Njia Pekee ya kukivunja Kiapo cha Waziri Mkuu alichokula Lowassa ni kumpeleka Mahakamani ili huko akaseme ambayo akisema leo anaweza kushitakiwa hata kwa Kosa la Uhaini! Kiapo hicho hakiwezi kutenguliwa kwa Hoja ya Richmond kurudishwa Bungeni wala kwa Mwakyembe kujiapiza kuachia uwaziri ili apambane kwenye majadiliano Bungeni,
Kunyamaza nako dawa
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe. Ni pale tu atakapokula kiapo cha Kimahakama ndiyo atakapokuwa na uhuru wa kusema yaliyojadiliwa kwenye baraza la mawaziri!! Hata nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri kubwa (Top secret) kiasi kwamba hata ukiondoka hutakiwi kuwa nazo!!

iv si ilikua tanesco ndio wanatafuta mzabuni wa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme iweje ikajadiliwe kweny baraza la mawaziri na sio tanesco

kwani mashirika ya sirikali yanapotoa tenda hua zinajadiliwa na baraza la mawaziri kupata mzabuni

SOMETHING IS NOT RIGHT
 
Tufanye EL ndio RICHMOND. Naomba kujua malipo kwa RICHMOND analipwa nani hivi sasa?
 
Hvi issue ya lowasa miaka mingapi sasa imepita uchaguzi wote tumeongerea hayo.mzee wa watu yupo kimya c tu muache.mangapi ya kifisadi yapo .mnatu tu chosha sana na issue hiyo.tufanye kazi .kama presedent anavyo taka lets join hand
 
Pamoja na kwamba lowasa simpendi,lakini huyu mzee ana busara sana,angekua ni mwingine katemwa ccm angeongea yote.we mcheki nape anavyolialia daily kwenye media kisa uwaziri.
dogo as asante kwa kutii ushauri wangu. Huoni unavyotema pointi. Sasa ole wako urudie kosa
 
iv si ilikua tanesco ndio wanatafuta mzabuni wa kuleta mitambo ya kuzalisha umeme iweje ikajadiliwe kweny baraza la mawaziri na sio tanesco

kwani mashirika ya sirikali yanapotoa tenda hua zinajadiliwa na baraza la mawaziri kupata mzabuni

SOMETHING IS NOT RIGHT
Mitambo ilitafutwa katika hali ya dharula na jambo lenyewe lilianzia kwenye Baraza la Mawaziri. Unakumbuka ile "Mvua ya kutengeneza"?
 
Hvi issue ya lowasa miaka mingapi sasa imepita uchaguzi wote tumeongerea hayo.mzee wa watu yupo kimya c tu muache.mangapi ya kifisadi yapo .mnatu tu chosha sana na issue hiyo.tufanye kazi .kama presedent anavyo taka lets join hand
Baada ya uchaguzi kuisha CCM wengi walishaacha kumtaja huyu mzee kwa jina la fisadi. Tatizo ni hawa akina Nassari wanakosa hoja halafu wanaanza tena kulazimisha watu wote kwa pamoja tumwone EL alionewa na Mwakyembe. Hayo yalipita na hakuna namna ya kuyaplay back ili sasa watu wamwone EL ni mt. Clean. Tuchape kazi.
 
Hayo yalipita na hakuna namna ya kuyaplay back ili sasa watu wamwone EL ni mt. Clean. Tuchape kazi.
Ina maana Mwakyembe hajui kama haiwezekani ku-Play back mambo ya Richmond. Mimi najua shuleni tulikuwa tunafundishwa jinsi wakoloni walivyowatenda mababu zetu. Jee tulifundishwa kwa lengo la kuurudisha Ukoloni?
 
Back
Top Bottom