Kama anayofanya Rais Magufuli ni kwa mujibu wa Katiba, basi Katiba ibadilishwe

Hakuna aliezuia, ila nachofanya nyinyi sio siasa ni upuuzi tu.
Mnaanza kukimbia kivuli chenu wenyewe. Mmewabeep watanzania, sasa wamewapigia mnakata simu.

Hizi sio zama za zidumu fikra zake Rais. Ukipuyanga ukarudishwa kwenye mstari. Katiba ipo na ifuatwe.
 
Kwa heshima na Taadhima napenda kumkumbusha Rais Magufuli kuwa, nchi yoyote duniani inaongozwa kwa Katiba ya nchi husika, na sio Ilani ya Chama. Ilani ya Chama hutumika tu kuomba ridhaa ya wananchi (kura), ili Chama husika kipate kupewa Mamlaka ya kuongoza nchi, chini ya Katiba.

Kuzuia vyama vya Siasa hasa vya Upinzani kuendesha shughuli zake za kisiasa, kwa kisingizio cha kukwamisha ahadi za Ilani ya Chama Chako CCM, ni hatua hatari sana ya kutokufuata Katiba ya nchi, ambayo ndio sheria mama inayoongoza nchi.

Kumbuka Ilani ya CCM haiwezi kuwa mbadala wa Katiba ya Nchi. Na madikteta wote duniani hupuuza Katiba.

Nakuomba na Kukusihi kwa jina la Mwenyezi Mungu, uongeze nchi kwa mujibu wa Katiba, ili usije ukaingia kwenye kumbukumbu za madikteta wa Dunia.

Nawasilisha.
Hiyo ilani ndiyo aliyoinadi. CUFnao walibadi ilani yao wakashindwa. Kama wananchi walizikubalu ilanu zake kwa ninu asipewe nafasi ya kuitekeleza. Kwsni Katiba inapinga amani?
 
Nj kipengele gani kimevunjwa cha katiba na uongozi haufanywi ndani ya box tu kuna wakati unjiongeza ili mambo yasogee
Kuna kipengere kinachosema ni kazi za vyama kufanya siasa muda wote. Unaposema hapana unakuwa unaenda kinyume na kipengere hicho.
 
wapi katiba imekanyagwa, msije mkawa mnapayuka tu humu jf
Shughuli za Vyama Vya Siasa vya Upinzani zimezuiwa mpaka 2020, kwa kisingizio cha kukwamisha utekelezaji wa ahadi za Ilani ya CCM, kinyume na Ibara ya 3 ya Katiba ya Tanzania.
 
Shughuli za Vyama Vya Siasa vya Upinzani zimezuiwa mpaka 2020, kwa kisingizio cha kukwamisha utekelezaji wa ahadi za Ilani ya CCM, kinyume na Ibara ya 3 ya Katiba ya Tanzania.

hakuna aliyezuia, kwa sababu akili zenu fupi ndio maana mnashindwa hata kumwelewa raisi. nendeni mahakamani basi kama katiba imevunjwa.
 
Karibu Donald Trump! Sisi Waafrica Bila Mjeled Hatuendi Kuna Watu Wanatawala Kanchi Kamoja tu Lakini Kiburi Walichonacho Utadhani Wanatawala Ulimwengu Mzima. Njoo Baba Utunyooshee !!
 
Back
Top Bottom