General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,077
Lkn mkuu wale si watumishi wa umma?Unakuwa huna kazi wala mshahara.
Na muda wao wa kustaafu bado?
Au hizo nafasi ni za mikataba?
Lkn mkuu wale si watumishi wa umma?Unakuwa huna kazi wala mshahara.
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Au wewe ndio tuliznguana pale halmashauri flani ukijifanya wewe ni boss wang nikakutoa knock out?Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Si umefukuzwa kazi? Sasa ulipwe mshahara wa nini?Lkn mkuu wale si watumishi wa umma?
Na muda wao wa kustaafu bado?
Au hizo nafasi ni za mikataba?
Yap nilimaanisha DAS kama mtoa mada anavyolinganishaMkuu nafikiri unamaanisha DAS. RAS ni Boss wa watumishi wote katika Mkoa including wa mashirika na Taasisi zote za Serikali na za umma.
Ndiyo DAS ni wa wilaya, mkurugenzi ni wa halmashauri.Basi hiyo ni special case mkuu WILAYA MBILI kuwa na HALMASHAURI moja, BARAZA LA MADIWANI moja na MKURUGENZI kwa maana ya DED mmoja. Japokua kwenye pointi ya DAS naona bado tupo pamoja kwa maana ya kwamba DAS ni wa wilaya (wilaya moja, DAS mmoja) kama ambavyo idadi ya wilaya mbili ulizozitaja inavyokwenda sawa na idadi ya maDAS uliyoitaja pia.
DED vs DAS, Nilimaanisha DAS sio RASDc sio boss wa RAS,
RAS ni mkubwa sana kuliko DC
watumishi wa wilaya kwa maana ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya sio kwa upande wa DED.... Watumishi wa serikali kuu tu na sio wa serikali za mitaaAsante mkuu kwa maelezo yako.
Nimesoma neno kwa neno post zote toka post ya kwanza ya uzi huu nikitafuta majukumu ya DAS.
Mpaka hapa nimepata majukumu mawili tu. Kuwa DAS 1) ni Mshauri mkuu wa DC 2) Ni mkuu wa watumishi wote wa Wilaya
Ila hilo jukumu la pili limenichanganya...! Atakuwaje mkuu wa watumishi wa wilaya wakati hawawajibiki kwake ?
Kama kuna majukumu mengine naomba kufahamishwa tena kwa maelezo ya kina.
DAS hana huo ukubwa.... DAS ni msaidizi wa majukumu ya DC.... Na ni mkuu wa Afisa Tawala (Wilaya), watumishi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya na makatibu tarafa..... Hagusi file la mtumishi wowote wa Halmashauri wala hana mamlaka kwa DEDKiprotoco DAS mkubwa na ndio maana anauwezo WA kusimamia maDED zaidi ya mmoja kwa Wilaya zenye Halmashauri zaidi ya moja.
DAS ni mfanyakazi wa mkuu wa Mkoa.
DC ni mfanyakazi wa mkuu wa Mkoa.
RAS ni mfanyakazi wa mkuu wa mkoa.
DED ni mfanyakazi wa TAMISEMI ambaye yupo chini ya Halmashauri ya wilaya/manispaa/mji (council as a whole).
DED hawezi kuwa chini ya DAS wala DAS kuwa chini ya DED.
DED hawezi hata kuwa chini ya DC, wala RC au RAS. Hawamuhusu kihivyo, bali katika kuwapa ripoti.
DED anaweza kumweka mtu selo kama DC anavyoweza au RC anavyoweza. Haingiliani na DAS,
Kimuundo hakuna DAS kuwa juu ya DED.... DC anaweza kujaribu ama kujifanya yuko juu ya DED ila DAS noMmoja ni bosi wa wilaya mwingine ni boss wa halmashauri. Ndani ya wilaya moja panaweza kuwa na Halmashauri mbili lkn ndani ya halmashauri moja hapawez kuwa na wilaya 2. Obvious DAS kuna mahali anaweza kuwa juu ya DED japo kila mtu ana majukumu yake na hakuna anaye report kwa mwenzake
kiitifaki DED anaweza kuwa chini ya DC but not DAS... DC na DED wana almost same rank... Ila DC ni raisi wa Wilaya ndio inammeza DEDKwa dhana ya "Wilaya" dhidi ya "halmashauri," mimi nadhani DAS yuko juu kiitifaki kuliko DED kwa mchanganuo ufuatao:-
DAS ni mtumishi wa wilaya. (Wilaya moja, DAS mmoja).
