KENPAULITE
JF-Expert Member
- Apr 6, 2017
- 3,511
- 3,313
Sikiliza kibwego, wacha kukata mauno mwanaume ujifunze mikakati ya kupigana, pale Garissa kuna Alshabab ambao walikua wamejificha kwenye paa na machine gun wakikimimina risasi kwenye lango kuu, na uani hapakua na jinsi ya kuingia, hivyo ilibidi kifaru kitumike kama ngao dhidi ya risasi za hao jamaa huku special forces wakifuata nyuma kwa nyuma.
Walipiga kifaru risasi zao hizo lakini hazikua na effect yoyote, kikasogea sogea huku wanaume wanakifuata nyuma hadi pale kilifika ndani ndio makomando wakapata fursa ya kuingia kwenye mchezo.
Hapakua na jinsi nyingine maana jengo lenyewe lilikua pekee kiasi kwamba hapakua na majengo ya karibu ili snipers wayatumie. Hata hao wapasua matofali wenu sidhani kama wangeingia mzima mzima wakati wanamiminiwa risasi za machine gun.
Hawa jamaa sasa hawa ni kdf ama GSU?