Katazo la Maandamano ya UVCCM ni Mkakati wa kuja Kukataza Maandamano ya Wanaopinga Serikali siku zijazo

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
519
1,246
Wakuu,

Ukifanya mipango inabidi ucheze vizuri karata zako usiwe 'too obvious' kama Wazaramo wanavyosema. We ulisikia wapi maadamano ya kusifia juhudi za 'Mama' yanapingwa tena karibia na mikutano/maandamano ya upinzani kupinga mkataba wa DP World?

Ikifika tar. 22 mtaona, wataambiwa hamuwezi kufanya mikutano/maanadamo hayo, hamuoni hata ya UVCCM yamekatazwa?

Serikali, mnaweza kufanya bora zaidi ya hivi, ni kinyume na ibara ya 18 na ibara 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kuweka zuio la haki ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa kushirikiana na wengine kutoa mawazo hadharani.

Ni haki ya wananchi kupinga miradi ya serikali kama wanaona haipo kwa maslahi yao. Nyinyi ni waajiriwa wetu, mnafanya kazi kwa niaba yetu kwanini hamtaki kuwajibika?

Polisi na nyinyi mnatakiwa kuwalinda wananchi, sio kutumika na wanasiasa/viongozi kukandamiza wananchi, mnatia aibu kwakweli!

Screenshot 2023-07-17 083123.png

Pia soma - Polisi yapiga marufuku maandamano ya UVCCM ya kuunga mkono Serikali yaliyokuwa yafanyike Julai 18, 2023
 
Yes ni kweli target ni maandamano ya tarehe 22/7 anyway vyo vyote iwavyo ujumbe utawafikia tu.
 
Yes ni kweli target ni maandamano ya tarehe 22/7 anyway vyo vyote iwavyo ujumbe utawafikia tu.
Hata huyo mwenyekiti wa uvccm hakumaanisha , ilikuwa ni mkakati wa serikali kumtuma atoe hilo tangazo
 
Back
Top Bottom