Mngurimi
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 819
- 790
Wakubwa kwa wadogo, itifaki imezingatiwa
Nianze kwa kurudia kusema kuwa, mimi ni non aligned kwa maana ya kwamba "sifungamani na chama chochote cha kisiasa nchini. Hata kama sifungamani na upande wowote lakini bado katiba inaniruhusu kufanya yangu pale kwenye sanduku la kura mnamo tarehe 28 mwezi Oktoba 2020.
Ni takribani siku 11 sasa tangu kampeni za uchaguzi mkuu ziruhisiwe rasmi na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC). Tathmini yangu kwa ufupi, naona mpambano mkali bado upo kama ule wa mwaka 2015 yaani ni vyama viwili vya CHADEMA na CCM ndivyo vinachuana vikali. ACT Wazalendo nao wapo kidogo japo sio kwa kiwango cha CCM na CHADEMA. Bado ni mapema sana kusema nani anaweza kutwaa mikoba ya nchi kwani siku za kampeni kuwashawishi wananchi zipo za kutosha. Baada ya hayo turudi kwenye mada kama heading inavyojitanabaisha.
Kama watu wengine, nami ni mazoea yangu kufuatilia matukio mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya nchi kupitia vyombo vya habari hasa vya hapa nchini kwetu. Moja kati ya habari ambazo kwa sasa raia tunazifuatilia kwa ukaribu sana ni habari za uchaguzi mkuu wa bara na visiwani.
Hadi kufikia leo bado naona kasi ya kuoneshwa kwa matangazo ya mikutano ya upinzani kwenye vyombo vya habari vya nchi hii inazidi kupungua sana. Kwa Chama cha Mapinduzi kwao naona hali ipo vizuri maana vyombo vya habari vingi kila kukicha utaona ni wao tu japo vyama vingine pia vinahitaji kuuza sera zao kwa wananchi. Hii imenijengea maswali kadhaa ambayo majibu yake yanaweza kuwa wazi au yasiwe wazi.
Nimekuwa nikiwaza, labda media zinahitaji pesa kubwa ili kurusha matangazo hivyo kusababisha cost kubwa ambazo vyama vya upinzani vimeshindwa kumudu?
Nimekuwa nikiwaza, labda vyombo vya habari vinaona kampeni za CCM ndizo zina mvuto sana kwa watazamaji wao kuliko zile za upinzani?
Nimekwenda mbali zaidi nikawaza labda kuna shinikizo kutoka mamlaka fulani kuzuia kuonesha matangazo ya vyama vya upinzani?
Maswali yote hayo yamenijia baada kufuatilia tangu kampeni zianze na niliwaona TBC1 pekee ambao walirusha ufunguzi wa kampeni za CHADEMA japo kwa kukatakata matangazo. Leo nimefuatilia UTV, TBC1, Star Tv na Channel 10 wote wanarusha matangazo ya kampeni za mgombea wa CCM Dkt. JPM akiwa Simiyu. Clouds wao hawana muda kabisa naona ni muziki tu labda bado wamejawa woga baada ya ban ya wiki moja.
Hii imenipa kitu kwenye fikra zangu na kuja na huu uzi kwenu CHADEMA kama mambo yataendelea kuwa hivi, hakika kushinda uchaguzi huu litakuwa ni jambo gumu sana kwenu. Nadiriki kusema hivi kwa sababu vyombo vya habari vina nguvu sana ya kueneza sera iwe mjini na vijijini. Kutembelea mikoa na wilaya pekee bado haitoshi kwa sababu zifuatazo:
i. Sio wakazi wa eneo husika wote hupata nafasi ya kuhudhuria mikutano ya kampeni.
ii. Mara nyingi mnatembelea sehemu za mijini tu na sio vijijini ambako ili sera zenu zienee vema yapaswa media ziwabebe.
iii. Media zinaheshimika sana kwa jamii yaani mtu anaamini sana kitu anachokisikia kwenye radio/TV kuliko source nyingine.
Kwa kusema hayo, naomba CHADEMA mtafute njia mbadala ili muweze kujinusuru na hili. Ogopa sana mtu anatembea kila mtaa akinadi sera zake huku wewe media zikikukaushia tu. Nasikia hadi matamko ya vyama vya waandishi wa habari vikiwataka muombe radhi, tafadhali fanyeni kila muwezalo habari zenu zipate airtime ila tofauti na hapo bado nafasi ya kushinda kwenu ni 20%.
Nafasi mliyobakiza ya kuwabeba kidogo ni huku online ambako nako sio wote wanaowapa support ipasavyo. Wapo wanaowaunga mkono wengi na wachache wanaowapinga lakini kumbuka kuwa idadi ya watumiaji wa hii mitandao ni ndogo sana kuliko wasiotumia.
Yangu ni hayo na ninawatakia kila la kheri, naomba kuwasilisha.