Optimists
JF-Expert Member
- Oct 17, 2021
- 374
- 1,068
Naongea kutokana na uzoefu kidogo, nineona kwenye interview vijana wakipanga mistari mirefu kupambania ugali wao, wengine wamekaa mtaani zaidi ya miaka 10, na bado wapo wanapambana kwenye usahili,
Utakapo pata nafasi ya kuingia kwenye ajira, Moja Kwa Moja na utakutana na watu uko kazini wakiwa wanawaza kuacha kazi, yaani wewe unapambana uingie utakutana na watu ambao wanataka waondoke, wakiwa na depression na mawazo tele, utakuta watu senior, wenye miaka 10 kazini wakiwa hawana nyumba, stress zikiwa nyingi mnooo, utashangaa kuona watu wakishinda na cadet mpauko, bado utakua uelewi elewi, utakaa miaka mitano bila ya kufanya jambo lolote la maana, hapo ndio utaanza kupata depression.
Nimeona vijana wengi wakisema tukishaingia tutafanya biashara au tutafanya kilimo, niamini Mimi kati ya walimu 10 waliofanya hivyo mmoja tu ndio alifanikiwa, kwasababu biashara au kilimo lazima uwepo wewe utajichanganya ufungue biashara alafu umuache mtu hapo ndio utakua Mwisho wako.
Huwezi Fanya jambo lolote la maendeo bila kukopa, mfano ukiingia na degree utakopesheka million 18, na mshahara utabaki na laki mbili au tatu, sasa inategemea hiyo million 18 umeipeleka wapi, kama umeenda kujenga chumba na sebule basi ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kifukara maisha yako yoote. Ukiiweka kwenye biashara na umemuweka mtu basi ndio mwisho wako huo.
Kukosa matumaini ya uliowakuta kazini, na miaka yako mitano uliyofanya kazi bila kumiliki chochote, ndio kitakufanya uanze kuwaza kuacha kazi, kuvumilia mateso tena unajikuta umepangwa vijijini uko, au kigoma, sumbawanga, Rukwa n.k hapo ndio utatamani urudi tu uache kazi urudi mjini.
Ubaya wa hii kazi hakuna marupurupu au pesa za kuiba, alafu unyonge wa walimu wa miaka iliyopita ndio itasababisha Kila mtu akuchukulie poa tu, ukijitambulisha wewe ni mwalimu hakuna heshima Wala recognition ambayo utaipata kwa mtu yoyote yule.
Karibuni kwenye ualimu, lakini kama una ndoto miaka Yako 15 ya ualimu utazidiwa na mtu aliyeko TRA, TPA mwenye miaka miwili kazini.
Believe me, nioneshe mtu mwenye status yoyote Tanzania hii ambaye kasomesha mtoto wake ualimu.
Asante.