Katavi: Mgambo wa Kijiji cha Majalila washtakiwa kwa kuomba Rushwa ya Tsh. 200,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,506
9,289
PIUS LYAMBISE na NESTORI GABULIELI wanashtakiwa kwa kuomba hongo ya Sh. 200,000/- kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.

Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Amos Mwalwanda amesema, washtakiwa hao mnamo tarehe 25 Aprili, 2024 waliomba hongo hiyo kutoka kwa DEVIDI ELIAS SHEM na ALPHANS JAPHET BWANGARO wa Kijiji cha Kazima, Kata ya Kazima, Wilaya ya Mpanda ili wawaachie baada ya kuwakamata wakisafirisha mbao kutoka Tanganyika kwenda Mpanda bila kibali kinyume na utaratibu.

Washtakiwa wamekana kosa na wamepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana.
 
mhh watajua hawajui..... 200k sio rushwa ya kuomba hiyo hela inatafutika vizuri tu ndani ya muda fulani....
 
Waliomba ombaje? huwa haiombwi hivyo ...sasa wenyewe ndiyo itabidi watoe rushwa ili waachiwe
 
Halafu jamii inavyowachukia mgambo.
Wajiandae kuitumikia serikali miaka miwili.
Wangeomba rushwa ya milioni Mia Kama mawaziri wa Burundi Wala tusingejua.
 
Back
Top Bottom