Katika Dunia yenye takribani watu Bilioni 8 leo, zaidi ya watu Bilioni 110 wamewahi kuishi na kufa

Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu.

Waliowahi kuishi na kuondoka ni wengi zaidi ya waliopo leo, na kila mmoja kwa wakati wake alikuwa na umuhimu wake.

Hivyo nafasi ya wewe kuishi leo isikufanye ufikiri kuwa ni ya kipekee sana, utaondoka siku moja na watakuja wengine. Maisha yataendelea vizuri tu bila uwepo wako.

Hii nimekumbushwa na huyu kijana wangu mkubwa, nami nikaona niwakumbushe.

Ncha Kali.

View: https://youtube.com/watch?v=q_dRsLRYhn8&si=2yfnObSZdHsyqFAM
 
Inatia sana huzuni.
Umenikumbusha kisa cha marehemu bibi yangu aliyefariki 2015.
Alifariki Jumatatu saa 2 asubuhi.
Jana yake Jumapili nilikesha Coco beach, piga sana pombe.
Inafika asubuhi saa 1, napigiwa simu bibi ananiita.
Kufika pale, kila mtu ananiambia bibi yako yuko hoi, anakuita.
Nafika chumbani na pombe pombe zangu bibi akaniambia nimpakate, nikampakata.
Akasema unanuka pombe na kwanini jana hujaenda kanisani.
Aliniambia maneno 3 tu.
Moja, acha pombe,
Pili, usiache kwenda kanisani na jambo la 3 ni siri yangu.
Baada ya pale akanipa funguo kisha akaniambia nakukabidhi huu funguo, tafuta mlango unaoingia funguo hii.
Baada ya pale nikaita watu huku nimempakata.
Akatabasamu, akafumba macho mwenyewe kisha akakata roho.
Aloooo.....sitasahau.
Bibi yangu alikuwa kipenzi changu sana sana sana.
Umeacha kunywa pombe kama bibi alivyotaka?
 
je uliupata huo mlango?

na pombe uliacha au ndio sote tutakufa?
 
Kama alisema uache ni kweli umevunja masharti.
Angesema upunguze ungekuwa upo upo sahihi.
Ila siyo mbaya hiyo ya mara moja moja.
Sasa hiyo mara moja yenyewe saza niulize inakuwaje..😄
Naweza kunywa na nikalewa wiki nzima.
Yaani, pombe nakunywa Jumamosi, ila mpaka Jumatano bado nahisi iko kichwani.
 
je uliupata huo mlango?

na pombe uliacha au ndio sote tutakufa?
Nimepunguza, sio kama kipindi kile.

Mlango sijaupata, ila nimeulizia kwa watu wazima kwetu, wamesema huenda ni huko kwetu kijijini.
Na kila nikienda, nashindwa kuupata, maana nyumba za koo zetu zipo nyingi na mbaya zaidi tumetapakaa kuanzia Tanga, Tabora, Dar,na kwingineko.
Najionea kuchoka tu.
 
Nimeuguza mtu mpaka kanifia mikononi.
Alikuwa anatapatapa huku anasema anaogopa sana, anasema eti kuna watu wako kwa mbali anawaona wanamsubiri.
Hata huko anapoenda ataishi kwa KUTAPATAPA vile vile.

Alitakiwa atuliee tu, alikuwa anaogopa asichokijua.

Fear of the unknown is the greater threat than the actual threat itself.
 
Back
Top Bottom