Kauli ya Lawrence Masha baada ya kukamatwa kwa Tundu Lissu

...ndio, tulitegemea kuwepo viwanda vingi hadi sasa lakini havionekani, kama TL anavikwamisha awekwe ndani tu!
 
TLS watafanya jambo jema sana kuahirisha uchaguzi kama Lissu atakuwepo rumande mpaka siku hiyo ya uchaguzi. Watangaze tu uchaguzi umeahirishwa hadi hapo hatima ya mmoja wa wagombea wa nafasi za uongozi wa juu ambaye amekamatwa kwa sababu ambazo hazijulikani, itakapojulikana. Huyu dikteta anataka kuingilia uhuru wa kila chombo muhimu nchini.

Kweli kabisa.Na hapo ndipo wataionyesha jamii kwamba wanajitambua
 
Nilikuwa sijaielewa serikali ilipoahidi ujenzi wa viwanda,kumbe ilimaanisha viwanda vya kesi! Hakika kwenye eneo hili serikali inastahili pongezi,imefanya vizuri mno kwa kuhakikisha inakuwa na kesi za kutosha dhidi ya wale wanaoipinga,inapendeza sana.
Ukiona nchi inatumia nguvu nyingi ya vyombo vya dola kuna shida mahali.
Tunaanza kuhama kwenye haki na demokrasia. Aidha hata ana liongoza jeshi la polisi kuanzia waziri, IGP nk kazi zimewashinda.
Mfano mzuri ni jinsi askari wa usalama barabarani walivyo hama kwenye fani ya kuwaongoza waendesha magari sheria za barabarani na kuwa wakusanya mapato. Hii ni aibu. Na iko Tanzania tuu.
Halafu bila aibu hujisifia kukusanya pesa za makosa. Aibuu
 
Najiuliza Swali Moja Hii Kamata kamata ya Viongozi wa Upinzani Kila Baada ya Siku Fulani Hasa Viongozi wa Chadena Kwa nini ni Chadema tu Siyo wa vyama vingine?
Vyama vingine kama vipi? TLP mwenyekit mzee mrema ndio mkuu wa tume ya parole Tanzania, lipumba ndio huyu kapitishiwa mabilioni ya ruzuku na msajili baada ya kufungua akaunti nyingine. Kimebaki chadema tu wengine wote ni CCM B
 
LAWRANCE MASHA ATOA MSIMAMO KUKAMATWA KWA LISSU.

Kukamatwa kwa Mhe. Tundu Antiphas Mughwai Lissu (MB) leo tarehe 6 Machi, 2017

Nimepokea taarifa muda mfupi uliyopita kuhusu kukamatwa kwa Mhe. Tundu Lissu (Mb) na Jeshi la Polisi leo asubuhi tarehe 6 Machi, 2017. Hii taarifa nimeithibitisha baada ya kuongea naye Mhe. Lissu kwa njia ya simu akiwa Central Polisi, Dar es Salaam.

Mhe. Lissu ambaye ni wakili mwenzangu, amekamatwa baada ya kesi dhidi yake, iliofungiliwa na Serekali baada ya kukamatwa kwake Bungeni mwezi uliyopita, kufutwa katika Mahakama ya Kisutu kwa maombi ya waendesha mashtaka. Alipokamatwa Mhe. Lissu alikua akilelekea kwenye kesi nyingine akiwa kama wakili mtetezi katika shauri hilo.

Tabia ya polisi ya kukamata watu baada ya kuachiwa na mahakama au kufutiwa kesi na waendesha mashtaka imeanza kuwa mazoea. Hii siyo mara ya kwanza imefanyika. Natoa rai kwa watumishi wa vyombo vya dola kwamba waheshimu haki za binadamu na waheshimu misingi ya sheria zetu. Kupindisha sheria ili kutimiza malengo ya watu fulani bila kuzingatia misingi ya haki itatupeleka pabaya kama nchi.

Kuna tetesi kwamba kukamatwa kwa Mhe. Lissu inahusiana na njama zinazofanyika na watu wasiojulikana kumzuwia kushiriki katika uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu. Kama hizi tetesi zina ukweli wowote napenda kuweka wazi msimamo wangu kwamba uchaguzi wa TLS usiingiliwe na chombo chochote cha dola. Wanasheria waruhusiwe kuchaguwa Rais wanaomtaka.

Uchaguzi huu wa TLS umekuwa na msisimko wa kipekee kwasababu Wanasheria walio wengi wamechoka kuona haki za watanzania zikiminywa kwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Watanzania wanataka Nchi inayoheshimu utawala bora na utawala wa kisheria, na wanataka chama cha wanasheria ambalo lina nguvu ya kukemea pale ambapo haki haitendeki.

Kwasababu Jeshi la polisi hawajatangaza sababu ya kukamatwa kwa Mhe. Lissu ni vigumu kwa wakati huu kuongelea kilichosababisha akamtwe. Ni vema lakini kwamba Jeshi la Polisi litoe tamko mapema ili watanzania wafahamu ni kosa gani ambalo Mhe. Lissu ametuhumiwa kufanya. Kukaa kimya kwa Jeshi la Polisi itaendelea kujenga hisia kwamba kuna ukweli kwamba kuna njama ya kumzuwia Mhe. Lissu kushiriki katika uchaguzi wa TLS, jambo ambalo ni haki yake kama mwanachama aliyechujwa na kupitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa TLS.

Lawrence Masha
Machi 6, 2017
 
Masha atoe upuuzi wake hapa! namkumbuka kipindi yuko waziri wa mambo ya ndani alivyokuwa na mambo machafu! mara anachukua wasichana wa chuo cha SAUT anakuja kulala naye New Mwanza Hoteli lakini kwa utaratibu kuwa RPC atoe gari ya kwenda kumchukua kimwana chuoni, aletwe Mwanza hoteli na kesho yake gari ya polisi imrudishe chuoni! mfyuuuu hana lolote mfia madaraka tu huyo, atoe dudu yake akakojoe alale tena asiseme neno maana ndio mshenzi aliyechezea mali ya umma
Hahahaha
 
Huku kupaniki si kwa nchi hii.
 
Back
Top Bottom