DED ni mtumishi wa halmashauri (kwenye Wilaya moja kunaweza kuwa na halmashauri zaidi ya moja).
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba "Wilaya moja, DAS mmoja".
Na pia tunaweza kusema, "Wilaya moja halmashauri moja au mbili na hivyo DED mmoja au wawili"
Katika mazingira haya simuoni DED akiwa juu ya DAS.
DAS Ni afisa Tawala Wilaya, huyu yupo kwa DC. DED, Ni mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya.Swali la msingi hapa ni.. Je kuna haja ya kuwa na DED pamoja na DAS kwa wakati mmoja? au nyadhifa mojawapo ingefutwa tu.
Ndio.Na zina ma ded wake?
Mkuu, Umenukuu Kifungu cha 22(2) cha Local Government Service Act No. 10 of 1982 ambacho kinampa mamlaka Mhe Rais kuteua wakurugenzi ambao wapo kwenye Category VI to VII na wakurugenzi hao waliokusudiwa hapa ni wa manispaa na majiji (Municipal Directors na City Directors).Wadungu naomba nami nichangie mada hii ambayo wengi wanaona kama uhusiano wa DED na DAS ki-protokali unachanganya. Mchango wangu utazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
1. Mkuu wa Wilaya (DC)
Mkuu wa Wilaya anateuliwa na Raisi kwa mujibu wa kifungu cha 13 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa (The Regional Adminstration Act, 1997). Majukumu yake ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Kwa mantiki hiyo anakuwa muwakilishi wa Raisi katika kusimamia ulinzi, usalama na shughuli za maendeleo kwa ujumla. Akishateuliwa mkuu wa Wilaya anaapishwa na kusimamiwa kiutendaji na mkuu wa Mkoa (kifungu 13 kifungu kidogo cha 3).
2. Katibu Tawala wa Wilaya (DAS)
Kifungu cha 16 (2) cha sheria ya Tawala za Mikoa kinamtambua DAS kama principal adviser (yaani mshauri mkuu) wa DC. Kifungu hiki pia kinasema DAS anateuliwa kwamujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Bahati mbaya sina hiyo sheria hapa na nimetafuta mtandaoni sijaweza kuipakua. Ila natoa hoja yangu hapa kwa kuzingatia uteuzi wa Ma-DAS uliofanywa tarehe 5.8.2018 na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma. Katika tangazo lake kifungu cha 1.2 Waziri alisema, "Leo nimewaita kuzungumza nanyi kuhusu Uteuzi na Uhamisho wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya. Kwa mamlaka niliyokasimiwa kwa mujibu wa Sheria nimefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya ili kujaza nafasi wazi kumi nane (18) zilizopo katika wilaya za Kinondoni, Mpwapwa, Dodoma, Iringa, Bukoba, Kigoma, Siha, Mtwara, Newala, Misungwi, Njombe, Kondoa, Manyoni, Kilindi, Chunya, Pangani, Bagamoyo na Handeni".
Hivyo, kwamujibu wa tangazo la Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma ambalo nimenukuu hapa, uteuzi wa DAS upo chini yake kisheria.
3. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED)
Kwa mujibu wa kifungu cha 22 (2) cha Sheria ya Utumishi wa Serikali za Mitaa ( The Local Government Service Act, 1982), DED anateuliwa na Raisi. Majukumu kiutendaji DED anakuwa Chief Executive wa Halmashauri na anaripoti kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).
Hitimisho
Kwangu mimi sioni mkanganyiko wowote wa kisheria kati ya DED na DAS, maana DED anateuliwa na Raisi na DAS anateuliwa na Waziri wa Utumishi wa Umma. Sema DAS anaweza kuonekana katika mazingira flani kuwa boss wa DED pale ambapo anatekeleza kazi anazotumwa na DC. Pia, nimewahi kuona mahala DAS anaudhuria vikao vya Council Management (CMT) ambavyo DED ndio mwenyekiti. DC ni mkuu kiitifiki kwa DED ingawa wote wanateuliwa na Rais, utofauti wao unatokana na majukumu. DC anapolinda amani, usalama na maendeleo ni pamoja na kazi anazofanya DED na wakuu wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Wilaya.
Huu ni uelewa wangu kwa kadri nilivyoelewa sheria husika, kama kuna mahala nimekosea niko tayari kukosoloewa maana mimi si mwanasheria kitaaluma. Asanteni