Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 281,794
- 733,012
Ni kama vile zimekufa kifo cha asili. Kelele za Uwakilishi wa 50/50 kwenye nafasi mbalimbali za uongozi nazo zimetokomea kizani.
Misemo maarufu ya wanawake wanaweza haisikiki tena! Huu ni wakati wao sasa. Na hakuna wakati mwingine zaidi ya huu. ITS NOW OR NEVER!
No wakati wa kuthibitisha kwa vitendo sasa slogans za #wakiwezeshwa wanaweza! #wanawake na maendeleo. Nknk!
Ukisoma historia ya Afrika wanawake walikuwa watawala na baadhi yao walikuwa majemadari hodari wa vita na wakafanya vema sana.
Hapo katikati mambo yaliyumba kidogo, mpaka ulipofanyika mkutano wao maalum mnamo mwaka 1994 hapo Beijing China ndio mabadiliko mbalimbali yakaanza kufanyika ili kuleta usawa wa jinsia kwenye ushiriki wa shughuli za maendeleo na nyadhifa za kisiasa na kiutawala
Miaka chini ya 30 ni kama bahati ya mtende imewaangukia.. Pengine mkutano ule wa Beijing umechagiza pakubwa sana kwenye hili.. Sasa uwanja ni wao hatutaki hadithi tena tunataka MATOKEO MAKUBWA SASA!
Kama mfumo dume ulichewesha maendeleo, tunataka kuona cheche za mfumo jike.
Kama mfumo dume ulijaa unyanyapaa, tunataka kuona mfumo jike ukimaliza hilo tatizo.
Kama mfumo dume ulishindwa kuleta haki sawa kwenye jamii, tunaanini mfumo jike hautarudia hilo kosa!
Wanasema kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanaume! Sasa kwasasa wako mbele. Tunataka matokeo makubwa sasa.
Mmewezeshwa wezeni sasa! Hatutaki kuona vijembe, husuda, wivu, majungu, masengenyo, kuchafukwa wala makasiriko yasiyo na msingi. Hatutaki kuona ya Cleopatra yakijirudia. Tunataka kuona kazi ikiendelea
Msibaguane kwa misingi ya itikadi,vyama, imani, uwezo, ukwasi, asili, ukabila,ukanda na mambo yote yanayofanana na hayo. Mkishindwa sasa mtashindwa milele. Mkiweza sasa mmepanda mbegu bora
Sisi tupo tu hapa tumevuta hand break. Tunakula mtori taratibu nyama tutazikuta huko chini naamini.