Kafulila: Rais Magufuli amesahau uchumi wa mnyonge

Sasa nimeanza kujua siasa
...kumbe sisi ndio wenye umeme nafuu Afrika Mashariki, Duuuuh!!!
 
Magufuli still the best ever president

In which way? When he took over the presidency I thought the same too, but now he turns out to be a laughing stock. I don't think he knows what he's doing. To make the matters worse he can't even talk convincingly in front of the nation. For instance, I remember watching a video clip of him "answering" a question about not involving the parliament in some of the decisions making. To my understanding he believes that he possesses more powers than any other government's branch, but he gave such a shallow answer in which he failed to explain where he's got those powers from to justify his argument.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpe Mgonja alifanya kazi nzuri sana akiwa katibu mkuu. Yeye aliachiwa na baada ya mahakama kumuona hana hatia. Ndugu Mgonja ndio alisimamia kikamilifu kuanzishwa kwa TRA na alipoondoka kama katibu mkuu aliacha hazina ina hali nzuri sana.
Mbona Proff. Muhongo alijiuzulu kwa kashfa ya Escrow na baada ya kubainika hakuhusika aliteuliwa kuwa Waziri tena.
Nakubaliana na wewe, namjua huyo Grey Mgonja, yuko vizuri sana kwenye hiyo wizara...
 
Noted.
Tumbili hana jipya amehama Ukawa amehamia Ukawa baada ya kuwa Compromised na Mkewe.
.. Zamani wakati nakua babu yangu alikuwa anapenda kuniambia..'' ingawa unaniangalia na macho yako makubwa lakini wala hunioni '' Sasa ingawa umepitisha macho kwenye huo uzi wa Kafulila lakini inaonekana hujaokota kitu...
 
Published on 8 Jan 2017
VIDEO: MADA MOTO NA DAVID KAFULILA MUELEKEO WA UCHUMI TANZANIA CHANNEL TEN


Source: Bin Seif
 
SOMA UCHAMBUZI WA KAFULILA KUHUSU UCHUMI MADA MOTO C.TEN JANA.IJUMAA 06,JAN,2017

Nikweli Serikali imejisifu kwa ukuaji wa uchumi wa asilimia7% , na nikweli kiasi hicho ni miongoni mwa rekodi ya juu ya ukuaji Afrika na dunia kwa ujumla kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za kimataifa.

Hata hivyo ifahamike kwamba rekodi hii imekuwepo na imendelea kuwepo tangu awamu ya Mkapa. kwani hotuba ya mwisho ya Awamu ya tatu, Bajeti ya 2005/06,ukuaji wa uchumi ulikuwa asilimia 6.9%. na imendelea kuwa hivyo miaka yote kwamba uchumi wetu unakua kwa asilimia 6%-7%.

Tatizo kubwa la ukuaji huu umeshindwa kupunguza idadi ya maskini.kwani maskani wanaongezeka kila mwaka.ndio sababu wasiojua nadharia za uchumi wanakataa kuamini kuwa uchumi unakua.

Ukuaji wa uchumi sio lazma upunguze umaskini. inategemea sana usimamizi wa uchumi huo.Kwenye uchumi kuna dhana mbili, UKUAJI WA UCHUMI na MAENDELEO YA UCHUMI. ukuaji wa Uchumi unapimwa kwa vigezo vya ongezeko la uzalishaji ndani ya mwaka katika nchi husika, bila kujali uzalishaji huo unahusisha watu wangapi, bila kujali ni wenyeji kiasi gani wanahusika.unapimwa kwa vigezo kama Kiasi cha uwekezaji, Mfumko wa bei, Mauzo nje, Manunuzi nje, Kiasi cha akiba(saving), Matumizi ya serikali, nk.

Maendeleo ya Uchumi yanapima ubora wa maisha ya watu. vigezo vyake ni kiasi gani mazingira ya uchumi yameboresha maisha ya watu, kama afya, elimu, maji, umeme, uwezo wa kumudu mahitaji, nk

Mkapa alikabidhiwa nchi ikiwa na mazingira magumu sana ya kiuchumi, lakini aliacha misingi imara ya kiuchumi. Kwa mfano riba za bank ilikuwa alikuta zaidi ya 26% ameacha 14%,Akiba ya fedha za kigeni alikuta ya miezi miwili, akacha ya miezi7, JK akabakiza ya miezi4 na itaendelea kuwa ya miezi4 kwa hali ilivyo,alikabidhiwa nchi haikopesheki akaacha deni la 10trilion,

JK ameacha zaidi trilion 40 na linazidi kupaa, changamoto pekee ambayo awamu ya nne ilipaswa kushughulika nayo ilikuwa kufanya ukuaji wa uchumi na misingi yake aloacha Mkapa itafsiri maendeleo ya uchumi kwa maana ya kuboresha maisha ya watu.

