Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 6,696
- 6,733
Kuna tetesi kuwa Maboresho yatakayofanyika katika reli ya TAZARA yanahusisha kuifanya reli hiyo kutumia treni ya dizeli kama Kenya.
Kama huu ndo ukweli napenda kuzishauri mamlaka za Tanzania kuukataa huu mradi.
Kama tumeweza kujenga reli yetu ya kati kwa kiwango cha SGR tena umeme itakuwa ni aibu na fedheha kuu tukijengewa kwa mkopo reli ya TAZARA iliyo na kiwango cha kutumia dizeli.
Mchina asitupande kichwani. Kama Zambia hawawezi kuwa na treni ya Umeme tumwambie kwa kujiamini kuwa kipande cha reli hii kwa upande wa Tanzania lazima kiwe na viwango vya kutumia umeme.
Akibisha tuachane nae tufanye kama Magufuli alivyoachana nao na kwenda kwa Waturuki kwenye SGR Reli ya Kati
PIA SOMA
- Maboresho ya Reli ya TAZARA yaangalie usifanyike udanganyifu kama wa Kenya
Lake Oil, Oil Com, GBP na wengineo watauza wapi mafuta?