Kashfa ya makontena TRA tena: Ni ya Silent Ocean

Hili litapita mana hili kampuni ni la aliyemtangulia
ungejua mkewe alivyowekwa ndani masaa 7,ndio utajua huyu mzee wa 5 hataniwi,mzee wa 2 ndio alienda kupiga goti juu ya hii inshu,mzee wa 4 aligoma kwenda kuongea na mzee 5 baada ya kuona itakuwa noma na kashfa,ila yamemezwa kimya kimya na hakuna alojaribu kuripoti chochote....
 
Haki ya mungu hivi ni lini mungu utasikia kilio cha watanzania dhidi ya CCM maana hii nchi wanaitafuna vibaya sana
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi kubaini kashfa ya kontena tisa zenye namba za kulipia kodi TZDL 16-10-25830 zilizoingizwa nchini na Kampuni ya Silent Ocean Ltd ambazo zilinaswa na kitengo cha "Fast Team" cha TRA zikiwa na bidhaa mbalimbali za vipuri vya magari, viatu vya ngozi na nguo za kifahari...

Hivi bado watu wanaendelea na hii michezo?? Hawaoni juhudi za Rais wetu na namna alivyo serious na mapato hasa bandarini?

Ipo kila sababu ya kumuunga mkono Rais wetu katika kuyakabili mambo kama haya.. Waliohusika waadhibiwe tu..maana hakuna namna!

hao silent ocean sio ndio GSM ? Kama hao ni marafiki wakubwa wa Kijana wa Ma Shisha
 
ungejua mkewe alivyowekwa ndani masaa 7,ndio utajua huyu mzee wa 5 hataniwi,mzee wa 2 ndio alienda kupiga goti juu ya hii inshu,mzee wa 4 aligoma kwenda kuongea na mzee 5 baada ya kuona itakuwa noma na kashfa,ila yamemezwa kimya kimya na hakuna alojaribu kuripoti chochote....

Msaada kwenye tuta!!! Mke aliyewekwa ndani ni yupi hapoo ?? Maana uneniacha kidogo
 
Juhudi na kasi ya mh raisi ni nzuri lakini ili afanikiwe anapaswa aimarishe umoja kitaifa na pia uhuru wa kutoa maoni. Hili litamsaidia kuipa nguvu jamii kuibua uozo.
 
Msaada kwenye tuta!!! Mke aliyewekwa ndani ni yupi hapoo ?? Maana uneniacha kidogo
mi nimemuelewa kwamba yule ubavu wa pili wa 4 alikuwa ni lida wa tasisi ya MA<>WA sasa makontena yake hii tasisi mwanzo yalikuwa yanapita bure sasa kipindi hiki yakawa yamepigwa stop mpaka yalipiwe na huyu j5.
 
Sisi wengine hatujakuelewa. Kama Tanzania ni ya wapiga dili, ndiyo maana hawahitaji transparency na matangazo live? Akili matope tupu.
Sikiliza Akili Matope tupu,
Sijaamanisha hicho ulichokiandika, nakueleza kuwa Madai ya kuwa kukosekana kwa transparency katika awamu hii kumeongeza rushwa si ya kweli, mbona katika awamu iliyopita mliyozoea kumtukana mkulu kama mlivyotaka bado rushwa,wizi na dili bado vilikuwa juu sana!, hivyo hiyo siyo hoja sana, Kimsingi sisi Watanzania(na mimi mmojawapo) tunapenda sana maisha ya dili dili, Awamu hii kidogo inajitahidi kupambana na rushwa, lakini si unaona ugumu uliopo toka kwa wananchi, malalamiko kila kona kwanini? kwasababu ya mfumo wa maisha tuliyozoea, ndiyo maana si ajabu unapokutana na watetezi wa wezi, watu wanaowaona wezi kama mashujaa, ndiyo jamii yetu ilipofikia, Tunawasifia na kuwaona mashujaa watu walioiibia serikali.
Nafikiri kidogo umenielewa Akili Matope tupu.
 
