Frank Hood
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 597
- 1,373
Mtu ana miaka 82 hilo deni analipa vp...hyu si anafariki na deni akiwa nalo bado....kwanza sidhan kwa umri huo km mtu anaweza kulipa ata hyo kodi....apa kuna sanaa nyng tu....tatzo bongo kila kitu ni deal....mtu mmoja unakuta anamilik apartment km hzo zaid ya 40Gharama ya nyumba inategemea vitu vingi na siyo vyumba tu. Hizo nyumba mimi sizijui lakini kwa kutumia tu akili ya kuzaliwa, nadhani milioni 48 ni resonable price. Serikali inaweza kuwasaidia kwa kuwapa muda wa kulipa uwe miaka 20 na pia kuwapa uhuru wa kuziuza iwapo wanataka. Yaani hata kama amelipa nusu ya bei na akataka kuuza, basi aruhusiwe kuuza na anayeinunua ndiye awe na jukumu la kumalizia deni lililobaki.
Eeh kuna kipindi wale wa jangwani waliambiwa waamie mabwepande... Wakapaona bush... Sasa hv wanapalilia
Boss unataka serikali ifanye biashara ya kupangisha nyumba? very bad idea, nafikiri hizo kazi waachiwe watu binafsi na serikali ikusanye kodi na kusimamia sheria na haki kati ya wenye nyumba na wapangaji, NHC wamefeli vibaya sanaTukiondoa hili swala la kubeba umasikini nchi yetu itafika mbali.
Maana serikali ingejenga majengo mengi na kupangisha watu
KweliNdo nasema jengeni zenu Kwa pesa mlizikopa na mzifanye za biashara mpate faida.
Hizo Zina maelekezo ya marehemu kuwa wapewe hao maskini waliopo kipaumbele.
Sasa kuwapandishia Bei Ili muwafukuze, hizo ni HILA.
Sasa kosa la JPM ni lipi. Mbona nongwaHutaki kuingia kwenye mkataba unafukuzwa tu, sisi tuko nje hapo tunazitamani nyumba hizo.
JPM alilazimisha zijengwe kisa tu Manji alikuwa na Nia ya kuweka shopping mall Kali hapo, ili kumkomoa, akasema wananchi hao wajengewe nyumba, Sasa tangu lini serikali inajengea wananchi nyumba?
Ukipata chumba na sebule Magomeni Mapipa mitaa karibu na zilipo hizo nyumba kiwanja rasmi kwa milioni hata 90 naomba nitafute kaka wewe nakupa yako 10MTunaongelea Magomeni .
Maelekezo ya aliyejenga nyumba hizo Magomeni alisemaje?
Aliyejenga alisema wakae bure miaka 5 ikiisha watanunua kama wateja wa kawaidaTunaongelea Magomeni .
Maelekezo ya aliyejenga nyumba hizo Magomeni alisemaje?
Eneo lilikuwa la manispaaHao si walivunjiwa nyumba zao za chini kwenye hilo eneo.
Makanyaga nadhani hili suala hulifahamu vizuri.Hili swala la nyumba hizi Serikali wasipokuwa makini litakuja kuwachafua; na hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea uchaguzi mkuu, ukizingatia kuwa muasisi wa wazo hilo hayupo tena, ameshatangulia mbele ya haki.
Hawa watu walikuwa na makazi yao pale ambayo yalibomolewa na hatimaye nyumba hizo kujengwa.
Ushauri wangu katika hili ni kwamba; Serikali wanatakiwa aidha wa-subsidize kwenye bei hiyo kwa kiasi kikubwa ili wakazi hao waweze kuzinunua, au wakazi hao wapewe nyumba hizo bure.
Setikali wasipofanya hivyo kitakachokuja kuibuka huko mbele ya safari ni maneno kwamba JPM aliwajali na sasa hayupo wanaanza kunyanyasika,; na haya maneno hayatatoka kwa wakazi hao, ila kwa watu wengine ambao Serikali ya CCM inawajua pia. Na kama itakuja kupelekea maneno hayo yakatamkwa, watamkaji lazima wataonekana wako sahihi kwa kila mtu atakayebahatika kuwasikia wanayatamaka
Serikali inaweza kuepusha tatizo hili kwa kuwapa wakazi hao nyumba hizo BURE kama kitendo kimojawapo cha kumuenzi muasisi wa wazo la wakazi hao kujengewa nyumba hizo, Hayati JPM
Ikiwezekana wawape BURE, hayupo mtanzania atakayelalamika kwa wakazi hao kupewa BURE nyumba hizo.
aliwadanganya yule chizi sasa thamani ya nyumba magomeni iwe ml 10 kweli?Mtanikumbuka
Hakuna mtu binafsi alikuwa ana miliki nyumba hapo magomeni kota, nyumba zote zilikuwa ni mali ya serikali na serikali ndio iliyoamua kuvunja nyumba zake chakavu za zamani ili kujenga nyumba zake mpya.Hao si walivunjiwa nyumba zao za chini kwenye hilo eneo.
Umeongea vizuri sana, na ninashukuru sana kwa taarifa nzuri mno.Makanyaga nadhani hili suala hulifahamu vizuri.
Kwanza ujue tu, eneo lote la magomeni kota na zile nyumba zote za kota za zamani pale zilikuwa ni mali ya serikali kwa 100%. Hakuna mtu aliwahi kumilikishwa nyumba au eneo pale. Hivyo mtu yoyote akiondolewa pale hawezi kudai chochote popote pale.
Pili, kilichotokea ni kuwa, serikali iliamua kubadilisha matumizi ya eneo lile kwa kubomoa nyumba za zamani ili kujenga nyumba mpya za kisasa ili kuziuza au kupangisha. Sasa wale wapangaji wa zamani wakahaidiwa (kisiasa, kiungwana na kiutu) na serikali kuwa, mara mradi wa ujenzi utakapo kamilika basi watapewa nafasi ya kupangishwa au kuuziwa. Sasa wakati wa kuuziwa ndio huu, wapangaji wanataka ama wapewe bure au wauziwe kwa bei sawa na bure!
Serikali imesema jambo hilo hapana na haliwezekani.
Pole yenu mliiokuwa mnatetea wananchi maskini kufukuzwa.Makanyaga nadhani hili suala hulifahamu vizuri.
Kwanza ujue tu, eneo lote la magomeni kota na zile nyumba zote za kota za zamani pale zilikuwa ni mali ya serikali kwa 100%. Hakuna mtu aliwahi kumilikishwa nyumba au eneo pale. Hivyo mtu yoyote akiondolewa pale hawezi kudai chochote popote pale.
Pili, kilichotokea ni kuwa, serikali iliamua kubadilisha matumizi ya eneo lile kwa kubomoa nyumba za zamani ili kujenga nyumba mpya za kisasa ili kuziuza au kupangisha. Sasa wale wapangaji wa zamani wakahaidiwa (kisiasa, kiungwana na kiutu) na serikali kuwa, mara mradi wa ujenzi utakapo kamilika basi watapewa nafasi ya kupangishwa au kuuziwa. Sasa wakati wa kuuziwa ndio huu, wapangaji wanataka ama wapewe bure au wauziwe kwa bei sawa na bure!
Serikali imesema jambo hilo hapana na haliwezekani.