Katibu Mkuu COTU, Francis Atwoli: William Ruto atakuwa Rais katika uchaguzi wa 2027 kufikia saa 4 asubuhi

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,412
3,596
Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, amesema kuwa itakuwa vigumu kumshinda Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 nchini Kenya.

Akiwa mgeni katika kipindi cha JKL Show usiku wa Jumatano, Atwoli alieleza kuwa hakuna mgombea anayeonekana kuwa na rasilimali na nguvu za kutosha kushindana na Rais Ruto. Alisisitiza kuwa nafasi ya kushinda dhidi ya Ruto ni ndogo sana kutokana na uwezo wake wa kimkakati na matumizi ya rasilimali za serikali.

1732772934640.png

"Uchaguzi wa urais humu nchini si rahisi, kuna watu naowaona hivi sasa wakidai wanataka kumng'oa Ruto mwaka 2027 ni wapiga kelele tu. Wengine wanapanga kufanya utafiti ili kubaini umaarufu wao. Huo si mtazamo unaofaa unapopanga kushindana na mtu kama William Ruto," amesema Francis Atwoli.

Aidha, Atwoli amesema kuwa kutokana na ushindi wa Ruto mwaka 2022 alipokuwa 'mtu wa nje ya serikali,' itakuwa changamoto kubwa zaidi kumshinda sasa kwa sababu ana rasilimali za serikali.

"Kila mtu alidhani Raila Odinga angekuwa rais, lakini nini kilitokea? Yule kijana (Rais Ruto) alipanga mikakati yake vizuri na kushinda. Mimi nilikuwa mfuasi wa Raila, na tulikuwa na rais aliyekuwa upande wetu pamoja na rasilimali za serikali, lakini Ruto alituonyesha vumbi," alisema Atwoli.

1732773554084.png

Pia, ameongeza kuwa uhamasishaji wa sasa wa Rais Ruto na uteuzi wake wa serikali ni wa kimkakati na umejikita katika kuhakikisha anapata uungwaji mkono mkubwa ifikapo 2027.

"Kwa mwenendo ambao Ruto ameuchukua, atakuwa Rais kufikia saa 4 asubuhi ya siku ya uchaguzi mkuu wa 2027," alisema Atwoli, huku akisisitiza kuwa hata madai ya kumwondoa Gachagua hayataathiri nafasi ya Ruto ya kuchaguliwa tena mwaka 2027.

===

Francis Atwoli, the Secretary General of the Central Organization of Trade Unions, COTU, says it will almost be impossible to beat President William Ruto in the 2027 General Elections.

While appearing on the JKL Show on Wednesday night, SG Atwoli maintained that there might be no candidate with machinery and resources adequate enough to win against President Ruto.

"A presidential election in this country is not cheap, and the people I'm currently seeing claiming they want to unseat Ruto in 2027 are just noisemakers. Some are even planning to do research to determine their popularity. That is not a mentality to have when planning to run against someone like William Ruto," SG Atwoli says.

In addition, he says following Ruto's victory in 2022, when he was literally a 'government outsider', it will be an uphill task to trounce him now that he has government resources at his disposal.

"Everyone knew Raila Odinga was going to be the president, but what happened? That boy (President Ruto) calculated his moves and won. I was a Raila supporter, and we had a sitting president on our side plus government resources, but he showed us dust," SG Atwoli says.

He adds that President Ruto's current mobilization and government appointments are well calculated, strategic, and meant to earn him massive support in 2027.

"With the trajectory Ruto has taken, he will be the President at 10AM in the morning of the 2027 general elections," Atwoli says, while also claiming that Gachagua's impeachment has no effect on President Ruto's supposed re-election in 2027.

Soma, Pia:
 
Kenya wakimaliza uchaguzi wanaanza tena kampeni za uchaguzi. Sasa wanaongelea 2027. Huu ndo ujinga Magufuli alitupilia mbali, ulikuwa umesha anza kipindi cha JK. Kuna muda wa kujenga nchi na muda wa siasa.
 
Back
Top Bottom