Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,434
- 3,223
Mchana umetoweka, usiku umeingia!
Wakati wa usiku, tunapokwenda kulala na kufumba macho yetu, hatuna uwezo wa kujua yanayotokea katika ulimwengu wa roho au hata kimwili. Ndiyo maana ni muhimu kumkabidhi Mungu maisha yetu kila usiku kabla ya kulala, ili atulinde na kutuepusha na mabaya.
Yesu alitoa mfano wa mtu tajiri aliyekuwa amejilimbikizia mali; akawa anapanga jinsi ya kuanza kula na kunywa na kustarehe. Aliona maisha yake yako salama lakini kumbe kulikuwa na watu wanawinda kumuangamiza usiku.
Luka 12:20
“Lakini Mungu akamwambia, ‘Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani?
Kwanini tuombe kabla ya kulala?
Mungu ndiye Mlinzi wetu Mkuu
Zaburi 127:1 inasema:
“...BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure."
Kumbe tunaweza tukawa na walinzi, au mbwa, au electric fence, lakini bado maadui wakatupata. Kwahiyo pamoja na kuweka mifumo ya ulinzi, tusiache kujikabidhi kwa Mungu (Rum 8:31-39).
Zaburi 60:12
Mungu akiwa upande wetu tutashinda, yeye atawaponda maadui zetu.
Hatufahamu yajayo
Kama ilivyokuwa kwa yule tajiri, hakuna anayejua yatakayotokea usiku huu tukilala. Ndiyo sababu tunapaswa kujikabidhi kwa Mungu. Yeye anaona yote, anajua yote na ana nguvu za kutupigania. Mfalme Daudi aliijua siri hiyo. Ndio maana aliomba asubuhi, mchana, adhuhuri (Zaburi 55:17)
Mungu anafurahi tunapomshukuru(Luka 17:16-19)
Kila siku tunayoishi ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hivyo tunapoomba tusiache pia kumshukuru Mungu kwa neema tunayopata ya kuwa hai. Mungu anapendezwa na watu wanaoshukuru.
Karibu sasa tuombe. Unaweza kufuatisha sala hii au ukaomba wewe mwenyewe tu kwa maneno yako:
Mungu wetu mwenye nguvu. Nakushukuru kwa kunilinda toka asubuhi. Kwa neema yako nimefika usiku. Asante kwa pumzi ya uhai, na kwa mema yote uliyonijalia siku ya leo. Mungu Baba, usiku umeingia. Najikabidhi mikononi mwako unilinde. Niepushe na mabaya yote ya usiku. Niwezeshe kupata usingizi wa amani, na unijalie kuamka kesho salama. Naomba kwa ajili ya familia, ndugu, jamaa na marafiki, uwalinde nao walale salama. Endelea kuilinda nchi hii, na viongozi wote, tuzidi kuishi maisha ya amani na utulivu. Wagonjwa uwaponye Baba, na wale ambao bado hawajakujua, Ee Mungu rehema zako ziwe juu yao, uwasamehe na kuwaokoa.
Kwa Jina la Yesu Kristo, nakemea na kuvunja hila zote za shetani usiku huu.
Asante Baba kwa kunisikia. Naamini nitalala salama na nitaamka salama, niendelee kukusifu na kukutukuza. Katika Jina la Yesu Kristo, amen.
May the angels of the Lord guard your sleep, His love cover you like a warm blanket, and His peace fill your heart till the morning light. Have a wonderfully blessed night.