Kampuni ya Bajaj imetoa toleo jipya la pikipiki aina ya Boxer 125 HD

Habari zenu wadau na wapenda bike, aisee niende moja kwa moja kwenye mada.

Kampuni ya Bajaj wamekuja na toleo jipya la pikipiki aina ya Boxer 125hd isiyokuwa na paper oil filter.

Tuone kama muendelezo wa uboreshaji huu utaweza kuboresha engine za boxer maana toleo hili jipya jamaa wameondoa kabisa ile paper oil filter.

Pia seat ya pikipiki hizi zina muonekano kama wa TVS mean imenyanyuka kidogo.

Naona jamaa wanajaribu kuboresha engine zao na kufuata mfumo wa engine za washindani wao TVS.

Asanteni na karibuni kwa mjadala
Omba msaada wa masahihisho ya kichwa cha habari kisomeke KAMPUNI badala ya KAMLUNI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu engine za tvs zinachemka balaa kuliko za boxer, boxer unatembea km za kutosha husikii kitu, ila tvs umbali kidogo tuu tayari
Kuchemka ni sawa maana engine za TVS kwenye cylinder head hazina nozzle ya kupumulia na kupunguza heat kwenye engine ila Boxer engine zao pale juu kwenye cylinder head kuna nozzle inayosaidia engine kupumua hivyo kupunguza heat kwenye engine fast than TVS
 
Na hata pulling,tvs ukiwa namba tano ukitembea 20kph inalalamika kuzima ila boxer unatembea bila malalamiko
Kwenye kuchanganya mara nyingi hutegemea ukubwa wa engine, uchomaji wa mafuta hapa tunangalia zaidi plug, air cleaner ya bike yako.
Bike yenye engine 125cc inachanganya haraka kuliko bike ya 150cc.
Plug ikiwa chafu itasababisha uchomaji wa mafuta kuwa mdogo au chini na kusababisha bike kutochanganya vizuri and vice-versa plug ikiwa bado mzima/safi.
Air cleaner ikiwa chafu haijasafishwa itasababisha poor air & fuel mixture kwenye carburetor, aaaah ndio hivyo yaan
 
Wodi za mifupa ziongezwe
Mkuu kuvunjiaka hata mahouse girls wanavunjika nyumbani ni kadari za Muumba.
Binafsi bike isha niburuza sana na last time ni mwezi march tu hapo hadi nikalazwa MOI ila siwezi acha kuendesha bike maana najua vitu kama ajali na faini za traffic haviepukiki kwa waendesha vyombo vya moto wote.
Halafu kama Sir God kashakupangia kwenda MOI hata uwe makini vipi utavunjika tu.
 
Kwenye kuchanganya mara nyingi hutegemea ukubwa wa engine, uchomaji wa mafuta hapa tunangalia zaidi plug, air cleaner ya bike yako.
Bike yenye engine 125cc inachanganya haraka kuliko bike ya 150cc.
Plug ikiwa chafu itasababisha uchomaji wa mafuta kuwa mdogo au chini na kusababisha bike kutochanganya vizuri and vice-versa plug ikiwa bado mzima/safi.
Air cleaner ikiwa chafu haijasafishwa itasababisha poor air & fuel mixture kwenye carburetor, aaaah ndio hivyo yaan
Upo vizuri kamanda, ngoja nikaifanyie service bike yangu air cleaner maana kitambo sana

Sema hizi boxer zinachosha kubadilisha oil filter
 
Back
Top Bottom