GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
- Thread starter
- #81
Walimu wako darasani walikupotosha au umesoma chuo cha kata kama siyo TIA basi IFM vyote hivyo ni vyuo vya kata vinatambulika Tanzania tuHuyu jamaa hajui kabisa uhusiano wa ACACIA na Bulyanhulu anadhani ni kampuni mbili tofauti na anakuja hapa kudanganya watu na kusema ni sub contractor. Watu wengi hawajui kabisa namna haya makampuini makubwa yalivyo majanja ya kuiba kisheria ukizubaa. Nilifanya kazi na kampuni moja inaitwa Skanska Plc, ofisini tulikuwa tuna operate vitabu vitatu tofauti. Skanska kama kampuni tanzu, Skanska Jensen international, na C G Jensen, mabao waliokuwa wanayapiga ni aibu kubwa. report za mwisho wa mwaka zinatengenezwa mbili moja ya kweli na nyingine ya kuonyesha serikalini. Watu kama mleta hoja wanaleta mambo wasiyoyajua wanafuata kelele za kina Zitto na Lissu watu ambao hawajawahi hata kufanya kazi serikalini ama mashirika ya umma ama binafsi zaidi ya siasa.
Kampuni hizo hazikulipa kitu kinaitwa Corporation Tax kwa miaka mitatu mfululizo maana katika P&L Account tulikua tunaonyesha loss hivyo huwezi kulipa kodi kama umefanya biashara katika hasara lakini katika vitabu vingine nyeti kila kitu kinaonekana sawa.
Kuna jamaa alikosana na wakubwa akawachoma aliishia kufukuzwa kazi maana jamaa wa kodi walipokuja walitaja jina lake na wakapewa rushwa kazi ikaendelea kama kawaida.
Ni aibu sana kuona mijitu inapiga kelele kusupport vitu wasivyovijua.