Awamu ya nne ilishindwa jukumu hilo kwa kiasi kikubwa na awamu ya tano haioneshi mwelekeo wa kupunguza maskini kwa kiasi kikubwa.

Sababu ya uchumi kukua bila kupunguza maskini ni pamoja na sekta zinazokua kiuchumi kubeba watu wachache au kuwa na athari ndogo kwa watu wengi.sekta ambazo ukuaji wake upo juu kwa miaka mingi ni Utalii, Madini, Mawasiliano, huduma za fedha, nk . ambazo kwa hakika zinabeba watu wachache.

Cha kufanya bado ni kuhakikisha kilimo katika dhana pana kinainuka, tangu miaka ya 2000s, Tafiti zilifanywa na Taasisi ya REPOA na kuonesha kwamba kilimo kikikuzwa japo kwa asilimia nane kwa miaka3 mfululizo kinaweza kupunguza idadi ya maskini kwa asilimia50%

Ni bahati mbaya kwamba kwa miaka yote kilimo hakizidi ukuaji ni asilimia3 ikianda sana 4% kwa zaidi ya miaka 20.na mbaya zaidi haionekani kama awamu hii inamsukumo katika eneo hilo.

Tafiti za REPOA zimeonesha uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya mbolea na tija katika kilimo. Kwa mfano kijijini eka ya mahindi iliyolimwa bila mbolea wanavuna kati ya gunia 3 mpaka5. Wakati eka iliyolimwa kwa mbolea mavuno ni gunia 20 mpaka30.hivyo mbolea inaongeza kwa kiasi kikubwa tija ya kilimo

Nasema awamu hii inaelekea haina mpango na wakulima kwasababu miaka yote tangu mfumo wa kutoa ruzuku kwenye mbolea, tija iliongezeka ingawa mbolea ilikuwa kiduchu.

Ripoti ya Poverty&Human Development ya 2014, inaonesha umuhimu wa sekta ya kilimo na hasa matumizi ya mbolea na kutoa mifano ambayo ni aibu kwetu.kwamba kwa wastani Mkulima China inatumia zaidi ya 260kg za mbolea kwa eka1, Tanzania tunatumia wastani wa 9kg kwa eka1. Inawezekana tukawa na hoja kwamba China ni taifa kubwa kiuchumi, lakn ripoti hiyo inaonesha hata Malawi, nchi dhaifu kiuchumi, wastani mkulima anatumia 29kg za mbolea kwa eka1.

Sasa tujiulize, kama huo wastani wa 9kg kwa eka ni wakati ruzuku ya mbolea ilitengwa walau. je sasa? maana mwaka 2015/16 , ruzuku ya mbolea ilikuwa 78bn, wakati mwaka huu 2016/17 ruzuku ya mbolea imeshuka mpaka 10bn.

Nivema Mhe Rais akatazama upya eneo hili. kiasi hiki cha ruzuku ya mbolea hakifanani na serikali ya wanyonge. repoti ya USAID, 2014, inaonesha watanzania walio kwenye kilimo ni asilimia70% na kati yao asilimia75% ni akina mama.

Nikweli nikiwa bungeni tulisema sana kuhusu aibu ya Taifa kukosa ndege, binafsi nakubaliana na uamuzi wa serikali kununua ndege. lakini sikubaliani na uamuzi wa serikali kutekeleza mpango mkubwa wa kuwa na shirika kubwa la ndege sasa. Lazma watanzania wajue kuwa biashara ya ndege ni ngumu mno duniani.

Na nchi nyingi hapa Afrika zinaendesha biashara hii kwa hasara ikiwemo Afrika ya kusini, Rwanda yenyewe pamoja na kununua Airbus juzi, lakn wanakiri kuendelea kutengeneza hasara isipokuwa wana malengo ya muda mrefu, Kenya Shirika lao hoi kwa madeni, Walau shirika la ndege Ethiopia wana nafuu, Biashara ya ndege duniani kwasasa imezidi kuwa ngumu, tunaona fahari ya Emmirates,

Lakini nchi hizi za falme ya kiarabu zimeamua ku pump mabilioni ya kutosha kwenye ndege kuwa wababe wa dunia kwenye usafiri huo kama mbadala wa mafuta ambayo wanajua yatakwisha au bei itakwisha sana kadiri ya muda.Ndio mana unaona wana ubavu wa kutikisa mashirika kongwe ya Ulaya kama KLM au British Air,

Hivyo hili la ndoto ya shirika kubwa la ndege maana yake tuwe tayari ku pump mabilioni ya kutosha kwa hasara ya miaka kadhaa . binafsi nakubaliana na ule msemo wa kupanga ni kuchagua. Je tunadhani hii inapaswa kuwa kipaumbele kiasi hicho? Nikweli ndio njia rahisi ya kuinua umaskini wa wanyonge? nadhani sio!

