Kariakoo: Polisi wafanikiwa kuwaua majambazi wanne baada ya majibizano ya risasi

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,695
2,143
Nimeona kuna taarifa zinasambaa huko Instagram kwamba kuna majambazi yalitaka kupora ktk mtaa wa Livingston Kariakoo bahati mzuri polisi wamewahi ktk eneo la tukio. Taarifa zinasema kulikuwa na majibizano ya risasi. Na kunaonekana picha za watu wakiwa wamepigwa risasi wapo chini kama watatu hivi.

Je, Kuna mtu anayejua lolote aje atutosheleze hapa?

---Updates---
Maeneo ya kwa Bakhresa Kariakoo usiku huu wameuawa majambazi wanne mtaa wa Livingstone na Aggrey karibu na mtaa wa Lumumba Mnazi Mmoja. Kuna mama mwenye mimba ambaye alienda kununua mikate kapigwa risasi mbili.

Tukio limetokea mida ya saa nne kasoro usiku huu.

 
Kweli kuna tukio la ujambazi ambalo halikufanikiwa na majambazi watatu wa kiume na mwanamke mmoja wameuwawa katika majibizano ya kurushiana risasi na Polisi. Tukio hilo limetokea Mtaa wa livingstone na Aggrey kwenye duka maarufu kwa Bakhresa usiku huu wa leo majira ya saa mbili plus. Picha zitafuata baadae zilizopo si nzuri kuziweka hapa.
 

Kama wameshaanza hadi kuvamia ' Kariakoo ' basi bila shaka hawapo mbali sana ' kuvamia ' Magogoni kwa ' Taita ' mwenyewe.
 
Asee hata mimi nimeziona hizo picha.
Wenye taarifa zaidi waje hapa kutuhakikishia.
 

Weka tu Mkuu ili tuweze kuwatambua Ndugu zetu ' Majambazi '.
 
Kadri ugumu wa maisha unavyoongezeka,watu nao wanazidi kuwa majasiri kukabiliana na ugumu huo wa maisha uliopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…