Kama 70% ya Umeme Wa Tanesco ni wa Gesi, Mbona Maji yanasingiziwa sana?

Blender

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
4,672
7,711
“Kwa wastani umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia ni takribani asilimia 65 mpaka 70 ya umeme wote unaozalishwa nchini. Wataalam wanatuambia kwamba kama tusingekuwa na gesi asilia, tatizo la umeme nchini lingekuwa kubwa zaidi. Kwahiyo, tushukuru sana Mungu kutuletea rasilimali hii ya gesi asilia.” – Rais Samia Suluhu.

20240203_180605.jpg
 
Nchi ambazo hazina gesi wanategemea umeme wa nini?
Na hiyo gas anayo isemea , ikianza kuchakatwa Kwa ajili ya matumizi ya umeme wa nchi nzima na matumizi mengine ya kuuza nje ya nchi basi , haizidi miaka 38 gesi ya mtwara inakuwa inekushwa ,

Tuna Rudi kulekule
 
Na hiyo gas anayo isemea , ikianza kuchakatwa Kwa ajili ya matumizi ya umeme wa nchi nzima na matumizi mengine ya kuuza nje ya nchi basi , haizidi miaka 38 gesi ya mtwara inakuwa inekushwa ,

Tuna Rudi kulekule
Ndo hapo sasa tutanunua umeme toka kenya
 
Nimeingia hapa stand Gerezani muda huu pale nje wakatisha tickets hawatoi huduma sababu umeme ulikatika na jenereta hawana.

Mambo ya ajabu kabisa,facility kubwa kama hii kushindwa kutoa huduma kwa wananchi halafu kuonekana jambo la kawaida sijui kama tuna viongozi wanaojitambua,nimeuliza so umeme usiporudi hakuna atakayesafiri wanasema hilo wao siyo juu yao
 
Unataka kusemama Nini....!Kamanda!

Ngoja nijifarji na Ngoma,Nyimbo za harakati! Za Wagosi wa Kaya.

"Umeme na Maji,Tanzania vishakuwa kero,Watu kero KERO"
 
“Kwa wastani umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia ni takribani asilimia 65 mpaka 70 ya umeme wote unaozalishwa nchini. Wataalam wanatuambia kwamba kama tusingekuwa na gesi asilia, tatizo la umeme nchini lingekuwa kubwa zaidi. Kwahiyo, tushukuru sana Mungu kutuletea rasilimali hii ya gesi asilia.” – Rais Samia Suluhu.

View attachment 2893074
Hii gesi ni ile wanayomiliki wachina?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Kwa wastani umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia ni takribani asilimia 65 mpaka 70 ya umeme wote unaozalishwa nchini. Wataalam wanatuambia kwamba kama tusingekuwa na gesi asilia, tatizo la umeme nchini lingekuwa kubwa zaidi. Kwahiyo, tushukuru sana Mungu kutuletea rasilimali hii ya gesi asilia.” – Rais Samia Suluhu.
20240203_180605.jpg
.

Hio 30 nayo imegawanyika kwenye Mafuta, Makaa ya mawe n.k.

Anyway uzuri Umeme hauluki nyumba, iwe ni ya kaki au kijani, Giza ni letu sote,
Ukiushinda nyumbani, utakushinda kazini/mtaani..
 
Kwani wanakosa cha kusema, utasikia Maji ndio yana pump Gesi.

Anyway, umeme wetu kwa kiasi kikubwa umeunganishwa na grid,
Pale unakutana umeme kutoka kwenye vyanzo vyote, unaunganishwa halafu unatolewa,

A) Kuna kiwango cha mwisho kabisa cha maji ili Mitambo iweze kuzalisha umeme, chini ya hapo ni kuzima baadhi ya generator(mgao) au kuzima Zote(Giza).

Lakini hivyo hivyo
B) Kuna kiwango cha chini kabisa cha Umeme kinahitajika ku operate zile plant pale ubungo na kufanya kazi bila shida na kwenda kwa wateja, hivyo basi shida ndogo ikitokea kule (A), impact kubwa itaonekana huku (B) hivyo
Ni either u shutdown mtambo mmoja(kama imegawanyika) upunguze uzalishaji, matokeo yake ni mgao maana Sio maziwa haya useme eti uwape nusu nusu au basi uzime plant nzima..

Yote kwa yote hii hailalalishi hii kata kata, kuna haja gani kuunganisha wote? Bora wangefanya kwa zones.
 
Ndo maana nikiskia mtu anasema mambo ya anaupiga mwingi natamani nimtie finga
 
Umasikini wa kujitakia bwana
Unaweza kuongea chochote na ukasikilizwa kwa sababu hakuna namna
Hapo na so called wasomi wanashangilia
 
Back
Top Bottom