Keissy: Wanaosumbua Bungeni wapimwe madawa ya kulevya

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekea kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.
Kessy huwa mara nyingi anaongea vitu vya ajabu kama vile anatumia madawa ya kulevya yaliyo expire.

Kessy ukitaka kujipendekeza upate uwaziri tuulize tukuambie jinsi ya kufanya. Unavyofanya unaishia kuji embarrass mtu mzina. Kwani lazima uwe waziri?
 
Huyo kessy anafahamika alimuundia zengwe walikua wanapambana nae wachadema kwenye miradi yake naakaweka upanuzi wabarabara kwenye nyumba zamgombea ambae alikua nimkwewake alioa binti yake barabara gani yakataya KIRANDO nipana kuliko hatayaubungo wakati nikatatu kessy nimshenzi naanaroho ya ndugai
 
View attachment 519753

Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekea kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale" - alisema Keissy.

Aidha, Mbunge huyo aliendelea kwa kusema kuwa "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika ni dhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo" aliongezea Keissy.

Chanzo: EATV
Baelezee mheshimiwa,hawa wanawatia aibu hata wazazi wao ,sijui kama hata wameolewa nadhani wana msongo wa mawazo hawa wadada
 
Yeye apimwe wa kwanza kabisa ili lile takwa lake la bangi kuhalalishwa kulimwa kama zao la biashara na itumike kama kiburudisho litimie! Ana hoja gani za maana huyu? Ni mweupe kama upara wake usioota nywele!
 
Wapime na magonjwa, kuna magonjwa yanakimbilia kichwani na kumfanya mtu kuwa na jazba sana.

Tuanze na huyu:

Spika Ndugai ameonyesha upendeleo wa wazi. "Aliposema Lusinde wewe ni kiboko yao mpaka wote wameondoka hii nikauli inamnyima sifa ya Uspika"
 
yeye mwenyewe wakati ule alipowakashifu wananchi wa zanzibar bungeni hadi akataka kuchapwa makofi na wabunge wa zenji nadhani kabla ya kuingia bungeni alikuwa keshapiga msuba - kitu cha arusha!
 
inawezekana ile ambulance aliyopewa na JPM ndiyo huwa inatumika kumleta bungeni maana yeye ndiye mgonjwa.
 
Yy Alikuwa Anataka Bunge La Ndiooooo! Ndiyo Mana Tumeingia Mikataba Feki Sbb Ya Type Ya Wabunge Wa Aina Yake,,,,akapimwe Akili
 
Mbunge wa CCM Ataka Bunge Lipitishe Sheria ya Kuwapima Wabunge Matumizi ya Madawa ya Kulevya..!!!

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekea kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy amesema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale" - alisema Keissy.

Aidha, Mbunge huyo aliendelea kwa kusema kuwa "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo" aliongezea Keissy.
 
Amepadharau manzese

kessy tunakutaka utuombe radhi na ufute kauli yako
 
Kabla ya kuwapima madawa ya kulevya wawapime na akili..... Huyu Kessy nina wasiwasi kama akili zake zimejaa vizuri
 
Back
Top Bottom