Kama askari wanaolinda hifadhi wamegeuka wauaji, basi Bunge libadili Sheria ili wanajeshi wapewe jukumu la kulinda hifadhi zetu

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
3,806
10,885
Kumekuwepo na ongezeko la mauaji ya raia yanayosababishwa na askari wa wanyamapori na wale wanaolinda hifadhi za taifa.

Hii siyo picha nzuri na imewafanya wananchi wanaoishi maeneo hayo kuishi kwa hofu kubwa wengine wakipata ulemavu wa maisha kwa sababu ya ukatili wa askari hawa.

Serikali ikiona inafaa basi hifadhi zetu hizi zilindwe na wanajeshi ili hawa askari wa wanyamapori walioshindwa majukumu yao na kugeuka majangiri ya binadamu yawajibishwe.
 
Unahisi hao askari ndio itakuwa bora?

Hujawahi ona matukio ya askari na raia mitaani?

Hawa askari wa TPDF unaosemea hawajajifunza kulinda wanyamapori, ni wastage of resources

Hao askari wa hifadhi hiyo ndio kazi yao, wamesomea hiyo hakuna sababu kuwaondolea jukumu lao sema wabanwe wafanye kazi kwa weledi, tatizo la nchi hii watu wanapenda mno kutumia madaraka yao kuonea wenzao, sio polisi wala migambo wala mahakimu!

Mkuu usipende sana kila kitu kifanywe na askari, naona siku hizi wanaingia kwenye kila kitu kuanzia siasa hadi mambo ya kiuchumi. Hii si sawa. Tuwaachwe wabakie makambini waendelee na majukumu yao
 
Back
Top Bottom