Wakuu,
Vyama vya kusindikiza na kukamilisha ratiba.
Katibu Mkuu wa Chama Cha National League of Democracy (NLD) Doyo Hassan Doyo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta sera ya 4R ambayo imeleta matumaini kwa vyama vingine vya kisiasa.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Novemba 5,2024 Jijini Tanga, katibu Mkuu Doyo amesema kuwa walifanya ziara kwaajili ya kuhamasisha wachama wao kuchukua fomu, na matokeo yake wamepata wagombea 7000 katika mikoa 10.
Kupata habari za mikoa yote kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa soma hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwenyekiti wa Chama cha NLD Mkoa wa Tanga Abdul Al Qarney amesema kwa eneo wamesimamisha wanachama 96 kwenye mitaa minne, na wajumbe 75 kwenye halmashauri za vijiji ambao watakwenda kugombea nafasi mbalimbali.
Katibu wa NLD Mkoa wa Tanga Salim Abdallah Salim amesisitiza wanasiasa kuheshimu na kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zile za vyama vyao, ili kuweza kuepusha uvunjifu wa amani wakati wa chaguzi.
Chama cha NLD Septemba mwaka huu kilivuna zaidi ya wanachama 150 kutoka ADC na ACT Wazalendo kwenye mikutano mbalimbali iliyofanyika na Katibu Mkuu wake Doyo Hassani Doyo.