Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni yaipongeza Kibaha Mji kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,735
13,498
ff99777a-1efd-4096-9de4-9c1b08baf26d.jpg
Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Wizara ya Elimu na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeridhika na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Shimbo iliyopo Kata ya Mkuza,Halmashauri ya Mji Kibaha

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Husna Sekiboko amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ndoto na maono yake ni kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata Elimu bora kwenye Mazingira rafiki ili kuandaa Wataalam kulitumikia Taifa lao na kwamba Kibaha Mji wamesimamia Ujenzi wa shule hiyo kwa viwango na thamani ya fedha inaonekana
d8cc3447-0232-4f13-ace6-7961dc1087e7.jpg
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Leah Lwanji ameieleza Kamati kuwa Jumla ya Shilingi 528,998,425 kupitia Mradi wa SEQUIP zilipokelewa ajili ya Ujenzi wa miundombinu 27 na tayari imekamilika na tayari Wanafunzi 281 kati yake wavulana 149 na Wasichana 132 wameanza kunufaika kwa kuwapunguzia umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 8 kuifuata shule Mama ya Nyumbu.

Mhe.Hamisi Shabani Taletale ameipongeza Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa Mradi na kushauri kujengwa kwa uzio ili kuwawekea utulivu wanafunzi wakati wa Masomo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko ametoa maelekezo ya Kamati kama ifuatavyo;
492bb2d8-995a-459a-9173-6883ebe41e83.jpg

57920a24-c5ae-49be-b59b-4039e1de2805.jpg
Mosi, Shule zote nchini ziwe na utaratibu wa kukagua maudhui ya vitabu kama vinaendana na maadili ya Watanzania kuelekeza vitabu vihakikiwe na kugongwa mihuri wa kuridhia Matumizi na Kamishina wa Elimu nchini.

Pili,Serikali iangalie upya mgawanyo wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya Miradi kwani yapo maeneo wanakamilisha Ujenzi na maeneo mengine hawakamilishi ama Kujenga chini ya Kiwango na kuathiri matarajio na malengo.Ameitaka Wizara ya Elimu kufanya tathmini ya kimaeneo ili fedha zinazotolewa zitosheleze ili kuongeza tija ya Miradi husika

Waziri wa Elimu Prof.Adolf Mkenda ameishukuru Kamati kwa kazi nzuri na kupokea maelekezo yote ya Kamati kwa ajili ya kufanyia kazi

Aidha,Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Sekiboko amempongeza sana Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa Mkurugenzi wa Mji Kibaha kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya Maendeleo kwa kushirikiana na Baraza la Madiwani kuhakikisha Mabilioni ya fedha yanayotolewa na Dkt.Samia Suluhu Hassan yanafanyakazi zinazoonyesha matokeo kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom