domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,546
- 1,725
Mashujaa wa upinzani wapo, wapo wengi tu, akina Kasanga Tumbo, Kasela Bantu, Mapalala, Chifu Abdala Fundikira, Abbasi Mtemvu, Masumbuko Lamwai, Aman Kaborou, Leo Lekanwa, Mchungaji Christopher Mtikila, Augustino Lyatonga Mrema, Mwaikambo, Mwakitwange, mbona mashujaa wa upinzani wapo walikamatwaa na upinzani ukafika hapa tulipo, tena wengine walikuwa enzi ya chama kimoja, magazeti matatu na radio mbili sembuse sasa vyama vingi, magazeti lukuki, radio usiseme! Upinzani wa kweli utabaki upinzani saka tonge huo utatoweka!