Uamuzi wa kutopandisha bei ya umeme kweli ni tija kwa wananchi na wenye viwanda, lakini naomba ieleweke tu kwamba Tanzania ndio nchi yenye bei ya chini ya umeme kuliko Rwanda, Kenya na Uganda. na ieleweke pia kwamba tatizo la viwanda Tanzania sio bei ya umeme bali umeme wa uhakika.

Sio affordability, but reliability. Pamoja na umeme wetu kuwa bei chini kiliko washindani wetu lakn kwasababu sio wa uhakika ni tatizo kwa viwanda kuliko hata nchi ambazo bei ipo zaidi yetu.

Pia ifahamike kwamba serikali inatumia fedha nyingi sana ya hazina ambayo ni kodi yetu kuliendesha shirika hili. zaidi ya bilioni 400 kila mwaka ni ruzuku inakwenda TANESCO. Hivyo tujue kwamba hata uamuzi wa juzi kuzuia bei kupanda, haina maana hauna madhara kwa wananchi kwani wanazuia bei kupanda na watapunguza bajeti ya elimu au dawa au kilimo au maji huko hazina ili kuibeba Tanesco.

Kwa hiyo ni sawa na kusema tumekubaliana gharama za umeme tubebe wote wenye umeme na wasio na umeme badala ya kuachiwa mwenye umeme peke yake. ndio ruzuku za zaidi ya 400bn huku mbolea kwa wakulima inaenda 10bn..afu tunasisitiza kuinua wanyonge

Mhe Rais amefanikiwa kuutikisa mfumo kwa kuutisha, anatisha, mfumo ambao kwa miaka yote ulikuwa very rigid. hilo nampongeza. ushauri wangu ni aende mbele sasa kutengeneza Katiba itakayotengeneza mfumo unaotisha dhidi ya ufisadi na uzembe.

Kama nchi tunahitaji mfumo unaotisha zaidi kuliko mtu anaetisha kwasababu mfumo upo leo na kesho lakini mtu yupo leo kesho hayupo. kama alikuja Nyerere akaondoka, Mwinyi, Mkapa na JK, wote wameondoka kama yeye atakavyondoka, lakin mfumo hata akiondoka atauacha.

Atekeleze agenda ya Katiba Mpya kutengeneza mfumo madhubuti na sheria, kwa mfano saivi ilipaswa apeleke mabadiliko ya sheria ya utumishi wa umma ili mengi anayoyafanya kwenye utumishi yawe kwa mujibu wa sheria, asipofanya anaweza kuingiza hasara kwani watumishi wengi watakwenda Mahakamani na kushinda kesi na kulipwa mabilioni.

Mambo mawili niliyasema sana nikiwa bungeni. mpaka mkutano wa bajeti wa mwisho June7,2015 nilisisitiza ilikuwa ni suala la kampuni za simu na migodi kuorodhesshwa kwenye soko la mitaji.Napongeza uamuzi wa serikali sasa kwamba kampuni za simu zimelazimishwa kuorodhesha hisa zoa kwenye soko la mitaji la Dar es saalam(DSE).

Kwa Kampuni za simu kuorodhesha hisa zao ni fursa kwa umma kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. lakini zaidi ni inatoa fursa kwa hesabu za kampuni hizi kufanyiwa uchunguzi na uchambuzi wa kutosha(sereous scruitiny).

Na hivyo kupunguza uwezekano wa kampuni hizi kuficha usahihi wa mapato na matumizi yao, kwani kampuni nyingi duniani zina tabia za kukuza gharama za uzalishaji na kupunguza mapato yake kwenye vitabu ili zionekane zinapata faida kiduchu ili kupunguza kodi ya faida.

Jambo la ziada kwa kampuni hizj za simu ni TCRA ihakikishe inanunua mtambo kurekodi matumizi ya simu ya simu zote ili serikali iwe na hakika zaidi ya mapato ya kampuni hizi. tangu mwaka 2007, sijawa Mbunge hoja hii imezungumzwa bungeni, lakn serikali ilikuwa na uzito saana.

