snipa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 4,310
- 1,823
Wanajukwaa ikumbukwe Google walishtakiwa Kwa kufanya monopoly kwenye search engine ikiwa ni pamoja na kumiliki platform nyingi kama vile, Android, Chrome, YouTube, Gmaps, Gmail, Gmeet, n.k now wameshtuka wanarecommend pia na browser nyingine
Lakini Kesi kubwa ilikuwa ni kudominate search engine, na kufanya watu wasitumie search engine za aina nyingine kama bing, duckduckgo n.k na hata browser kama vile Firefox n.k zilikuwa na default Google kama search engine.
Na vile vile Google walikuwa wakilipa watengenezaji wa browser Ili waweke Google kama default search engine.
Sasa tukiangalia ulimwengu wa AI tuliopo Sasa hi monopoly waliyofanya Google imewapa uwezo mkubwa sana wa kutrain AI kwaiyo Google wanadata nyingi sana ukilinganisha na Kampuni nyingine.
Google inaweza kulazimishwa kuuza au kutomiliki baadhi ya platform zake hususani Android, ikumbukwe Apple nao wanasakamwa Kwa hizi hizi monopoly kama vile Iwatch kutofunction kwenye android na hivyo mtumiaji wa Iwatch ni lazima awe na iphone na Janja Janja nyingi kama tulivyoona kipindi iphone Zina jack ya earphone Kuna baadhi zilikuwa zinazingua, yalifanywa yote ilimradi utumie earphone zao.
Sasa Tuangalie Kampuni ya Bakhresa, King'amuzi Cha Azam na chanel zake, wao ndio wanaorusha matangazo ya ligi za bongo na baadhi ya nnchi, shida inapokuja ni kuwa Ili uone ligi ya bongo ni lazima uwe na Kisimbusi Cha Azam bila hivyo huwezi, hii ni Moja ya monopoly inayofanywa, binafsi naona Kuna haja Serikali ikailazimisha Azam kuonyesha channel zake kwenye visimbusi vingine Ili kuondoa monopoly kwenye biashara.
snipa 2024