Kazi za Kitaaluma Kugawiwa kwa Fadhila! Tumekwisha

Umesema kweli mkuu, nimeona jina la dogo Abubakar Asenga!!!! Nimebaki kushangaa DAS ñi taaluma si kazi ya kisiasa naona mvurugano mkubwa unakuja huko mbele ngoja tusubiri tuone kitakachotokea
Punguza ushenzi unajua CV yake?
 
Nyie mlikuwa wengi mnatafuta uteuzi wa MTU mmoja tu wa kugombea urais, mkapitisha garasa , yan mko vichwa vingi mnapitisha kapi, sasa iweje ccm wasikosee kwenye kuchagua watu 300
 
Hebu twambie..Abubakari Asenga hana degree?Mtela hana degree?
Umiza akili basi na wewe mhaya hizo ni kazi za umma sio za siasa na alitakiwa Mtanzania yeyote ku apply ili mchujo ufanyike apatikane mtu sio kwa kuteuliwa wanachama wa CCM hata kama sio wanachama wa CCM bado walitakiwa wazingaze na uyo asenga au mtela wasindanishwe mana izi sio nafasi za siasa ni za utaalamu, iwe masibota
 
Kwaiyo sasa ivi kazi za umma Mtawala ndio anateuwa kwa kuchukua wale wa LUMUMBA afu kulikua na katazo la kuajiri kwani limeshaisha? Pia navyojua kazi za umma si lazima zitangazwe je hii inatoa picha gani kwa wananchi kama MTAWALA anateua hadi nafasi zinazotakia kutangazwa pia ina maana hakuna watu wakukataa anachokifanya na kumpa muongozo? Hii nchi inakoelekea CCM ndio wanajua pekee yao afu ivi faiza uyu nayemjua wa jamii forum ndio uyo kateuliwa tanga? Kama ni ivyo mbona mdini sana wakristo si watapata shida sana
 
Mkuu labda uwe hujafanya kazi kwenye utumishi wa Umma,lakini DAS na RAS ni watu muhimu sana kwenye utumishi wa umma sanaa tuu!!Hiki cheo hakiitaji siasa!Tutashangaa kesi zinajaa Mhakama ya Kazi au CMA(Commision for Mediation and Arbitration)

Cheo hiki si cha mwanaisiasa bali cha mtumishi ambaye ni Parmanent and Pensionable...anatakiwa mtu aliyekulia ndani ya utumishi wa umma hata kwa miaka kumi,mwenye uelewa wa "Organizational Culture" ya ofisi za umma hasa kwa upande wa utumishi,ni cheo kinachotokana na mtu aliye ndani ya utumishi anayepandishwa akiwa ndani ya utumishi wa umma

Hawa vijana wengi walioteuliwa hawajawahi kuajiliwa na serikali,hawa wote walikuwa Lumumba na CCM Makao Makuu Dodoma.Hawajafanyiwa usaili wa aina yoyote kuingia katika nafasi hizo,ndio maana unaona hata Utumishi hawana CV zao ndio maana wameambiwa waende nazo.Wanaenda kuongoza watu waliodumu kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu na weledi wa kutosha katika kanuni,taratibu na sheria za utumishi

Kifupi ni kuwa DAS au RAS ni sawa na Katibu Mkuu katika Wizara,na sio Waziri...Waziri anaweza kuja leo na kesho akashindwa uchaguzi akakosa hiyo nafasi,lkn Katibu Mkuu yupo pale pale,yeye ndio mwenye kujua haswaa Wizara na mahitaji yake,hatokani na siasa au vyama bali mfumo ndani ya utumishi wa umma.Sasa DAS ni kama Katibu Msaidizi na DC kama Naibu Waziri,Wakati RAS ni kama Katibu Mkuu na RC kama Waziri.DC na RC wanaweza hamishwa hamishwa sbb za kisiasa lakini si RAS na DAS

Hawa vijana wanaenda kukutana na watu wengine ndani ya ofisi ya DAS wenye uweledi kuwazidi,hawa wamedumu utumishi na wameingia kwa usaili na si kubebwa.Angeteuwa basi wale walio na weledi,uzoefu na ufahamu wa hii kazi na si hii "shukrani ya kisiasa"

