``` 1. *Mwenzako akinyolewa tia maji.* -Siku hizi tunanyoa kwa mashine. Ukitia maji zinateleza hazinyoleki.
2. *Barua ni nusu ya kuonana.* -Siku hizi watu wanaonana kwa watsap. Mkingojea barua mtakufa bila kuonana.
3. *Akili ni nywele.* -Vipi kuhusu Mawigi?
4. *Mchagua jembe si mkulima.* -siku hizi tunatumia zaidi matrekta ya kukodi
. 5. *Alalae usimuamshe akiamka utalala wewe.* -siku hizi unaweka alam mwenyewe unaamka hausubiri kuamshwa na mtu.
6. *Polepole ndio mwendo.* -siku hizi kuna mwendo kasi ukienda polepole utabaki. *Hatupendi mambo ya kizamani...*