Kamati ya Bunge kujadili usalama wa nchi

huyu spika alikuwa mgonjwa nadhani akili bado haijamrudia vizuri.
wabunge wetu wamepiga kelele muda mrefu.....wananchi wanatekwa ,wengine wamepotea leo ndio spika anashtuka???
huyu wamrudishe india akaendelee na matibabu.
Wamtume India kama Katibu.
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kazi yake ni Masuala ya Usalama hivyo wanachojadili ni kazi yake ya kiada ni tofauti na hoja ya Mbowe na Bashe ambao walitaka Bunge lijadili Kama hoja ya dharura sio Kamati ya Bunge ijadili
 
Dola ni lazima iogopwe na wahalifu na vilevile inabidi iaminiwe na watu wake. Hii ni hatua nzuri na naipongeza sana. Ni wakati mzuri wa kujitafakari ni wapi tulitaka kukosea ili kuondoa hofu iliyotaka kujengeka miongoni mwetu. Katika kulinda uhai wa watu wake ni vema hatua ziwe zinachukuliwa haraka, kwa uhakika na haki ili wananchi watekeleze majukumu yao kwa uhuru mpana zaidi kwa maendeleo yetu wote.
Hii haraka mmeiona Leo? KUB alipotoa hoja kama hii mkaona atapata kiki au nini? Nchi hii sijui imelogwa na nani? Yaani hoja yenye maslahi inaweza kukataliwa Leo kwa vile tu imetolewa na mpinzani lakini kesho ikapokelewa kwa mbwembwe kwa vile imetoka ccm!! Mimi niliamini Bunge ni taasisi inayojitambua na isiyo na ubaguzi lakini kwa hizi double standards mnatulazimisha tuwadharau viongozi wa Bunge.
 
Tako hutoa pumzi ya harufu mbaya na wakati mwingine harufu haisikiki !!!!!!
 
Hii nchi iweze kuendelea lazima tukubali tukatae maslai ya Nchi kwanza lakini naona CCM wanatanguliza chama kwanza Nchi baadae
 
Back
Top Bottom