Kama una gari hizi Prado 95 au Prado 120 (diamond) pitia hapa upate moja mbili, ikuingizie kipato

Padidu G

Member
Jun 25, 2021
18
20
Kuna Watu Mmejaaliwa vipandwa na miongoni mwa vipandwa hivyo ni aina ya hizi gari PRADO 95 (MCHAGA),PRADO 120 (DIAMOND) Hizi gari zinaweza kukusaidia kuingiza kipato kwa kukodisha kwa watu binafsi au Makampuni

Mie ni Dereva wa tours kwa miaka kadhaa sasa na utafiti Wangu nilioufanya ni kua Gari inarudisha Pesa Haraka kuliko Nyumba lakini Nyumba inadumu mda mrefu na gari haidumu muda mrefu (Inategemeana na dereva/Msimamizi wako)

Mfano wake ni huu katika soko la ukodishaji PRADO 120 DIAMOND ndo gari zilizopo kwenye Soko sana na Ukodishaji wake upo kama hivi

Ukipata kazi mkononi yaani wewe bila kupitia kwa Kampuni au dalali Bei Hua Ni laki tatu (300,000) mpaka laki mbili na hamsini (250,000) kwa siku na hapo mafuta anaweka mteja

Na Ukipata kazi kupitia kampuni au Dalali Malipo hua Wanalipa kwa Siku laki mbili (200,000) Mpaka laki na hamsini (150,000) mafuta ni kwa mteja

Kwa Hizo PRADO 92 (MCHAGA) Bei Yake Hua ni laki mbili (200,000) ukipata kazi mwenyewe na ukipata kwa kampuni au dalali hua wanalipa laki na hamsini (150,000) kwa siku mafuta kwa mteja

Ukipata kazi ya week mbili au zaidi utajua wewe unapata bei gani unatumia bei gani na unampa dereva bei gani ila Madereva mara nyingi hua wanalipwa elfu hamsini (50000) kwa siku

Hii akiwa safari maana kuna kulala kula na mengine kama hayo na akiwa mjini hasa mfano kwa Dar hua dereva anachukua elfu thelathin (30000) na pesa hii inakua anatoa Tajiri kwenye makubaliano ya gari

Kama utalipwa 250000 Utatoa 50000 kwa Dereva

CHANGAMOTO: MALIPO kuchelewa au kuto kulipwa kwa wakati pindi unapofanya kazi hii inatokana na kampuni nyingi hawana mitaji ya kutosha kumudu kazi husika

Hua wanasubilia kulipwa ndo walipe na wachache hua wanalipa Advance kisha ukimaliza kazi unamaliziwa pesa yako hapo kwenye Advance hata kama kampuni haina Mtaji wa kutosheleza hua ni jambo la lazima kwa kabla Ya kazi

USHAURI: Ukivutika kufanya biashara hii kwa mwanzo fata utaratibu ambao umewekwa na LATRA na Draft MKATABA WAKO ambao utampa pia mtu anaechukua gari lako kama ni kampuni au mtu binafsi

Katika mkataba huo base sana kwenye malipo utalipwaje ili ukifanya kazi usije kusumbuka mbeleni

Ukiwa na Gari Unataka Tufanye kazi karibu Na kwa Ushauri Zaidi Karibu pia Inbox au niandikie email (Mstaarabu92@yahoo.com)
 
Kwann haujaweka picha ya hizo gari?! Wengine hawafahamu zipoje na zinafananiaje, pengine wanazo au wanajua ndugu wenye nazo na zimepaki tu?!

IMG_0563.jpg

Hiyo ndio Prado diamond

IMG_0564.jpg

Hii ndio prado mchaga au mkulima.
 
kuna Nissan Patrol Y61, 2002, Black, Good Condition. Offer zenu zikoje? (Terms- Dereva lazima awe wangu))
 
Back
Top Bottom