Kama CCM na Upinzani wanaungana kutetea Maovu, kuna haja ya kuwa na Vyama vya upinzani.?

Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
Mkuu idawa, unaikumbuka ile issue ya wabunge watatu wa CCM kupelekwa mahakamani pale kisutu?. Tangu ilipoibuka ile issue heshima yangu kwa wanasiasa imepungua sana.

Ni kundi jingine la wachumia tumbo, ni kundi jingine la wafia maslahi, ambao wanatumia hadhi zao katika kutetea maslahi yao.
 
Kumbe kazi ya CCM ni kutetea uovu hapa nchini! Sikuwa nafahamu. Huyu mleta ni hovyo sana siku hizi. Mleta nada usiichafue CCM tafadhali!
 
Tuache kuongea kwa chuki ...Makonda ametoa kauli gani ya kudharau Bunge? Mbona kuna vitendo vingi tu vya dharau kwa bunge hatujawahi kuona wakiungana kwa nguvu hii? Pamoja na mapungufu ya Makonda lakini wanasiasa wetu wanajali maslahi yao kupitia kujifanya wanatutetea. Hivi Polisi walivyofika viwanja vya bunge kumkamata Lissu kwanini uongozi wa bunge haukuzuia kwasababu ya kutopewa taarifa? Siasa za nchi hii zimevurugwa mno!
Mkuu mtazamo!

Shida iko kwa namna mtoa mada alivyoconclude ujumbe wake kwetu...

".......... hakuna haja ya kuwa na upinzani"

Kwanini asiseme hakuna haja ya kuwa na CCM - CHAMA DOLA?

Maana ake anathibitisha CCM ni waboooovu na upinzani unawaanga mkono siku hizi...

Tukirudi kwenye mada.. Umeuliza Makonda amelidharau vipi bunge!! Je kusema watu wanasinzia tu na kuna wachekeshaji kama mkuu wa mkoa ni sawa kikazi? Bunge duniani kote huheshimiwa sana na mihimili mingine kwasababu ndio unaoleta check and Balance! Na tena kwa nchi nyingine hutumika kuidhinisha nyadhifa nyingi zilizopo kwenye EXECUTIVE.

My take!

Kiti cha Spika kilitaka kuachia Bunge lutumiwe na executive vibaya... Naona Spika amekumbuka - which is great. Nakumbuka ni executive ndio iliyoleta mswaada wa kutonyesha Bunge live na wao wakapitisha kiajabuajabu. Hata ile issue ya kusitisha ajira waliunga tela tu bila kuwa critical kama wabunge. Bora wamejirudi labda hata mambo yataanza kwenda vzuri.
 
Wabunge wote wameungana bila kujali vyama vyao kupinga vita ya madawa ya kulevya.

Wote wanaongea lugha moja, wanagonga meza pamoja, wanashangilia pamoja....

Wote wameungana kuangamiza Taifa kwa madawa ya Kulevya....

Je, Kuna umuhimu wa kuendelea na vyama upinzani Tanzania......?
hama tu nchi mkuu, usipate pressure.

lol...
 
Kumbe kazi ya CCM ni kutetea uovu hapa nchini! Sikuwa nafahamu. Huyu mleta ni hovyo sana siku hizi. Mleta nada usiichafue CCM tafadhali!
Kwa sisi tuliochoshwa na CCM tunahitaji chama mbadala..... Sasa inapotokea chama kinachotakiwa kuwa mfano kwa chama tawala kikafanya Madudu yaleyale..... Lazima tuhoji uwepo wake kama kinastahili.
 
Mkuu idawa, unaikumbuka ile issue ya wabunge watatu wa CCM kupelekwa mahakamani pale kisutu?. Tangu ilipoibuka ile issue heshima yangu kwa wanasiasa imepungua sana.

Ni kundi jingine la wachumia tumbo, ni kundi jingine la wafia maslahi, ambao wanatumia hadhi zao katika kutetea maslahi yao.
Mkuu hawa wabunge ukiwachunguza sana unajisemea tu bora Magufuli afanye tu anavyoweza.
 
Huko ni kupambana na dawa za kulevya au ni kuonyesha upumbavu kutoka kwa Makonda? Yani umetega sikio kabisaa kuwa Makonda anapambana na mihadarati? Pole sana kwa kukosa uelewa!
 
Wanapambana na comedy sio kupinga harakati,zinatakiwa zifwate na ziheshiwe taratibu na sio mihemuko.
 
Back
Top Bottom