Kashfa: Askofu Kweka, bintiye wagombea mali

Huo Ni mfumo dume uliojengeka Tu,kwani wanaume wangapi wanaachiwa Mali na wanaishia kwunywea viroba na piua?na watoto wa kike wangapi wanasimamia Mali za urithi,labda babaake aliona ndio mwenye akili kuliko wengine thats y akamuachia cha msingi Mary apewe chake,
Nakuunga mkono
 
Hilo suala limenyooka vizuri sana. Askofu aliuziwa shamba mwaka 1991. Na waliandikishana kwa mwanasheria na mkataba wa makubaliano upo. Huyo dada ana ndugu zake wa kuzaliwa zaidi ya 10, lazima ujiulize kwanini hawajasimama upande wake?
Msiamini sana habari za magazeti bila kujua ukweli wa mambo.
 
Wana wa yule muovu utawajua tu. Siku zote Ku point finger na kuhukumu.Huyo askofu sio malaika anaishi katika ulimwengu wa nyama. Mahitaji yake ni kama mwanadamu mwingine. Akikosewa anaweza kwenda mahakamani kama wewe. Pia anaweza kosea kama mwanadamu mwingine.
 
Habari JF,

Leo katika gazeti la Raia mwema kuna hii habari inayomhusu Askofu mstaafu Erasto Kweka wa KKKT anaegombea eneo la ekari 12 na binti wa ndugu yake bi. Mary Kweka. Kwa mijibu wa habari ni kuwa baba mzazi wa binti wakati wa uhai wake alimpa askofu shamba awe akilishia mifugo yake ila Askofu akajimilikisha mojakwamoja na mara baada ya kifo cha Baba Mary huyo askofu akaja na madai kuwa alishauziwa. Askofu alipoulizwa na mwandishi kuhusu hizo tuhuma alijibu sio kweli na huyo Mary sio mtu wa ukoo wao.

Binafsi nimepatwa na wasiwasi mkubwa kwenye uadilifu wa Askofu huyu aliyejipatia heshima kubwa. Ninaamini JF ina watu wengi wanaoweza kutuweka sawa katika hili.

Karibuni.
Kwakuwa gazeti limemtuhumu Askofu basi tuhuma ni za kweli? Acheni kuchafua watu. Tuhuma ni kitu kingine na uhalisia ni kitu kingine
 
Sijui kwanini asilimia kubwa ya watu waliookoka na wale wa swala tano matendo yao ni tofauti na wanavyotuaminisha...angalia hata mtaani kwenu matendo yao yalivyo...huyo Askofu amewakilisha hao.
Usi generalize wewe.. . Tena kama babako na mamako hawajakufundisha, Mimi ndo nakufundisha sasa, ishu zinazowahusu wachungaji USIKURUPUKE Ku-Komenti
 
Tutolee huu ushuzi wako hapa. Mtoto wako ni mrithi wako automatically bila mjadala. Na huyo Kweka huenda anataka kudhulumu.
Naliona tatizo la msingi sana kwenye uwezo wako wa kufikiri na kufanya judgement. Gazeti ndo linakufanya uwe biased? Kesho likija na taarifa ya kuomba radhi kuwa walikosea nina je? Na wewe utakuja hapa kuomba radhi? Usiwe kama una ubongo wa panya
 
usi

usiangalie upande mmoja tu, wapo watumishi wa umma walioficha mali kwa majina ya wadogo zao au shangazi zao, haujawahi ona mtu anastaafu kazi ghafla biashara za ndugu zake zinaanza kuyumba? yapo makampuni baada ya kigogo wa serikali kustaafu maroli yote yanabadilishwa majina. Wapo mapadre wanamajumba na magari yaliyoandikwa kwa majina ya ndugu zao.


Mkuu hii hoja yako inahusiana nini na madai ya huyo mtoto kwa babake mdogo? Unataka kuhalalisha dhulma?!

