Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Ushawahi sikia siku polisi wanatangaza mtu kafa hana ndugu? Watu kibao wanakufa wanazikwa na halmashauri kimya kimya bila kelele
Swali lako halijaeleweka vizuri ila nikujibu tu...

Polisi kawaida hutoa ripoti za matukio mbalimbali iwe ya kihalifu au ajali ili kuuhabarisha umma, mfano matukio ya ujambazi mara nyingi husema wamekamata majambazi kadhaa yakiwa na silaha wakitaka kwenda kufanya uhalifu/wakiwa eneo la tukio wakifanya uhalifu.

Pia huripoti matukio ya ajali, ambapo husema ajali imetokea eneo fulani ambapo majeruhi au marehemu ni idadi kadhaa, na majeruhi hao au miili yao imehifadhiwa kwenye hospitali fulani..
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi @ Babu G...
Tangu tarehe 10 April mpaka jana tarehe 22 April Polisi walishindwa kutangaza kuokotwa kwa maiti ya mtu huyo ‘aliyegongwa na gari’ pamoja na jitihada zote za ndugu zake kumtafuta? Waliuhifadhi huo mwili ili iweje?

Maeneo ambayo ndugu walimtafuta ni pamoja na vituo vua Polisi, je Polisi walishindwa kuangalia kwenye Mortuary yao?
 
Yaani Ndugu yenu anauawa kinyama halafu mkihoji mnakamatwa .

Screenshot_2024-04-23-19-37-47-1.png


Mungu ibariki Tanzania
 
Ila ukisikiliza maelezo ya Kamanda Muliro, kuna namna Jacob kakosea. Inaonyesha kuwa hata ndugu zake na huyo Marehemu wamekubaliana na maelezo ya Polisi.
 
Na
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi @ Babu G. ambaye picha yake imeambatanishwa kwenye taarifa hizo kuwa alipotea tarehe 11 Aprili, 2024 na baadae kugundulika katika Chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road huku ikidaiwa Polisi kuhusika na kifo hicho kwa kumuua..

Ukweli ni kwamba tarehe 11 Aprili, 2024 majira ya saa 10 Alfajiri Askari Polisi wa Usalama barabarani alipewa taarifa na mwananchi kuwa eneo laTaa za kuongozea magari za Buguruni, Ilala mtu mmoja mwanaume aliyekuwa akivuka barabara eneo hilo la Kimboka kuelekea Chama aligongwa na gari ambalo halikusimama (hit and Run).

Mtu huyo alipata majeraha makubwa kichwani, kifuani na eneo la chini la mgongo na kisigino cha mguu wa kulia. Eneo hilo lina watu wengi ambao wanakesha kwa biashara mbalimbali na walishuhudia tukio hilo.

Mtu huyo alipelekwa haraka hospitali ya Amana na Polisi lakini baada ya kumfikisha Madaktari walibaini kuwa mtu huyo alikuwa tayari amekwishafariki, Kwa sababu chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Amana kilikuwa hakina nafasi, ilishauriwa akahifadhiwe kwenye Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyo barabara ya Kilwa Temeke ambayo inatoa huduma hata kwa raia kuhusiana na suala hilo.Tarehe 21.4,2024 ndugu wa marehemu walipatikana na wakautambua mwili wa ndugu yao kwani hakuwa na kitambulisho wala simu. Taratibu za mwisho za mazishi zinafanywa ili akazikwe.

Kutokana na taharuki iliyotengenezwa na kujengwa kwa makusudi na mtu anayejiita Malisa gj na Bonoface Jacob ambao kwenye “post” zao walionesha nia ya wazi ya kutengeneza chuki dhidi ya Polisi na Serikali kwa wananchi kuwa mtu huyo aliyepata ajali alikuwa ameuawa na Polisi , Kitendo kilichofanywa na watu hao ni kosa kisheria na hakivumiliki na lazima Jeshi lichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwakamata , kuwahoji kwa kina na kuwafikisha mahakamani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la Polisi halitavumilia watu ambao wanaibuka na taarifa za uongo na uzushi ambazo zinalenga kujenga chuki na taharuki kwa wananchi. Jeshi litaendelea kusimamia misingi ya kisheria na halitakuwa na huruma kwa mtuhumiwa yoyote wa kihalifu na litamshughulikia haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Pia soma:


Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?
Muhimbili nako kulijaa?
 
Ile report hapana ni kupikwaaaa
Sasa kama ya kupikwa mbona Ndugu wa Marehemu wameridhia ila Boni ndo anapinga..?
Hivi kweli Boni hajui kwamba anatakiwa akafungue kesi ya kuomba uchunguzi wa mwili kama ana mashaka yeyote..? Mbona hafanyi yote hayo..?
 
Back
Top Bottom