Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,020
- 5,293
Wakuu,
Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule za Sekondari za Kagera River na Kituntu Sekondari zilizopo katika Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga zaidi ya bilioni nne kujenga shule mpya ya sekondari ya wasichana Kagera River, ambayo itakuwa mkombozi kwa watoto wa kike.
Aidha, wanafunzi wa Kituntu Sekondari wamesema kuwa miundombinu katika shule hiyo imeboreshwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi wa shule hizo wameanza kwa kuipongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa kutenga muda wa kuzitembelea shule hizo, ambazo zimenufaika na Awamu ya Sita.
Wamesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeongeza miundombinu ya elimu kwa kujenga shule mpya za wasichana nchini na kutenga baadhi ya fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule nyingine.
Mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Kagera River amesema kuwa anaomba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kumaliza baadhi ya changamoto zilizopo shuleni na kusema kuwa wanafunzi waliotimiza miaka kumi na nane hawatamuangusha Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumchagua tena aendelee kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akimalizia kwa kusema, "Rais Samia, mitano tena."
Reminatha January, mwanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Kituntu Sekondari, mchepuo wa HKL, amesema kuwa kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Kituntu Sekondari, anatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na walimu wa shule hiyo kwa juhudi kubwa walizozifanya shuleni hapo.