Kero: Nyimbo za dini sehemu za kazi

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,382
Ni kweli tunastahili kuvumiliana na kuheshimiana. Ustahamilivu hasa hutambua uwepo wa wenzio wenye imani tofauti na wewe. Sasa katika hali ya kawaida suala la nyimbo za dini kwenye taasisi za umma ni kero hasa kwenye nchi isiyofuata dini. Hatumuhitaji Magufuli au wizara zake kuelekezwa hili. Inakera. Sasa hivi hata kwenye mabasi ya mwendokasi hali ipo hivi. Tafadhali eleweni nyimbo hizo unaweza kuzipenda wewe kwa mwingine ni kero.
 
Mara nyingi nyimbo hutegemea utashi wa dereva, hiyo ni ofisi yake huwez kumchagulia asikilize nin kwan kwake ni kazi na dawa, hili la maofisini mmmh inategemea na mahudiano yao kazn
Hakuna cha kujiridhisha na mahusiano. Watu wanakaa kimya ila wanakerwa. Kwanini usisikilize kwako? Eti dereva hapo ni ofisi yake! Hiyo inaonyesha poor customer care. Hujali wengine eti ofisi yako?
 
hata taarabu huwa ni kero sana kwa wengine mbona......
 
Mie hilo halinihusu maana na zenyewe sizifagilii. Ila sina hakika kama ni nyimbo za dini au zenye asili ya Pwani.
nlikua nammanisha tu nyimbo yoyote inaweza kuwa kero kwa wengine sio ya dini tu....labda kama hizo redio zngezmwa kabisa ndo kila mtu angekuwa huru
 
Hakuna cha kujiridhisha na mahusiano. Watu wanakaa kimya ila wanakerwa. Kwanini usisikilize kwako? Eti dereva hapo ni ofisi yake! Hiyo inaonyesha poor customer care. Hujali wengine eti ofisi yako?
Kwa upande wa dereva unakosea, anapakia walevi, wenye dini zao na vichaa, je amsikilize yupi na amwache yupi?
 
Kwa upande wa dereva unakosea, anapakia walevi, wenye dini zao na vichaa, je amsikilize yupi na amwache yupi?
Watu hawalalamiki na kina Diamond, Mbaraka, JD nk. Dini inagusa hisia maalum. Upigaji wa nyimbo za dini, uvutaji sigara hadhari, kuruka foleni, kutukana nk ni kero zinazotambulika. Ni ustaarabu tu kutambua hisia za watu.
 
Hahaha wewe unakosea sana, huwezi kumridhisha kila mtu, nikikuta unapiga khasida mimi mkristo inabidi nivumilie hadi mwisho wa kituo changu cha gari, mwislam naye avumilie kwaya vilevile na mtu wa dini awavumilie wapenda music wa akina diamond pia.
Mwarobaini wa hili ni kununua gari yako uweke upendacho
 
Hahahaha kwa sababu huna upendo wa dini nyingine ingeweka mihadhara ungekuja kusifia.Acheni kujiinua Mungu hapendi mnasema MUNGU MMOJA HUKU UNAMCHUKIA MUNGU WA JIRANI YAKO.Hii ni nchi huru panda gari shuka endelea na mambo yako.
 
Kunasiku nimeenda nakumati Mliman city nimekuta wameweka nyimbo za injili aisee nili injoi sana
Kwenye festival period inastahamilika. Sio kila siku. Sasa unakuta nyimbo hizi polisi maana yake nini? Kama mtu akafuata haki mazingira hayo tu yanamtoa imani.
 
Ha ha ha zinapendwa sana ndg mleta Uzi had bar unakuta mtu kapiga laga zake anaselebuka "utamu wa Jesus" (r muhando) au ile Nina baba yangu asiyeshindwa kamwe,

Pia unakumbuka kwenye graduu moja hiv DJ kapiga hiz za kawaida mzuka haukuwa mkubwa sn ila DJ alipogusa "wema wa mungu umenizunguka" ilikuwa hatari mkuu.
Mleta Uzi vumilia tuu
 
Kwahiyo na kazi niache nikafanye yangu. Haya ndio madhara ya kujiaminisha kuwa nchi ni ya watu fulani.
 
Hahahaha kwa sababu huna upendo wa dini nyingine ingeweka mihadhara ungekuja kusifia.Acheni kujiinua Mungu hapendi mnasema MUNGU MMOJA HUKU UNAMCHUKIA MUNGU WA JIRANI YAKO.Hii ni nchi huru panda gari shuka endelea na mambo yako.
Usikariri ndugu. Ni familia chache isiyo na watu wa imani zote. Huko kwenye nchi za washika dini upuuzi huu hakuna. Unataka kufanya kazi au kusikiliza muziki. Nunua earphones km ni lazima sana. Si kusikilizisha kila mtu.
 
Hahahaha kwa sababu huna upendo wa dini nyingine ingeweka mihadhara ungekuja kusifia.Acheni kujiinua Mungu hapendi mnasema MUNGU MMOJA HUKU UNAMCHUKIA MUNGU WA JIRANI YAKO.Hii ni nchi huru panda gari shuka endelea na mambo yako.
Usikariri ndugu. Ni familia chache zisizo na watu wa imani zote. Huko kwenye nchi za washika dini upuuzi huu hakuna. Unataka kufanya kazi au kusikiliza muziki. Nunua earphones km ni lazima sana. Si kusikilizisha kila mtu.
 
Sasa niko ofisini kwangu & wewe umefuata huduma utanichaguliaje nyimbo za kusikiliza?!!

Otherwise iwe "Ofisi changanyikeni" ambapo nyie ni watu wazima mnapaswa kujadiliana sio kukimbilia huku.
Mjadala kwa wengine ni chuki na uhasama. Kama ni ofisi yako haina shida, tatizo ni ofisi za umma zinazohudumia wananchi. Kama unahudumia watu kwenye ofisi ya umma bado ni tatizo. Hii huweza hata kujenga hisia mbaya pale mteja asiporidhika. Ndio maana kwenye auditing wanahimiza independence in appearance etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…