Kambi rasmi ya Upinzani, yalaani Kutekwa Kwa Mwanahabari Bi Salma Said Zanzibar

Tanzania na dunia nzima inaelewa kuwa marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ni batili. Na kwa kuwa uchaguzi huu ni batili, watawala yaani Chama cha Mapinduzi kimeingia katika historia ya kipekee duniani kwa kuwanyima haki wananchi wake.

Matukio mbalimbali yanayoendelea Zanzibar ikiwemo matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa si kwa taifa letu tu pekee bali pia kwa dunia nzima.

Tukio la kutekwa kwa mwanahabari Bi Salma Said wa Deutsche Welle (DW) kimezua maswali makubwa lakini hofu kubwa kwa wananchi, familia yake na wadau hasa wanahabari wa ndani ya nchi na jumuia za kimataifa. Ni dhahiri kuwa kutekwa kwa Bi. Salma Said kunatokana na kazi yake ya uanahabari na ndio maana ushahidi wa awali ambao umepatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, unaelezea wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea hasa katika uchaguzi batili wa marudio ya Zanzibar.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inalaani kwa nguvu zote kitendo cha utekaji wa mwanahabari huyu kutokana na kazi yake. Aidha, tunaitaka Serikali kuhakikisha kuwa mama, dada, rafiki na ndugu yetu Bi Salma Said anapatikana akiwa salama.

Tunaendelea kuamini kuwa kuchelewa kupatikana kwa Bi Salma Said na ukimya wa vyombo vya Serikali na Usalama ni matokeo ya uminyaji wa demokrasia kwa wale wasiofanya kazi kwa mashinikizo ya Chama tawala.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, itaitisha maandamano makubwa nchini ili kushinikiza upatikanaji wa haraka wa Bi Salma Said lakini pia kupaza sauti kwa ulimwengu kuwa Tanzania si mahali salama kwa wanahabari.

Kwa niaba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, tunaungana na watanzania wote hasa familia ya Bi Salma Said na watu wote wenye mapenzi mema kumuombea heri Bi Salma na kuamini kuwa atapatikana akiwa Salama Salmin na kuwatia hatiani watekaji wake.

Imetolewa na,

Joseph O. Mbilinyi (MB)

Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo.

19/03/2016
Hawa ndio wabunge wanaojua wajibu wao siyo nape amekaa kimya tu kama vile hasikii chochote kile kinachoendelea juu ya kutekwa kwa mwanahabari huyo
 
Naona watamwachilia wakishamaliza maigizo yao ya uchaguzi wao. Alafu wanasema uchaguzi wa huru na haki wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa .
Mkuu ni sawa na vichaa walio lazwa mirembe kujuliana hali.ccm wametia aibu na wameonyesha kuwa hawana tofauti na nkurunzinza
 
Ningefeli vibaya darasani si ungeniona nagombea Uenyekiti wa Chama chako? Kumbe ukitongozwa huwa unajiuma uma vidole mie sitombi watafuna kucha tafuta Mwingine!

http://chui mkali kuliko wewe lakini anazaa .usiwe mkali humu jf watu hawatukani
 
mimi bado niko shamba .wewe ulikuja mjini kwa kufata msafara wa mwenge ndio unaongea pumba za wakuha

Acha kukariri kuwa kila aliepo mjini alikuja? Wengine tumezaliwa mjini kama kuja basi kuja porini. Eti pumba "WAKUHA?"
 
Acha kukariri kuwa kila aliepo mjini alikuja? Wengine tumezaliwa mjini kama kuja basi kuja porini. Eti pumba "WAKUHA?"
http:// siku nyengine usijipendekeze tena kwangu .sema leo j2 nimekuhurumia .mimi ni kijukuu cha popobawa .angalia sana wewe dogo usije ukadhurika bila bila kuvuliwa nguo
 
siku nyengine usijipendekeze tena kwangu .sema leo j2 nimekuhurumia .mimi ni kijukuu cha popobawa .angalia sana wewe dogo usije ukadhurika bila bila kuvuliwa nguo

Wewe si ndie wa kwanza kuni quote!!ushasahau mara hii? Ungeijua historia ya Popobawa usingejiita hivyo! Anachofanya Popobawa ni kulipiza kisasi? Je nawe unalipa kisasi kwa yaliyokukuta?
 
Mbinu za kuweka urimbo mtini ili ndege anase ccm mmeyakanyaga Wajerumani watawakanyaga
 
Chadema wamekosa la kusema wanatafuta makosa hata kazi ya polisi mgambo wataingilia mwaka huu
 
Ningefeli vibaya darasani si ungeniona nagombea Uenyekiti wa Chama chako? Kumbe ukitongozwa huwa unajiuma uma vidole mie sitombi watafuna kucha tafuta Mwingine!
hili jukwaa hata serikali ikilifungia ni sawa tu, unawezaje kuacha mtu anaporomosha matusi kiasi hiki bila kuchukua hatua?
 
Ningefeli vibaya darasani si ungeniona nagombea Uenyekiti wa Chama chako? Kumbe ukitongozwa huwa unajiuma uma vidole mie sitombi watafuna kucha tafuta Mwingine!
uzuri ni kwamba jf inavumilia hata vichaa .
 
Katekwa,Kajiteka au kaenda kwa hawara kula sikuku kuu naye? Ripoti za kupotea mwanamke au msichana mtu mzima ukizipeleka polisi husita kidogo.Wakaishia tu kusema sawa ripoti tumepokea.Maana aweza kuwa kaenda mchepuko.

Hicho kisauti kinachosemekana kinafanana na chake ndio ushahidi tosha wa kusema katekwa na serikali au na polisi?.Hawa waliotoa tamko hilo wana uhakika ni yake au ya kuigiza? wao ni wataalamu wa Forensic? Wakiburuzwa mahakamani waweza toa ushahidi kuwa polisi wanahusika?

Wanasiasa wa Tanzania hasa wa upinzani hawajui sheria.Huyo mfano yuko guest house na hawara ndiko anakopigia wao ndio wanajua aliye guest house na hawara na aliyetekwa?

Anaweza kufanya mchezo wa kuigiza kuwa katekwa ili kupandisha joto la kisiasa lakini ni hatari kwake ikigundulika kuwa wakati anapiga hiyo simu alikuwa kifuani kwa mtu au alikuwa nyumbani kwa nduguze katulia akijifanya katekwa.

Alichofanya yawezekana ni michezo ile ya kitoto unajificha halafu unawataka wenzio wakutafute ulipojificha!!!! Ujinga mtupu.Siasa za kitoto na za kizamani

Mchelea mwana kulia Italia mwenyewe. Subiri siku nduguyo wa damu akifikwa utajua kama alikuwa na mwanaume au lah.Pole lakini
 
Kumbe imetolewa na Mjomba Sugu sawa.Natamani ni mjadili yeye na niiache mada,ila kwavile suala ni la kutekwa Salma, leo sichangii chochote.
 
Back
Top Bottom