Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma Ujumbe Gani kwa TV yake ya TBC?!.

... ni matumizi mabaya ya muda, na kaonyesha mfano mbaya sana. kesho si ajabu kusikia waigizaji wenzake akina kingwngala, n.k. nao wanaiga
 
Acha uswahili mzee yan hiyo ni moja ya kukuza uhuru wa mawasiliano na kuwafanya vituo vingine waongeze ufanisi yan kama unajiuliza swal dogo kiasi hcho akili yako ww tunaitilia mashaka
Mkuu Dukila, kabla ya hii elimu bure ya Magufuli, elimu ya Mtanzania ni elimu ya darasa la saba, hivyo nakuomba usiitilie shaka elimu yangu, mimi elimu yangu ni darasa la saba la UPE na nilihitimu shule ya Kolomije na niliishia hapo. Watanzania wengi hiki ndicho kiwango chetu cha elimu ya Mtanzania.

Paskali.
 
Wanabodi,

Kitendo cha Rais Dr. John Pombe Magufuli, kuangalia Clouds TV na Kuipongeza, kimeniacha na maswali mengi kuliko majibu, mojawapo likiwa ni kama rais anaangalia Clouds TV, nani anaangalia TBC?!.

Pongezi zake kwa Clouds Media pia zimetuma ujumbe mzito silently kwa TBC ambayo ndio TV yake na Redio Yake, kama Rais anatazama TV ya watu wengine na kuipongeza kwa kazi nzuri, vipi kuhusu TV yake?!, Kama rais hatazami TBC, na badala yake anatazama Clouds TV, na kuipongeza, then nani anatazama TBC?!.

Kitendo cha mwenye TV kutoiangalia TV yake, kinatuma ujumbe kuwa jee kuna uwezekano rais haangalii TBC kwa sababu inaboa?!, hivyo anaangalia Clouds TV kwa sababu imechangamka?!, na ndio maana amaipigia simu kuipongeza?!.

Au kunauwezekano, rais anaangalia TV zote ikiwemo Clouds TV na pia anaangalia tv nyingine ikiwemo TV yake ya TBC, na TBC pia inafanya vizuri, na inastahili pongezi za rais, lakini kwa vile TBC ni TV yake, kufuatia kanuni ya usijisifu, bali usubiri kusifiwa, then hata TBC ifanye vizuri kiasi gani, bado rais Magufuli, hataisifu kwa hoja, haistahili kusifiwa na rais, bali ameisifu Clouds kwa sababu ni ya wengine, na imefanya vizuri kuliko ilivyotarajiwa!.

Au pia inawezekana ni.ile tabia tuu na yale mazoea ya mtu kudharau chake na kuthamini cha mwenzie?!.

Hongera sana Rais Dr. John Pombe Magufuli hongera sana for reality, simplicity, genuinity na being down to earth, kwa kupiga simu Clouds TV, kwa vile Clouds media ni "the peoples station, then you are A man of the people!.

Paskali

Kwa kweli Kaka Paskali TBC inaharibu sana, yani mimi hata nikiiweka kimakosa nashtuka automatically moyoni, simply useful na HAIFAI. Kwa mfano hii habari fake ya TRUMP, imenisikitisha sana, wakati mwingine waweza kusema labda kikundi cha watu kinataka au kimepanga kumsifia rais, kumbe ni watu wachache na bila sababu. This is very wrong in deed. Ahsante kwa kupembua vizuri.
 
Yani umemuona Magufuli mshamba kiasi hicho mpaka aangalie tbc?
Kwani lazima aingalie tbc
Wakuu Jungle Warrior na Moto Chini, TBC ndio TV pekee ya taifa, hivyo suala la rais ambae ndiye Mkuu wa nchi kuangalia TBC sio issue ya ushamba au a matter of choice kuwa rais yuko huru kuangalia TV yoyote na kuipongeza, lakini kwa rais kuangalia TBC sio a matter of choice, ni compulsory as an obligation, yaani ni wajibu rais wetu kuangalia TBC kwa sababu rais ndiye Editor in Chief wa vyombo vyote vya habari vya umma kwenye organization setup zao, hivyo suala la rais kuangalia TBC sio a matter of choice ni must, awe anaipenda au haipendi, iwe inamfurahisha au haimfurahishi, kuangalia ni wajibu, ila rais kuangalia TV nyingine zozote ndio a matter of choice na kwenye kupongeza pia its a matter choice kupongeza chochote kile kinachomfurahisha.

Rais kama alivyo Commander in Chief wa majeshi yetu ataonekana ni mtu wa ajabu kama atasifia tuu majeshi ya jirani na kukaa kimya kuhusu majeshi yake, kwa sababu kusifia has something to do with encouragement and boosting morale ya wapiganaji wetu, vivyo hivyo kwa hao wapiganaji wake kwenye sexta ya media.

Paskali
 
Binafsi siamini kama kweli Raisi Magufuli aliamka tu asubuhi akaamua kupiga simu clouds, bali ni jambo ambao lilipangwa na hata clouds wenyewe walijua ni kama vile tu viongozi wa Marekani wanavyozukia ma talk show ya akina sijui David Letterman huwa kila kitu kimeshapangwa na hata maswali ya kuulizwa anakuwa alishapewa na kuyafanyia mazoezi!

Vivyo hivyo hapa clouds walijua kila kitu sasa kwa nini Magufuli aliamua kuwapigia simu clouds hilo analifahamu yeye mwenyewe na watu wake inawezekana kabisa ni moja kati ya ulipaji wa fadhila kwa wote waliojitolea kwa hali na mali kwenye kufanikisha ushindi wake ambapo clouds entertainment wana mchango wao mkubwa tu sana ukichukulia tayari Raisi Magufuli ameshakutana na wasanii Ikulu kwa lengo hilo hilo!

