Kenyatta: Sie 100% recurrent budget yetu tunalipa mishahara tofauti na Tanzania wao 40% ni misaada

Mkuu umesema Kenya wana ukabila alafu hapohapo unasema wana Utaifa...!!

Unawezaje kuwa na ukabila alafu ukasema nchi ina Utaifa!??
 
Watu mnachonga vitu hamfuatilii Kenya imekopa sana na wako ktk wakati mgumu wa kulipa madeni wanadaiwa Kenya sh trillion 80 mnaponda tu siku hizi kila kitu kipo kwenye mitandao acheni ujua wa kukomenti kitu ambacho hauna taarifa nacho!
 
Huyo Uhuru Kenyatta ameona atudhalilishe kwa kusema tunalipa mishahara yetu kwa kutegemea wafadhili?
Pesa ya kuwalipa wafanyakazi ni yetu na tunalipa wafanyakazi kwa wakati,Kenya wana mgomo wa madaktari mwaka sasa,hawana hela ya kuwalipa wamefikishana mahakamani
Kweli uchaguzi umemkalia pabaya Kenyatta
 
Kama waTanzania tunapaswa kujitafari kwa yale mabaya yetu ambayo tunahitaji kurekebisha, haijalishi yanasemwa na nani. kama yana ukweli inabidi kujitafakari. Tujibu kwa vitendo sio maneno, tufanye kazi kuinua uchumi wetu, serikali nayo isaidie kukuza sekta binafsi. Naamini ndani ya miaka kumi, tunaweza kuipiku kenya kiuchumi kwani tuna rasilimali nyingi kuliko wao.
 
Wadau nimesikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Kenya bwana Uhuru Kenyatta kuhusu uchumi na uwezo wa kukusanya kodi katika Afrika Mashariki.

Kwa jinsi pia nilivyomsikia waziri wa utumishi anavyosema kuwa viongozi wa kisiasa wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tuu, utagundua Rais Uhuru ni kiongozi anayetambua kazi yake.

Hebu msikilize mwenyewe halafu tujaribu kujilinganisha na sisi.
 

Attachments

  • VID-20170427-WA0050.mp4
    2.6 MB · Views: 24
Hatuwezi kutoka kama baada ya uchaguzi kuna warafi wengine wanapandikiza chuki miongoni mwa wanaishi na kufanya nchi isitawalike kwa kisingizio cha kufanya siasa
 
Mm sishangai maana tumeruhusu akili ndogo itawale akili kubwa yaan huwezi kua na mawaziri wabunge wakuu wa mikoa na wilaya wanao jua kuosoma na kiuandika tu.Hawawezi kuja na mawazo ya zaidi ya kusifia na kupalilia vibalua vyao
 
Kenyatta anasaka kura kwa Njia za Kitapeli na Uongo!

Matatizo ya wa Kenya sio kujua kiwango cha Misaada kutoka Nje kinachogharimia Bajeti Bali ni uduni wa huduma zote za Kijamii Kama Tanzania,

Maskini anahitaji huduma zilizoboreshwa sio chanzo cha Mapato ya kugharamia Bajeti
Tanzania kuna huduma gani ya kijamii iliyoboreshwa? acha kuchekesha watu wewe.

