Kauli ya Wilsoni Kabwe baada ya kutumbuliwa jipu darajani na Rais Magufuli

Atalipwa fidia hehehe!!
pole yake
Japo naona kawa kipenzi cha Ukawa
Hawa sijui wapoje!!
Mtu akitumbuliwa kaonewa akiachwa CCM ni ileile
Tz kuna vizazi vyahovyo kweli
Adui wa adui yako ni rafiki yako.
 
Msheshimiwa Raisi Dkt J. P. Magufuli atakapokuwa mwenyekiti wa CCM - Taifa (ikumbukwe mpaka sasa hana madaraka katika chama) ndipo tutajua kwa CCM ni ile ile au la!
Wakati huo atapokutana na vigogo wa chama na kujua nyeupe na nyeusi ndipo dhamira yake itakapopata jukwaa la kupimwa vyema.
 
Ukiona hivyo ujue anajiamini atashinda.tatizo serikali yetu kesi nyingi zikienda mahakamani huwa inashindwa na kuishia kulipa fidia ambayo ni kodi za wananchi.
Hata akishinda afukuzwe kazi. Unajua mwizi ni mwizi tu na mjanja si rahisi kumkamata hivyo inapotokea loophole kama hii unapiga chini tu lete mwingine afanyekazi, kwani wewe huwezi kuwa Mkurugenzi kuna nini cha ajabu pale kukufanya ushindwe kupiga mzigo.
 
What if baada ya kusimamishwa na baada ya uchunguzi regardless of outcome, Rais akatoa Notice ya kumfuta kazi kwa manufaa ya umma. Unafikiri kuna Mahakama itakayosajili kesi ya Kabwe dhidi ya chochote kwenye sakata hili? Unamshauri vibaya mwenzako!
Kabwe siyo mwenzangu, mimi ni kati ya watu wasiomtaka tangu akiwa Mwanza, alitusumbua sana kwenye uchaguzi wa 2010.

Jibu la swali lako ni kwamba kama hakuna ushahidi wa makosa yaliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa, ana uwezo wa kwenda kumshtaki kwa kosa la kumvunjia heshima mbele ya umma.
 
Walikuwa wanaona kumfukuza kabwe kungempa sifa wenje na upinzani, matokeo yake wakamuhamisha na jamaa ameendelea kuitia hasara serikali, halafu kuna kada anasema ukawa inatetea ufisadi, watu wengine hovyo sana.


watoto wa lumumba wao wanachoangalia ni sifa ya chama sio tz.
 
Msheshimiwa Raisi Dkt J. P. Magufuli atakapokuwa mwenyekiti wa CCM - Taifa (ikumbukwe mpaka sasa hana madaraka katika chama) ndipo tutajua kwa CCM ni ile ile au la!
Wakati huo atapokutana na vigogo wa chama na kujua nyeupe na nyeusi ndipo dhamira yake itakapopata jukwaa la kupimwa vyema.
Aisee wee unafikiria kutokea wapi

Hivi unaona uenyekiti wa chama ndio mkubwa kuliko nafasi ya rais aliyonayo?
 
Jamaa Ni Mpigaji Nguli Tangu Alipokuwa Mbeya, Mwanza Na Dar. Kimsingi Mhe. Pinda Alimtoa Na Hatimaye Mhe. Magufuli Amemtwaa.
Mungu Amjalie Maisha Mema Mtaani Au Jela...Amen
 
Hivi tujiulize mbona amekimbilia kulibwa fidia badala ya kujitetea kwanza kwa hoja za kiutu uzima?? Kweli huli ni jipu kubwa saana.
Chamuhimu afutwe kazi tu hapo panakua hakuna fidia maana mh raisi anaweza kumtengua kwa mabufaa ya umma.
 
Hi yo yote anajibu jeuri kwasababu wakitumbuliwa wanaachwa wanazagaa mitaani.Utaratibu uwekwe kuwa mtu akitumbuliwa,ashikiliwe na polisi baadae keko akisubiria uchunguzi
 
What if baada ya kusimamishwa na baada ya uchunguzi regardless of outcome, Rais akatoa Notice ya kumfuta kazi kwa manufaa ya umma. Unafikiri kuna Mahakama itakayosajili kesi ya Kabwe dhidi ya chochote kwenye sakata hili? Unamshauri vibaya mwenzako!
Kama mtu hana hatia maslahi ya umma yanakujaje? ?umma una m
 
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika kwamba nilionewa nitalipwa fidia?”

Alisema hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.

Alipoulizwa jana, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na mazungumzo yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwandishi: Habari mkurugenzi?

Kabwe: Salama.

Mwandishi: Tumepata taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba maoni yako.

Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?

Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni.

Kabwe: Alitamka palepale au?

Mwandishi: Ndiyo.

Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.

Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo?

Kabwe: Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote nitalipwa?

Chanzo: Mpekuzi
Mwache ajiburudishe
 
Rais ana mamlaka ya kumfuta kazi mteule wake yeyote hata bila ya kutoa sababu, tatizo ni pale ambapo Rais amemwondoa kwa kumtangaza kwenye mkutano wa hadhara na akataja sababu. Sababu zile zikithibitika siyo za kweli ana haki ya kushitaki kwa kudhalilishwa, siyo kwa sababu ya kuondolewa kazini. Bahati mbaya zaidi sababu zile zilitamkwa na Mkuu wa Mkoa ambaye anaweza kushtakiwa, hana kinga ya kutoshtakiwa.
Aliyemsimamisha kazi sio Mkuu wa mkoa!! Afu wewe huijui sirikali, au unaisikia kwa mbaaali!!!! ...ngoja nikupe dondoo "kwa manufaa ya umma sababu zingine hazikutajwa"
 
Back
Top Bottom