Kitu pekee ambacho TCRA walifanya ni kununua mtambo wa kurekodi simu za nje tu. ambayo ni asilimia ndogo sana ya matumizi. Hii ni tatizo kubwa ambalo nadhani linahitaji msukumo wa Rais kwasababu watu wake wanavuta miguu kutekeleza kwa karibu miaka kumi sasa

Ni kweli hali ya mzunguko wa fedha kwenye uchumi ni mdogo sana. Nikweli kiasi fulani inatokana na serikali kuziba mianya ya dili. lakn tuseme kweli kwamba sio msingi wa ukubwa wa tatizo. kuna sababu nyingi, ikiwemo stracture ya deni letu na ulazma wa kulipa deni hilo. deni letu ni uwiano wa 80:20.

Kwamba asilimia 80% ni la nje. na limeiva kwa kasi. kiasi kwamba kila mwezi serikali inalazimika kulipa wastani wa 700bn. wastani makusanyo ya ndani ni 1100bn. lakini pia kwa kipindi cha mwaka mmoja huu serikali imekopa sana ndani kiasi cha kuvunja rekodi ya miaka yote. serikali imekopa karibu trilion2. kuanzia Novemba2015 mpaka Disemba 2016.

Miaka ya nyuma mikopo wa ndani kwa mwaka haikuwa inazidi 1trilion.na inakopa zaidi ndani kwasababu imekwama mikopo ya Ulaya. ndio mana umemsikia Waziri wa Fedha juzi akikiri kukosa mikopo nafuu na misaada toka Ulaya na kwamba wameamua kujielekeza nchi za Japan, China, Korea ya kusini, India,nk.

Sababu kubwa ya kukwama mikopo nafuu na misaada ni masharti ya siku zote kuwa Ulaya wanataka kuona demokrasia na utawala bora. ndio maana unamsikia waziri anasema mikopo mikwama kwasababu riba za ulaya zimepanda toka 6% mpaka 9% bila kusema huko upande wa pili riba ni kiasi gani?. tumevuruga uchaguzi zanzibar, sheria mbovu ya mitandao, vyama vya upinzani kuminywa na bunge gizani ndio siri ya ushirika wetu na ulaya kuchechemea.

Hali ni mbaya. tunajua sehemu kubwa ya miradi ya maendeleo inategemea misaada na mikopo nafuu toka nje. Baada ya kabanwa misaada na mikopo nafuu toka nje sasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka mzima ni chini ya 30% ya makisio ya bajeti. Hii ni kwa mujibu wa Monthly Economic Review Reports zinazotolewa na BOT kila mwezi. Makusanyo yetu ya mwezi yanaishia kulipa deni na mishahara tu

Kama tunalipa 700bn, na mishahara 560bn, wakati makusanyo ni wastani ni 1100bn, unategemea nini? ndio maana kwa mujibu wa repots hizo MER za BOT, inaonekana deni la ndani wakati awamu ya kwanza inamaliza muda wake ilikuwa 1.7trilion, na kwa miaka10 ya JK deni la ndani likafikia 7.5trilion na mwaka mmoja huu deni la ndani limefikia 10trilion kwa maana ya nyongeza ya zaidi ya 2trilion

Kasi zaidi ya serikali kukopa ndani inapunguza kiasi cha pesa kwenye mzunguko. lakini kwakuwa haina namna inabidi iwe hivyo, na hii inachochea kuzidi kushuka kwa shughuli za biashara(austerity economy).

Binafsi naamini Rais ana dhamira lakin inakosekana focus , hajawa strategic kufikia lengo lake analojipambanua kama Rais wa wanyonge. asipoangalia miaka 5 itamalizika bila kupunguza makali ya maisha na kubaki na orodha ya waliotumbuliwa. Huyo mvuvi ameuliza kwanini uvuvi baharini bado haupewi msukumo. Ndio msingi wa hoja yangu awali kwamba sekta ya kilimo katika dhana pana ambayo ni mazao, ufugaji na uvuvi, haijawa na msukumo

Tazama Nambia ukanda wa bahari kwajili ya uvuvi kwao una urefu wa 1500km na sisi 1400km, ni karibu sawa, lakn Namibia ndio wanaongoza kwa kuuza nje samaki ukanda wa kusini mwa afrika, na kwao baada ya madini,uvuvi ndio sekta ya pili ktk uchumi wao. Tunahitaji sera ya viwanda iwe ktk viwanda vya processing na mafacturing ya mali ghafi za kilimo. hivi ndio viwanda vinavyoajiri watu wengi dunian

KWA HIYO HAYA ULIYOANDIKA ILIKUWA PUMBA AU?
 
Nadhani huyu ndiye kijana lema alisema jana kwamba yupo mmbioni kurudi CCM, BADO WALE MAMEYA 2
 
Back
Top Bottom