Ni GSM hapo hakuna kesi,pia habari ya huyu bwana haieleweki.Yamenaswa wapi?wakati TRA ndiyo wanaothaminisha mzigo?jee hayakulipiwa kodi?
Hao mkuu tutaumiza kichwa bure, ni "untouchables". Kama ni kweli ndio wamehusika, hatuto zisikia sarakasi za faru John kwenye hili, litazimwa kama ishu ya Lugumi
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi kubaini kashfa ya kontena tisa zenye namba za kulipia kodi TZDL 16-10-25830 zilizoingizwa nchini na Kampuni ya Silent Ocean Ltd ambazo zilinaswa na kitengo cha "Fast Team" cha TRA zikiwa na bidhaa mbalimbali za vipuri vya magari, viatu vya ngozi na nguo za kifahari...

Hivi bado watu wanaendelea na hii michezo?? Hawaoni juhudi za Rais wetu na namna alivyo serious na mapato hasa bandarini?

Ipo kila sababu ya kumuunga mkono Rais wetu katika kuyakabili mambo kama haya.. Waliohusika waadhibiwe tu..maana hakuna namna!
Hiyo Silent .... inamilikiwa na nani?
Ushauri wangu kwa rais ni kwamba, atumie nguvu yake yake ya executive power. Weka watu ndani hata ikibidi mawaziri wake mwenyewe. Kama ataendelea kufukuza na kukamata tuuu bila kutia adabu, watu siyo wasikivu kiasi hicho.

Hawa wanajaribu. Wakikamatwa wanasema bahati mbaya, wakipenya ndo basi! Hii inaonyesha kuna sehemu nyingi wanakofanikiwa.

Rais weka watu ndani hata kwa mwaka mmoja au miwili. Tumia vyombo vya usalama wa nchi, achana na polisi na mahakama kwa watu kama hawa.
 
Nakubaliana na wewe tumuunge mkono raisi katika mambo mazuri kama kupambana na ufisadi lakini tumkosoe pia anapochezea katiba na sheria za nchi
Hata tukimuunga mkono Mkuu anachagua majipu ya kutumbua. Hili jipu haliwezi ni sawa na Lugumi trust me!
 
Sikiliza Akili Matope tupu,
Sijaamanisha hicho ulichokiandika, nakueleza kuwa Madai ya kuwa kukosekana kwa transparency katika awamu hii kumeongeza rushwa si ya kweli, mbona katika awamu iliyopita mliyozoea kumtukana mkulu kama mlivyotaka bado rushwa,wizi na dili bado vilikuwa juu sana!, hivyo hiyo siyo hoja sana, Kimsingi sisi Watanzania(na mimi mmojawapo) tunapenda sana maisha ya dili dili, Awamu hii kidogo inajitahidi kupambana na rushwa, lakini si unaona ugumu uliopo toka kwa wananchi, malalamiko kila kona kwanini? kwasababu ya mfumo wa maisha tuliyozoea, ndiyo maana si ajabu unapokutana na watetezi wa wezi, watu wanaowaona wezi kama mashujaa, ndiyo jamii yetu ilipofikia, Tunawasifia na kuwaona mashujaa watu walioiibia serikali.
Nafikiri kidogo umenielewa Akili Matope tupu.

Ukiona wewe binafsi unapenda maisha ya dili, acha kutumia neno "Sisi". Hiyo inaitwa over generalization. Ndiyo tatizo la kukariri kariri kila unachokisikia. Watanzainia wengi ni decent na wanafanya kazi kwa bidii sana kwa ajili ya maisha yao na watoto wao. Wanafanya hivyo katika mazingira magumu kutokana na mifumo yetu ya utawala kushindwa kutatua matatizo ya msingi, yanayoweza kuwarahisishia wananchi wengi kujiletea maendeleo haraka. You don't need a Ph.D to know these simple facts. Jf hapa tunatoa elimu ya uraia bure pia.....Acha kabisa kuwasemea mambo ya kipuuzi watanzania kama kuwaita "wapiga dili".
 
Back
Top Bottom