Sent from my TECNO R7 using JamiiForums mobile app
 
Mazingira yanamruhusu kueleza hayo ili kuwaridhisha wapiga kura wake. Kenya iliisha malizana na wafadhiri toka enzi za Mwai Kibaki. Kuna masharti waliyakataa na wafadhiri wakasusu na kenya haikuwabembeleza. Kenya sasa hivi inayo mika mitatu toka iingie kwenye kundi la nchi zilizoendelea. Kama ulikuwa hujui hilo tambua sasa.
Haya sasa baada ya kumsikia Kenyatta,ihakiki kauli yake kwa kusoma bajeti yetu iliyopita ili uone bajeti ya mshahara na mapato yetu ya ndani uwiano wake ukoje? Ni kama alivyosema Kenyatta? Au Kenyatta hakusema kweli. Makusanyo ya kodi yanatarajiwa kuwa tirioni 15 na yasiyo ya kodi tirioni 2.5. Jumla tirioni 17.5. Matumizi ya mishahara karibu tirioni 6 hata ukiongeza na matumizi ya ofisi tirioni 2.5 inabaki tirioni tisa za kufanya maendeleo. Serikali ilikuwa ikope tirini 7. Mkopo ni hela ya serikali. Kwa bajeti iliopita msaada ulikuwa ni asilimia 6. Oteo la bajeti ijayo msaada ni 12%. Msaada upo kwa kuwa wasaidiaji wapo. Wakikataa Tunakwenda wenyewe.
Hivyo wewe usiyejitambua Tanzania inao uwezo wa kukusanya mapato yake na kujitosheleza kulipa mishahara mara tatu kwa idadi ya watumishi waliopo iwapo haihitaji miradi ya maendeleo.
wadanganye wajinga !!!!!

Sent from my TECNO R7 using JamiiForums mobile app
 
Edward Lowassa: Namwunga mkono Raisi Kenyatta-BBC London.
(Siku za karibuni Jamani Pigeni Makofi atatangaza kumwunga mkono Laila Odinga)
 
Hata kama ni ukweli lakin nchi yetu haimuhusu. Kenya ni moja kati ya nchi ambazo ufisad ni mkubwa mpk bhas. Kenya ndiyo nchi pekee nazan kutoka Africa, ambayo serikali yake inatumia pesa nyingi kwaajiri ya starehe, hapa nazungumzia magari ya kifahari wanayo tembelea viongoz wa serikali, hasa ikulu ni ya bei ya juu sana. Haipingiki kenya wapo mbele yetu sawa, lakini hiyo ni misingi ya kikoloni inafanya wawe apo. Sisi mdogo mdogo tunawakuta tuu si ndiomana Mnaona mara hawa taki gas yetu iingie kwao. Mfano wew unapata laki moja afu unatumia elfu 80 kwa sterehe, huwez fika. Hela wanayo pata kenya tungekuwa Tz fly over mpka mikoan zingewekwa.
Note : Asitutolee mifano kwa mabaya tu, kwan tunamazuri mengi tu na sisi.


Wew nahisi hapo ulipo ni maskini sana kwa hizo ideology zako za mdogomdogo utafika,, Iwe kweli au uwongo anachosema kenyatta ikuongezee wew changamoto na hamasa mpya ya kupambana na sio kujifariji kipumbavu,, Kubali kua huna, na chukua hatua kutafuta sio kujikweza kwa ambacho tayari unacho..!!

Time iz moving fast more than we do,,!!!.. Utakapofadhiliwa na Kenya kwa misaada ndoto unayoota itakukurupusha usingizini mapigo ya moyo yakikuendea mbio..!!! Kwa sasa wew chapa usingizi tu wenzako wako kumekucha mda mref xana..!!
 

Wew nahisi hapo ulipo ni maskini sana kwa hizo ideology zako za mdogomdogo utafika,, Iwe kweli au uwongo anachosema kenyatta ikuongezee wew changamoto na hamasa mpya ya kupambana na sio kujifariji kipumbavu,, Kubali kua huna, na chukua hatua kutafuta sio kujikweza kwa ambacho tayari unacho..!!

Time iz moving fast more than we do,,!!!.. Utakapofadhiliwa na Kenya kwa misaada ndoto unayoota itakukurupusha usingizini mapigo ya moyo yakikuendea mbio..!!! Kwa sasa wew chapa usingizi tu wenzako wako kumekucha mda mref xana..!!
Kenya haitatokea iwe mfadhili wa Tanzania, sahau. Ila mengi yanashiria kinyume chake inawezekana. Watu hawaishangai kwanini Kenya inaendelea bali kwanini Tanzania ilichelewa? Kivyovyote vile, maendeleo ni dhana pana na inategemea na mtu anavyotaka kuitafsiri na kuiamini tafsiri yake.
 
Back
Top Bottom