Kero ya mabasi ya mwendokasi, Serikali iingilie kati

Agiza Express

Member
Sep 26, 2022
52
118
Kama ni mtumiaji wa mabasi ya mwendokasi utanielewa hiki nachotaka kusema, imekuwa ni kero ya muda mrefu na sasa imezidi maradufu kwa sisi watumiaji wa mabasi yaendayo kasi na bahati mbaya hatuna pa kusemea.

Kujazwa kwenye mabasi, kukalishwa muda mrefu kwenye foleni ya kusubiri mabasi, kukata tiketi kwa shida na mambo mengine kibao.

Imagine unafika kituoni unaambiwa hamna chenji na kwaiyo mteja unaanza kazi ya kusubiri na kupoteza muda kibao, kwanini wahusika wasiige mfumo mpya wa kivukoni kwenye pantoni ili kumaliza changamoto hii isiyo ya lazima.

Rai yangu kwa serikali na wadau wa mwendokasi, kama wameshindwa kazi wabadili mzabuni waweke mtu anaejitambua kutoa huduma, au waturudishie route za mabasi ya MBEZI POSTA NA MBEZI KARIAKOO ILI SISI WASAFIRI TUSIENDELEE KUHUJUMIWA KWA HAYA YANAYOENDELEA.

UJUMBE UWAFIKIE NA MLICHUKULIE HATUA STAHIKI HILI SWALA NI KERO KUBWA SANA NA IMEONGEZEKA ZAIDI KWA HIKI KIPINDI CHA KARIBUNI.

IMG-20231011-WA0016.jpg


MNAKERA SANA KAMA VILE HAKUNA UONGOZI UNAOONA HAYA.​
 
Back
Top Bottom