Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amemwagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo kuzungumza na waziri wake, Hamad Masauni, ili kuona namna ya kuwaachia viongozi wa Chadema waliokamatwa mkoani Mbeya, akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Dk Nchimbi ameeleza hayo leo Jumatatu Agosti 12, 2024 alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro iliyopo mkoani Geita anakoendelea na ziara yake akitokea mkoani Kagera.

Amesema alifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wenzake wa vyama vingine vya siasa, ili wawe na mazungumzo kama vyama vya siasa, aliwasiliana na baadhi ya makatibu wakuu, hata hivyo alipata taarifa wengine wamekamatwa mkoani Mbeya.

"Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, ongea na Waziri, tunaomba muone uwezekano wa viongozi wa vyama vya siasa waliokamatwa kule Mbeya waachiwe huru.

Pia soma=> John Mrema: Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hadi sasa ni 427

"Mtupe nafasi na sisi wanasiasa tuzungumze, siyo mambo yote yanatatuliwa kisheria, mengine ni ya kisiasa," amesema Dk Nchimbi akimwelekeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani aliyeambatana naye kwenye ziara hiyo.

Viongozi wanaodaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), John Pambalu na viongozi wengine wa baraza hilo.

Pia wamo viongozi wa Bavicha, Twaha Mwaipaya, Moza Ally, Deusdedith Soka na wengine.

Wengine wanaodaiwa kukamatwa ni Wakili Deogratias Mahinyila na waandishi wa habari wa Jambo Tv ambao ni Ramadhan Khamis na Fadhil Kirundwa.
 
1000030853.jpg
 
So, Dr. Nchimbi amekubali serikali yake imekosea, awaombe radhi wanachama wa Chadema na watanzania kwa ujumla, kwa makosa ya serikali ya chama chake.

- Nchimbi anavyosema sio mambo yote ni ya kisheria, mengine ni ya kisiasa, hivyo wanasiasa waachwe waongee, hajui hata siasa ina sheria zake? Mfano, mikutano ya siasa mwisho saa 12 kamili jioni kisheria?!

Pia bado inatakiwa na IGP nae aombe radhi, kwa polisi wake kuwakamata vijana na viongozi wa Chadema wasio na kosa lolote, kinyume cha sheria.

Kama watu wanataka kukutana na kufanya mkutano wa kisiasa, kwanini polisi wasitoe ushirikiano kwa watu hao kuwapa ulinzi?

Wape ulinzi wafanye mkutano wao, ukifika muda wa kumaliza saa 12 kamili jioni, waambie washuke jukwaani waondoke eneo la mkutano.

Kama watagoma kufanya hivyo, hapo polisi watakuwa na sababu ya kuwaeleza watanzania jamaa ni wasumbufu, hivyo kuweza kutumia nguvu dhidi yao.

Lakini kuwazingira watu kabla hawajaanza mkutano, tena polisi wakiwa na silaha za moto, huo ni utekaji, polisi wanavunja sheria za nchi wazi kabisa kwa jambo dogo lisilohitaji kusumbuana vyovyote vile.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amemwagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Daniel Sillo kuzungumza na waziri wake, Hamad Masauni, ili kuona namna ya kuwaachia viongozi wa Chadema waliokamatwa mkoani Mbeya, akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Dk Nchimbi ameeleza hayo leo Jumatatu Agosti 12, 2024 alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro iliyopo mkoani Geita anakoendelea na ziara yake akitokea mkoani Kagera.

Amesema alifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wenzake wa vyama vingine vya siasa, ili wawe na mazungumzo kama vyama vya siasa, aliwasiliana na baadhi ya makatibu wakuu, hata hivyo alipata taarifa wengine wamekamatwa mkoani Mbeya.

"Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, ongea na Waziri, tunaomba muone uwezekano wa viongozi wa vyama vya siasa waliokamatwa kule Mbeya waachiwe huru.

"Mtupe nafasi na sisi wanasiasa tuzungumze, siyo mambo yote yanatatuliwa kisheria, mengine ni ya kisiasa," amesema Dk Nchimbi akimwelekeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani aliyeambatana naye kwenye ziara hiyo.

Viongozi wanaodaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni Mbowe, Katibu Mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), John Pambalu na viongozi wengine wa baraza hilo.

Pia wamo viongozi wa Bavicha, Twaha Mwaipaya, Moza Ally, Deusdedith Soka na wengine.

Wengine wanaodaiwa kukamatwa ni Wakili Deogratias Mahinyila na waandishi wa habari wa Jambo Tv ambao ni Ramadhan Khamis na Fadhil Kirundwa.
🧶 Ushafika kwa KIPA.
 
Hata hivyo wameshakula hasara, hata pocket money zimeisha, na ukumbi waliolipia muda wake umeisha, pia hata costa walizokodi muda waliolipia kukaa nazo umeisha, utabidi walipe tena
 
Mwanaccm hii hekima ameitoa wapi ? Au mtu ukiwa umekanyaga ardhi ya kanda ya ziwa unaambukizwa akili automatically.

Tlaah tlaah yeye anashangilia Lissu kukamatwa .
 
Watendaji wa serikali wanakiharibia sana chama tawala utendaji kazi wao haufati misingi ya haki na ukweli ndo maana chama cha ccm kimetoa hilo tamko ili kisipakwe matope kwa utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi wa serikali
 
Back
Top Bottom