Kanuni 50 Za Kuwekeza Kwenye Ardhi Na Majengo Kwa Mafanikio Makubwa

Aliko Musa

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
209
305
Kanuni Na. 04.

Kuwa Na Fokasi.

Fokasi ni kuchagua mtaa mmoja na kuwaachia mitaa mingine wawekezaji wengine. Fokasi ni kujenga timu bora sana kwenye mkoa mmoja au wilaya moja na kuacha mikoa/wilaya zingine wawekezaji wengine.

Fokasi ni kuchagua njia/mbinu moja ya kuwekeza kwenye ardhi na majengo mpaka kupata mafanikio ya kuweza kukuza njia nyingine ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Fokasi ni kuchagua aina ya vigezo fulani vya kupata kiwanja au nyumba inayolipa bila kutamani viwanja vingine ambavyo havina vigezo vyako vya kiuwekezaji.

Fokasi ni kutokubali kumiliki viwanja au majengo nje na mpango biashara ulioandaliwa na timu yako ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Fokasi ni kutumia ardhi na majengo kujitajirisha na kuacha njia nyingine zitumiwe na watu wengine. Mpaka uwekezaji wako uwe na uzao mkubwa sana wa kiuwekezaji.

Fokasi ni kuchagua na kulisimamia jambo moja mpaka likamilike bila kuacha. Fokasi ni kudumu kwenye mchakato wa kujenga mtandao bora sana (hasa mtandao mahalia) katika kipindi chote cha uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Hii ni kwa sababu, bahati ya kupata viwanja au majengo yanayolipa sana hutegemea sana mtandao sahihi ulionao. Fokasi ni kuchagua kuwekeza nguvu zako na muda wako kwenye mambo ambayo unayafanya kwa ubora sana na kuacha mambo mengine wafanye wanatimu wako mahalia.

Fokasi ni kuchagua kumiliki nyumba chache ambazo hutengeneza kiasi kikubwa cha kipato endelevu na kuacha nyumba za kipato cha kawaida wamiliki wawekezaji wengine.

Fokasi ni kutafuta na kuchagua mashamba yanayoingiza kiasi kikubwa cha kodi kwa kila mwezi na kuacha wengine wamiliki mashamba ya kodi za viwango vya kawaida.

Fokasi ni kuendelea kukusanya mtaji fedha kwa ajili ya kuanza kununua, kuendeleza na kuuza viwanja bila kuanzisha biashara nyingine katikati ya mchakato wa ukusanyaji wa mtaji fedha.

Darasa la jumatano hii litakuwa na kanuni muhimu mno kuhusu uwekezaji wa ardhi na majengo.

Unahitaji kipindi cha miaka mitatu (3) ili kujenga ubobevu kwenye wilaya moja unayowekeza kupitia umiliki wa ardhi na majengo.

Kwa miaka mitatu (3) ya mwanzo unahitaji kuweka fokasi kwenye maeneo mawili:

✓ Fokasi kwenye wilaya (jimbo) moja tu.

✓ Fokasi kwenye njia moja ya kutengeneza fedha. Mfano; kununua na kuuza viwanja.

Naomba uwakaribishe rafiki zako wawili (2) tu tuweze kujifunza pamoja.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711

Bofya hapa kujiunga na kundi letu zuri....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom