Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini Yagawa Vifaa vya Ujenzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,687
1,238
Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameitisha Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kwa lengo la kugawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo.​

Waliohudhuria Kikao hicho:
(i) Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo
(ii) Sekretariati ya Mfuko wa Jimbo
(iii) Wenyeviti wa Serikali za Vijiji
vili vyotuma maombi
(iv) Wakuu wa Sekondari zilizotuma maombi

Fedha za Mfuko wa Jimbo: Tsh 75,796,000 (Tsh 75.796m)

Vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa:
(i) Saruji Mifuko: 1,970
(ii) Mabati ya rangi: 322
(iii) Nondo, 8mm: 430

Orodha ya Sekondari zilizogawiwa vifaa vya ujenzi:

(i) Sekondari zinazojitayarisha kufunguliwa - Muhoji, Nyasaungu na Rukuba (Kisiwa)

(ii) Sekondari zinazokamilisha ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi - Mtiro, Makojo, Nyambono, Bwai, Mkirira na Etaro

(iii) Sekondari zinazoanza ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi - Bukwaya na Nyanja

(iv) Sekondari mpya zinazoanza ujenzi - Chitare (Kata ya Makojo), Mwigombe (Kata ya Kiriba), Mmahare (Kata ya Etaro), Musanja (Kata ya Musanja), Kataryo (Kata ya Tegeruka) na Nyabakangara (Kata ya Nyambono)

Vifaa vya ujenzi vilivyogawiwa: Kiambatanisho kilichowekwa hapa kinajieleza ipasavyo.

Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha: Washiriki wa Kikao cha Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini. Kikao kimefanyika leo, Kijijini Suguti, Makao Makuu ya Halmashauri yetu (Musoma DC)

Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6, Musoma

Tarehe: Jumanne, 7 Jan 2025

WhatsApp Image 2025-01-07 at 18.38.14 (1).jpeg
WhatsApp Image 2025-01-07 at 18.38.14.jpeg
 
Back
Top Bottom