Kwa hili sipo na JPM...hii ni upotofu,hii si sawa!!Fanyia siasa koooooote lakini si kwenye "Muundo wa Utumishi" wa umma unaoongozwa na Sheria,Kanuni na Taratibu!!Sasa nini Maana ya kuwa na "Government Standing Order?"
mungu akubariki mkuu. kwa hili tumsaidie rais wetu kumwambia wasaidizi wako wamemwangusha....
 
wapi wazee wetu? huyo kijazi anafanya nini ikulu? arudishe hela yetu bwana. rais amepotoshwa kwenye uteuzi wa madas.
 
Ni shida sana kama mapenzi yanatufanya tuamini Mkaa ni mweupe,hivi kweli tunakubaliana na utaratibu wa kumpa mtu kazi ya kitaaluma bila kujua sifa yake kitaaluma? Hivi akija na cv inayoonesha ana elimu ya darasa la pili b,tutangaza kutengua uteuzi wake?Watanzania tutoke kwenye sifa za kijinga.
 
Lazima akue(grow) kwa nafasi hiyo
Wengi wao ni wale waliosoma Public Administration, Sociology, Manpower planning, Human Resources mgt, Adminstration and Management. Wamefanya kazi hizi muda mrefu. Ajabu kama hujui kuandika hata dokezo sabili na file movement hujui ndio kazi. Lazima uwe mhitimu wa first degree and above. La sivyo utakuwa una administer waliokuzidi elimu Na uzoefu hapo wilayani.
Tanzania yetu hii.. Wenye degree first class wanaongozwa na diploma/certificate holders.. Ndo nchi yetu ya mwendokasi... I wish haya mawazo ya watanzania yangekua yanamfikia mukulu.. Ila ndo ivo mwenyewe hataki kukosolewa... Kila kitu kipya na cha kustaajabisha tutakiona kwenye huu uongoz wa hapa kasi tu...
 
Kuna watu humu wanabisha wasivovijua.. Wanabisha kwa sababu wao ni wa chama tawala.. Hawana hoja za msingi... Nawafananisha na NG'OMBE JIKE MWENYE JOTO,SASA ANAHAHA KUTAFUTA DUDU... Mada inahusu ma-das jitu linasema lowasa mara j23, kama mambo hayakuhusu acha nyeg* pita kuleeeee
 
Kuna kazi ambazo huwezi mpa mtu hata kama unampenda sana kama hana taaluma hiyo.
Hatuwezi kumpa Pasco wa JF ukuu wa kitengo cha upasuaji MOI kwa kufurahishwa na michango yake JF. Wala Mbwana Samatta kuwa Katibu Tawala Simiyu kwa vile ni mcheza mpira mahiri.
Nimesikia orodha ya ma DAS imetoka na wengi ni vijana watumikaji kisiasa bila utaalamu.
Kwa wanao fahamu, kazi ya DAS (Katibu Tawala Wilaya) sio ya kisiasa wala ya blabla na watendaji wa kazi hiyo walikuwa wanaandaliwa rasmi toka zamani katika chuo chetu cha Mzumbe.
Ni kazi ya kiutawala inayosimamia sheria na taratibu za utumishi ndani ya wilaya. Huyu ndio mtaalamu wa kumuongoza mtawala wa siasa (DC) asiende harijojo.
Sasa orodha iliyotoka ETI hata watu wenye weledi mdogo kama Mtela Mwampamba wamepewa u DAS sio tuu ni kichekesho bali ni matusi kwa hiyo wilaya aliyopelekwa.
DAS,RAS au Katibu mkuu wa wizara akiwa bogus ni maafa katika sehemu hiyo.
Sio wivu kama watu wenye akili nyepesi watakavyo fikiri bali tujiulize Taifa hili tunalipeleka wapi? Hakika kwa mwendo huu ndani ya miaka 3 tutakuwa watu wa migogoro itayo hitaji msaada wa nje.

Hivi mlikuwa hamsomi wala hamsikii!? Walipokuwa wanawawekea ule wimbo unaosema"CCM NI ILE ILE" mlikuwa ham elewi maana yake??
 
Back
Top Bottom