Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 52
- 138
Zanzibar ni muunganiko wa visiwa viwili cha Unguja na Pemba vilivyoko kwenye mwambao wa Afrika mashariki vinazungukwa na bahari ya hindi ambapo vimekuwa ni chachu na vivutio vya watalii na watu kutoka maeneo mbali mbali ya Dunia.
Kama waswahili wanavyosema ''Kizuri kinajiuza na kibaya kinajitembeza''. Hivyo uzuri wa viziwa vya Zanzibar kutokana na vivutio vyake, Historia, Mazingira yake na uwoto wake wa asili umepelekea visiwa hivyo kuwa maarufu sana kila pembe ya dunia na kuwafanya Watu kutoka maeneo mbali mbali kufunga safari kuja kuona vivutio na haiba nzuri ya mazingira ya visiwa hivyo.
Mji Mkongo wenye historia kubwa unaopatika kisiwa cha Unguja mkoa wa Mjini Magharibi una majengo mengi ya kihistoria kama Beit Ajab, Kanisa la Mkunazini, Ngome konge na mengineo ambayo yanayobeba historia nzima ya Tawala kwa mwambao wa Afrika mashariki na kati na tawala za kifalme zilizokuwa zikitumika kuwangonza watu wa visiwa hivyo.
Mji huo ulijipatia umaarufu sana mnamo karne ya kumi 15 mara baada ya kuwa na soko kuu la watumwa kwa Afrika mashariki ambapo watumwa walikuwa wakichukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na kupelekwa katika soko kuu la mkunazini na kuuzwa.
Katika vivutio vyote vinavyopatikana Mji mkongwe, Kanisa la mkunazini ni kivutio kikubwa kutokana na historia yake ya kutoka kwenye soko kuu la watumwa kwa mwambao wa afrika mashariki na kati ambapo watu walikuwa wakichukuliwa kutoka maeneo mbali mbali na kufikishwa sokoni hapo na kuuzwa.
Kanisa la mkunazini limejipatia umaarufu sana Duniani na kuwafanya watu wa Mataifa mbali mbali kufunga safari ya kulitembelea kanisa hilo kutokana na kuwa na historia kubwa kutoka soko la Watumwa hadi kufikia sehemu takatifu ya ibada (Kanisa).
Watumwa walifikishwa eneo hilo la mkunazini na walifungwa kwenye mti mkubwa wa Mkunazi uliokuwa ukipatikana hapo kwa ajili ya kunadiwa na kuuzwa ambapo walichapwa uchi kwa mkia wa taa na wale waliolia waliuzwa kwa bei ya chini na wale waliokuwa hawalii bei yao ilipanda.
Kwa wale waliokuwa hawakuuzwa walihifadhiwa katika mahandaki yanayopatikana katika eneo hilo la kanisa ambapo ndio kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea eneo hilo.
Mti huo wa mkunazi uliweza kupelekea kupatikana jina la eneo hilo na kuitwa Mkunazini na kusabibisha kanisa hilo kuitwa kanisa la mkunazini.
Watummwa waiokuwa wakitoka maeneo tofauti ya Afrika walifikishwa maeneo ya kama vile Bagamoyo na kilwa na kupandishwa majahazi na kupelekwa Zanzibar katika eneo la soko kuu la mkunazini kwa ajili ya kunadiwa na kuuzwa.
Wanunuzi wa biashara hiyo walikuwa wanatoka maeneo mbali mbali ya bara la ulaya na asia na kuja mkunazini katika soko kuu la watumwa la afrika mashiriki kwa ajili ya kununua watumwa.
Dr living stone alikuja katika mwambao wa afrika ya mashariki mara baada ya kupotea kwa safari yake ambayo ilikuwa na lengo la kuchunguza chanzo cha mto Naili na kujikuta amefika katika naeneo ya ujiji na kukuta biashara ya utumwa ikiendelea kufanyika.
Kwa wakati huo biashara ya utumwa iliashasitishwa nchini Uingireza kutokana na mapinduzi ya viwanda karne ya 18 ambapo Dr living aliamua kulichukua swala lile na kulipeleka kwa malkia wa uingereza kwani kipindi hicho Zanzibar ilikuwa chini ya himaya ya muingereza japo ilikuwa inaongozwa kwa dola ya kisultani.
Mnamo tarehe 6 ya mwezi wa 6 ya mwaka 1873 hapo ndipo soko kuu la watumwa lilifungwa visiwani Zanzibar na muingeleza ingawa biashara hiyo iliendelea kwa siri katika maeneo mengine mpaka mwaka 1907 hapo ndipo biashara ilisimamishwa rasmi.
Mara baaada ya kusitishwa rasmi kwa biashara ya utumwa Padrii Edward stear aliweza kulitumia eneo hilo la mkunazini ambapo awali kulikuwa eneo la soko la watumwa kwa alianzisha ujenzi wa kanisa la dhehebu la Angelekana mnamo mwaka 1873 mpaka 1880 kwa lengo la kuwakomboa waafrika na kueneza mafundisho ya dini ya kikristo.
Baada kukamilika ujenzi wa sehemu takatifu ya kanisa mwaka 1877 ibada ya mwanzo ya kanisa hilo ilifanyika katika kipindi cha sikuu ya Chrismas, ambapo mpaka leo hii kanisa la Mkunazini limekuwa linaendelea na ibada zake na kuwa katika hali ya uimara kutokana na ustadi wa ujenzi uliofanywa toka enzi hizo.
Kuwepo kwa kanisa hilo la mkunazini ni kielelezo tosha cha kukomeshwa kwa biashara ya utumwa iliyokuwa inafanywa katika maeneo ya bara na pwani ya afrika kwa ujumla ambayo ilikuwa ikimzalilisha mwaafrika na kumuweka katika mateso na uzallishaji.
Ndani ya kanisa hilo kuna mahandaki yaliokuwa wakihifadhiwa watumwa ambapo mpaka leo hii yanapatikana. Na kinanda cha pekee cha kale kinachopatikana ndani ya kanisa hilo tangu 1880 ambacho mpaka sasa kinafanya kazi na barani afrika vipo viwili kingine cha kale kinachofanana na hicho kinapatikana katika kanisa la Saint George huko Afrika Kusini.
Kanisa la mkunazini lina urefu wa futi 60 na linachukua waumini 150 mpaka 200 kwa wakati mmoja na limejengwa kwa mawe na udongo uliochanganywa na chokaa hivyo imepelekea uimara na umadhubuti wa jengo hilo.