Kasi ya kushuka kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Ninashindwa kuelewa kuwa kuna matatizo gani iliyoifanya shillingi ya Tanzania kushuka kwa kasi wiki hii dhidi ya dollar ya Marekani?. Juzi juzi shillingi ya Tanzania ilikuwa Tshs.2180 dhidi ya dollar moja. Jana ilikuwa Tshs.2193.73 dhidi ya dollar moja.

Leo Tshs.2204 dhidi ya dollar moja. Na hii ni taarifa ya BOT na siyo kwenye maduka ya kubadilishia fedha. Kulikoni?.
 
Kuna sababu nyingi,inawezekana hatuzalishi.lkn mababa ya unyonyaji imf yanatuambia uchumi umekua
 



Wafanyabiashara wanaagiza bidhaa toka nje kwa kasi. WaTzD hatuuzi mali au bidhaa nyingi nje msimu huu, hatujavuna au hatujazalisha. Hakuna uwiano mzuri wa biashara za kuuza na kununua toka nje.
 
Mwaka 2015 kuanzia Jan - Desemba, exchange rate ilikuwa kiasi gani?
Je hio exchange rate ya 2180 ni ya muda gani sokoni? Mabadiriko ya jana na leo yanakutoa jasho wakati 2015 mwaka mzima hadi mwanzoni mwa 2016 ngoma ilikuwa inakaribia kuipita pound.

Fanyeni kazi muuze nje
 
Huwezi kuelewa kama tayari katika fikra zako huna mtazamo chanya katika Serikali ya awamu ya tano.
Watu wengi mmekuwa Wanaharakati na mna chuki za kutisha mioyoni mwenu.
Ukitaka kujua kwa nini Shilingi inashuka kwa kasi dhidi ya Dola inabidi uangalie suala husika kwa mtazamo wa kiuchumi na Biashara na sio Kisiasa za Uanaharakati. Tufanye kazi tujenge TAIFA letu pendwa.
 
nimeona asubuhi nikiwa njiani nikashtuka, kwa muda mrefu imekuwa inacheza kwenye 2200
 
Tueleweshe wewe mchumi usiyekuwa mwanasiasa sio kupiga mboyoyo hapa ebho!
 
inawezekana kuna ka uhaba fulani hivi katika hazina ya foreign currency ya dollar kule benk `kubwa` . Ku control exchange rate sio kazi ndogo, especially production ikishuka na importation ikawa inaongezeka (negative balance of trade)
 
Huwa inafika 2400 lakini badae inashuka kwa hiyo huwa ni exchange late tu wala isikupe presha maana wakati mwingine mmea hustawi na kunyauka
kuna watu wanatengeneza pesa sana pindi inapofika hyo beh asa wale waliokuwa wamenunua dola kwa 2000
 
Toa utoto wako hapa wewe bulushi. Hajakuelewesha baba yako mzazi kuwa na heshima na busara,nije kukuelewesha mimi masuala ya Uchumi!!??
Kumbe na wewe ni mweupe tu! Unalaumu watu wanaolalamika then badala ya kutoa maelezo ualalamikia wanaolalamika; unamalizia kwa kauli za kusiasa eti watu tuchape kazi, my foot; scatter brains! Bs.
 
Na bado kilimo kimekwama,mvua hakuna,export za mazao zitashuka,tutaanza kuagiza chakula,ikimaanisha watu watahitaji madolari zaidi kuagiza chakula kuliko shilingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…