Kumbuka Raisi Magufuli ni mtu smart sana klk wengi mnavyodhania na hakuna kitu anachofanya ambacho hajakipigia mahesabu nakumbuka wakati alipokutana na Wasanii mpaka aliimba wimbo wa Malaika msanii ambaye hata hajulikani na mwenyewe Malaika hakuamni macho yake kwamba Raisi anamkumbuka, huyu Malaika alimtungia wimbo maalumu Magufuli wakati wa kampeni!
Ndiyo maana unaona hata aliwataja kwa majina watangazaji wa clouds yote hii ni kuwafanya tu wajisikie kwamba Raisi ni wa watu na anayejali maisha ya kila siku ya Mtanzania wa kawaida!


Raisi Magufuli atakuja kuwashangaza watu sana huko mbele, dont understimate him this guy is very intelligent kuliko mnavyodhani kila kitu anachofanya ukikichunguza kiko well calculated!
Kuna sababu kwa nini Mtu kama Mwapachu ameongea alivyoongea na kuamua kurudi CCM, mwanzoni walimu underestimate lkn wameona kwamba Magufuli ni namba nyingine kabisa!

Hivyo ndiyo ninayohisi ni sababu ya yeye Raisi na Mke wake kuwapigia simu clouds!


Kuhusu TBC hilo liko mikononi mwake na TBC itatoboa tu nina uhakika mipango iko jikoni!
Mkuu Barbarosa, nimeipenda objectivity yako na mtazamo kuwa hakuna coincidence, everything ni pre meditated na calculated move, jee unamaanisha hata zile ziara za kushukiza zilikuwa ni maigizo?!. Nijuavyo mimi ni kweli kuna vitu rais Magufuli anapanga mwenyewe na ni kweli anashtukiza, kama hili la kupiga simu ni la kushukiza kwa sababu asingepata clearance ya wale 'jamaa', ila ile ya Obama kupanga foleni kununua burger was premeditated na calculated move.

Paskali
 
Hahaha! Safi sana inaonesha anaangalia station za nyumbani na sio DSTV ..
Huu ndio uzalendo, na hivi ndivyo inavyopaswa kufanywa na Watanzania wote hadi walioko ughaibuni at least once in a while kuangalia local contents from home.

Paskali
 
Mnataka kudhani rais ni mjinga kiasi hicho mpaka apoteze muda wake kuangalia TBC??
 
Kwahiyo mlitaka Rais azipigie simu TV na redio zote anazoangalia na kusikiliza ndio mjue anaangalia na kusikiliza vyombo gani?
Mkuu ZeMarcopolo, hapana, it's just a nod from a concerned citizen kusikiliza what does that mean kwa TV yetu ya TBC.

Paskali
 
Sasa Kaka, boresheni basi TBC, twawezaje kuwa wazalendo na TBC wakati hakuna kitu?
Mkuu uttoh2002, naunga mkono hoja ya kuandaa vipindi bora na interesting to watch, not necessarily TBC tuu, local contents za TV zote ziko available online.
Paskali
 
Wakuu Jungle Warrior na Moto Chini, TBC ndio TV pekee ya taifa, hivyo suala la rais ambae ndiye Mkuu wa nchi kuangalia TBC sio issue ya ushamba au a matter of choice kuwa rais yuko huru kuangalia TV yoyote na kuipongeza, lakini kwa rais kuangalia TBC sio a matter of choice, ni compulsory as an obligation, yaani ni wajibu rais wetu kuangalia TBC kwa sababu rais ndiye Editor in Chief wa vyombo vyote vya habari vya umma kwenye organization setup zao, hivyo suala la rais kuangalia TBC sio a matter of choice ni must, awe anaipenda au haipendi, iwe inamfurahisha au haimfurahishi, kuangalia ni wajibu, ila rais kuangalia TV nyingine zozote ndio a matter of choice na kwenye kupongeza pia its a matter choice kupongeza chochote kile kinachomfurahisha.

Rais kama alivyo Commander in Chief wa majeshi yetu ataonekana ni mtu wa ajabu kama atasifia tuu majeshi ya jirani na kukaa kimya kuhusu majeshi yake, kwa sababu kusifia has something to do with encouragement and boosting morale ya wapiganaji wetu, vivyo hivyo kwa hao wapiganaji wake kwenye sexta ya media.

Paskali
Mkuu kwa kilichotokea majuzi pale TBC mpaka baadhi ya waandishi kusimamishwa ni ushahidi usio na shaka kwamba hata viongozi wetu hawana imani na hiki chombo cha habari?
 
Nachokiona ni taofaut kabisa na watu wanavyowaza humu.

Kwanza
Maguful anauhakika na TBC ya kwamba hata asipoitazama ama kuipigia simu kuipongeza still itazidi kubroadcast mambo yake na kumsifia (refer habari ya trump),mh hana wasiwasi na TBC pamoja na wafanyakazi wake anajua ni wake tu.


Pili.
Anajua clouds ni media inakuwa kwa kasi (kuifunika IPP media) na anaamini kwa kuwa clouds media walikuwa nyuma yake since kampeni ni inatizamwa na kuangaliwa na vijana wengi ni muda mwafaka wa kuwasika maskio na kuwapongeza hata katika vile vipindi ambavyo havitupeleke kwenye ile nchi yake ya viwanda (SHILAWADU) sababu hutizamwa na kuskilizwa na vijana wengi.

Redio ya watu plus raisi wa watu.
Shilawadu
 
Back
Top Bottom