**Two wrongs.......
 
Huo Ni mfumo dume uliojengeka Tu,kwani wanaume wangapi wanaachiwa Mali na wanaishia kwunywea viroba na piua?na watoto wa kike wangapi wanasimamia Mali za urithi,labda babaake aliona ndio mwenye akili kuliko wengine thats y akamuachia cha msingi Mary apewe chake,
Wanawake wangapi wameachiwa mali wakakaa kulea viserengeti boys na ving'asti, tena wanawake ndio wachafu hamana mfano, akiachiwa mali yeye kila siku kuoa vivulana.
 
Sijui kwanini asilimia kubwa ya watu waliookoka na wale wa swala tano matendo yao ni tofauti na wanavyotuaminisha...angalia hata mtaani kwenu matendo yao yalivyo...huyo Askofu amewakilisha hao.
Inasikitisha sana!
 
Huyu mtoto anataka kumdhulumu mtumishi wa mungu, anaona akitumia media basi mzee ataona aibu na kumwachia.


It's either you are lame ama wajitoa Ufahamu mkuu! Social media inauwezo wa kusaidia haki kupatikana lakini eti mtoto amdhulumu baba yake mdogo kwa kusaidiwa na social media?! Or maybe unajua zaidi kuhusu hii tuhuma!
 
Hawa watu wanaojifanya watu wa Mungu wana matatizo sana ya ulafi wa mali, wanajitahidi sana kuficha ila tabia haifichiki hata Dr. Slaa ameshindwa kuficha akajifichua.
 
Naliona tatizo la msingi sana kwenye uwezo wako wa kufikiri na kufanya judgement. Gazeti ndo linakufanya uwe biased? Kesho likija na taarifa ya kuomba radhi kuwa walikosea nina je? Na wewe utakuja hapa kuomba radhi? Usiwe kama una ubongo wa panya
Adhabu pekee inayokufaa ni kukupuuza kwa pumba unazoongea. Halafu pia usimchukulie Askofu ni malaika, naye pia binadamu anaweza fanya dhambi vilevile. Ninakuahidi kukupuuza kwa comment yoyote utakayotoa kwenye thread hii.
 
Huyu mtoto anataka kumdhulumu mtumishi wa mungu, anaona akitumia media basi mzee ataona aibu na kumwachia

Eddy unaloliongea ni sawa kabisa. Na ndio ukweli ulivyo. Since i know both sides of the story very well - nimegundua kuwa magazeti wakati mwingine yanapotosha sana ukweli na haki ya mtu inaweza kupotea au mtu kuchafuliwa kwa namna hii.
 
Huu mtifuano siyo wa kitoto, mleta mada huenda unahusika moja kwa moja, either we ndiye binti au mchumba wa huyo Mary, wakati unawasilisha mada ulionekana kuwa neutral but kadri komenti zinavyoongezeka unaleta jazba za kitoto.


Labda niseme tu katika hili mtaanguka vibaya na mtaaibika mno. Time will tell, askofu Kweka hajapungukiwa chochote.
 
Wanawake wangapi wameachiwa mali wakakaa kulea viserengeti boys na ving'asti, tena wanawake ndio wachafu hamana mfano, akiachiwa mali yeye kila siku kuoa vivulana.
Mbona umekuja kwa speed hivo na WW Ni mmoja wao nini,labda hukunielewa nlichotaka kusisitiza Ni Kula mtu Ana haki ya kurithi Mali regardless Ni me au ke,kwahiyo we ukiwa na Mali uta.rithisha jirani kwakuwa umezaa mabinti?
 
Mtumishi wa Mungu hatapata hasara Duniani,amuachie tu huyo binti,anyenyekee kulinda ushuhuda wake mzuri.

Watumishi wa kanisa wanaishi kwa mahitaji sawa na watu wengine. Wanamiliki mali na lazima wazilinde.
Hapa unahitajika uthibitisho tu wa umiliki halali bila kujali uaskofu!
Wakati mwingine waovu wanaweza kutumia sifa ya unyenyekevu wa watumishi wa Mungu kama ulaini wa kuwanyang'anya haki zao.
Pia dini yaweza kutumika kama mwavuli wa kuficha mabaya ya mtumishi.
Hapa ni hoja za kisheria na haki zinazohitajika, siyo majungu na hisia!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom